Waziri wa Madini, Dotto Biteko acharuka baada ya kushtukia ukiukaji wa sheria unaofanywa na mgodi wa North Mara

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,208
4,703
Imeelezwa kwamba mgodi wa North Mara umekiuka Sheria ya Ushirikishwaji wa Watanzania (local content) baada ya kutangaza zabuni nje ya nchi na kupata mzabuni kinyume cha Sheria za Madini.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Madini Doto Biteko baada ya kufanya ziara maalum mgodini hapo Desemba 18, 2020.

Kanuni za Madini (Ushirikishaji wa Watanzania), 2018 Tangazo la Serikali Na. 2/2018 zinataka wamiliki wa migodi kutangaza zabuni hapahapa nchini na endapo hakuna mtanzania mwenyewe sifa au vinginevyo, zabuni hiyo inatangazwa nje ya nchi na atakaepatikana atalazimika kushirikiana na Mtanzania.

Biteko alisema, kwa mujibu wa sheria hiyo, mgodi utakaokiuka utatozwa adhabu ya dola za kimarekani milioni tano.

Aliongeza kuwa sheria hiyo inalenga kutoa fursa ya watanzania katika kushiriki masuala ya uchumi wa madini.

Meneja Mkazi wa Mgodi wa North Mara, Hilaire Diarra, alikiri kosa la kutofuata sheria kwa kuwa walikuwa katika presha ya kutekeleza mradi huo. Diarra aliomba radhi na kwamba wapo teyari kufuata maelekezo yatakayotolewa na Serikali.

Kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeo ya jamii (CSR), Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila alihoji kuhusu utekelezaji wa (CSR). Meneja Mgodi anaeshughulikia Mahusino Gilbert alisema wametekeleza kwa kujenga madarasa, kujenga visima vya maji na masuala ya afya japo Prof. Msanjila alimwambia hawajafuata utaratibu unaotakiwa katika kutekeleza miradi ya CSR.

Kutokana na majibu hayo, Biteko aliuagiza wa mgodi huo kuanda mpango wa utekelezaji wa miradi ya CSR na kuwasilisha kwenye mamlaka ya serikali za mitaa ili waipitie na kuidhinishwa teyari kwa ajili ya kutekeleza.
 
Karibu mjini.

Umeliwa tayari na kumwagiwa hiyo mimba yako lea tu mkuu.

Hapa duniani ni kutesa kwa zamu huko aliko atawatambia sana rafiki zake kuwa kuna jamaa la kuja amelipiga laki 5.

Sent from my Infinix X622 using JamiiForums mobile app
 
Hatuhitaji mawazir wanaocharuka... tunahitaji sheria tabirishi hapa. Wala dunia haihitaji kutoa macho kama alivyofanya wazir wa maji UWESU. we need system and law in place co matamko. Wazir mkuu anajua ununuzi wa magar ya serikali upoje kwa kujibu wa sheria anapokuja kulalamika kutulalamikia juu ya ununuzi wa magari ya ma v8 ya MA DED kwetu ni nini basi kama siyo kufeli kwa mfumo ( pombe kunywa pombe mwanangu chapa kazi) weka sheria miaka 4 co mingi
 
Back
Top Bottom