waziri wa maji ingilia kati dawasa hali ya maji dar ni mbaya sana

LUS0MYA

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
865
1,103
Mheshimiwa waziri wa maji matatizo ya maji ya miaka kumi iliyopita yamerudi katika jiji la dar es salaam pamoja na kwamba hakuna taarifa ya kupungua kwa maji.Hali ni mbaya zaidi kwa dawasa kimara ambapo pamoja na kupitiwa jirani na bomba kubwa kutoka ruvu juu uhakika wa maji ni mdogo.
Hali ya utendaji imeshuka sana na upotevu wa maji unaonekana mabarabarani. Watumishi wasio waaminifu wanashirikiana na magari ya wauza maji ambayo mengi yanamikiwa kwa siri na watu wa dawasa.Huduma kwa wateja imekuwa mbovu na hata mwitikio wao umekuwa mbovu.mafundi wanaopita mtaani hawana sare wala vitambulisho hivyo inakuwa vigumu kuwatofautisha na vishoka.
 
Kwanini walimtoa yule muhandisi LUHENEJA sijui kama nimepatia pale DAWASCO na kumpeleka kazi na ajira sasa kwa VC ambako kimsingi hakuna kazi zenye madhara ya moja kwq moja kwa watu?
 
Back
Top Bottom