Waziri wa habari awaasa wasanii juu ya katiba inayopendekezwa

nyimbag

Member
Feb 28, 2015
41
17
HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO MHESHIMIWA DKT. FENELLA MUKANGARA (MB) WAKATI WA KUFUNGA MKUTANO NA WASANII TAREHE 27 FEBRUARI, 2015 KATIKA UKUMBI WA UWANJA WA TAIFA, DAR ES SALAM

Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Viongozi wa Wasanii wa fani mbalimbali,
Wakurugenzi Wizara ya Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo,
Mtoa Mada,
Waandishi wa Habari
Mabibi na Mabwana
Habari za Mchana,

Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kufika siku ya leo na kuuona mwaka 2015. Niwatakie wote heri ya mwaka mpya, uwe wa baraka na mafanikio makubwa katika shughuli zenu za kila siku.

Nichukue nafasi hii kuwashukuru kwa kuitikia mwaliko wetu na kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Mkutano wa leo pamoja na majukumu mazito mlionayo.

Ndugu Wasanii,
Napenda kutoa pongezi za dhati kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kueleimsha Jamii katika masuala mbalimbali. Aidha kazi zenu zimekuwa ni chachu ya kuleta mabadiliko chanya katika Taifa letu na zimekuwa ni utambulisho wa Utaifa wetu nje ya Tanzania. Nawapongeza wote mlioshinda tuzo mbalimbali za kitaifa na kimataifa mmekuwa mstari wa mbele kuitangaza nchi yetu nje ya mipaka yetu kupitia usanii. Tunajivunia kazi zenu.

Ndugu Wasanii,
Niwahakikishie kuwa siku zote tupo pamoja na nimekuwa nikifuatilia kazi zenu mbalimbali, katika Luninga, kusikiliza Nyimbo, kuona michoro mbalimbali, ubunifu katika mavazi na sanaa zinginezo. Kwa hakika ubora wa kazi zetu za Sanaa naushuhudia ukiongezeka siku hadi hadi siku.

Ndugu Wasanii,
Kama mnavyojua mwaka huu 2015, Taifa letu linatarajia kuwa na matukio makubwa mawili, kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu. Serikali kwa kutambua umuhimu wenu, imeona ikutane na wadau wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa lengo la kuelimishana na kukumbushana kuhusu jukumu letu kama Wasanii katika kuelimisha na kuhamasisha umma katika masuala mbalimbali muhimu kwa taifa letu.

Katika Mkutano wa leo tutajikita zaidi katika kuelimishana juu ya wajibu wenu kama Wasanii katika kuielimisha Jamii kuhusu Katiba Inayopendekezwa na kujadili juu ya nafasi ya Sanaa/ Wasanii katika katiba inayopendekezwa, ikiwemo haki mbalimbali za Wasanii.

Ndugu Wasanii,
Taifa linatarajia kuendesha kura ya maoni tarehe 30 Aprili mwaka huu na ili zoezi hili lifanikiwe kwa kiasi kikubwa taaluma na nafasi yenu kama wasanii inahitajika kutumika kwa ufasaha na umakini mkubwa.

Ni ukweli usiopingika kuwa ili wananchi waweze kufanya maamuzi sahihi wakati utakapowadia ni vyema wakapata elimu kupitia njia mbalimbali hususan kupitia sanaa juu ya katiba inayopendekezwa, bila kusahau makundi yenye mahitaji maalum. Tunafahamu kwamba mna washabiki wengi ambao kupitia Sanaa mnaweza kuwaelimisha kuhusu mchakato wa upatikanaji wa Katiba Inayopendekezwa na umuhimu wa ushiriki wao katika kuunga mkono Katiba Inayopendekezwa.

Ndugu Waasanii,
Tumeona ni vyema sisi kama Wizara yenye jukumu la msingi la kuelimisha jamii katika masuala makuu ya kitaifa pamoja na nyinyi Wasanii tukawa na ufahamu wa kutosha juu ya mategemeo yetu kwenu katika jambo hili muhimu la Kitaifa. Hasa la kuinadi Katiba Inayopendekezwa, kuhimiza wananchi kujiandikisha na kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya maoni.

Kama mnavyofahamu na watoa mada walivyowasilisha kwenu kwamba katika Katiba Inayopendekezwa, yapo mambo mazuri yanayoendana na wakati uliopo sasa ukilinganisha na Katiba ya Mwaka 1977. Naamini kabisa baada ya kikao hiki, mmepata uelewa zaidi na ukweli kuhusu katiba Inayopendekezwa.

Tumieni sasa nafasi yenu kuwafikia wananchi kwa weledi na usahihi. Waifahamu Katiba Inayopendekezwa, wajiandikishe na kuipigia kura hapo ifikapo Aprili 30, 2015. Ni ukweli usiopingika kuwa Katiba Inayopendekezwa imesheheni haki za makundi mbalimbali bila kusahau kundi la wasanii na haki zenu zilizofafanuliwa vizuri katika Ibara ya 59 ya Katiba Inayopendekezwa. Hii inamaanisha kwamba wasanii kwa mara ya kwanza kilio chenu kuhusu ulinzi na haki zetu kikatiba umezingatiwa. Hivyo kazi zenu za ubunifu zitaweza kulindwa kikatiba

Ndugu Wasanii,
Nimeelezwa Mada zilizowasilishwa na kujadiliwa leo, zimetolewa na mtu mahiri ambaye alishiriki katika Bunge Maalum la Katiba. Hivyo ni matumaini yangu kwamba kupitia kwake tutaongeza uelewa wetu juu ya wajibu wetu na umuhimu wa Katiba Inayopendekezwa. Ni matumaini yangu kwamba tumesikiliza, tumeuliza maswali, tumejadili na kutoa maoni ambayo yatatusaidia kutoa elimu sahihi kwa umma. Hasa kwa kuisemea na kuitangaza Katiba Inayopendekezwa kwa mlengo wa kuvuka katika kura ya maoni na wingi wa kura ya Ndiyo.

Ndugu Wasanii,
Kwa mara nyingine nitumie nafasi hii kipekee kuwashukuru na kuwapongeza kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya ya kuelimisha na kuburudisha Jamii bila kusahau kulitangaza Taifa la Tanzania .

Mwisho nawaomba sana tusaidiane katika kufanikisha hili jambo muhimu tuweze kuendelea kujipanga vizuri katika kujenga na kuilinda nchi yetu.

Niwashukuru tena kwa kuja na kushiriki nasi na niwatakie kazi njema ya kulijenga Taifa letu.

Asanteni!
 
Hii serikali ni ya ajabu sana. Walisema vikundi na taasisi zinazotaka kutoa elimu ya uhamasishaji wa kura ya katiba pendekezwa wapeleke barua za maombi. Baadhi ya waliopeleka barua hawajajibiwa, wao wanawaomba wasanii wahamasishe kura ya NDIYO! Hovyo kabisa hawa wabaka demokrasia na haki za raia
 
Hivi kati ya Rais na wizara nani alitakiwa atangulie kuwapongeza wasanii kwa kazi zao na mchango wao mkubwa kwa taifa. Kweli ukiwa na watu wazito, hukawii kuonekana una maslahi binafsi.
 
Duh! Yaani hiyo ndio hotuba ya waziri?

Hivi haoni hata aibu? Kweli waziri anaongeo hivyo.

Nilitegemea aonyeshe hiyo katiba kipengele kwa kipengele ambacho kundi hilo litafaidika katika katiba Mpya.

Nilitegemea aonyeshe utofauti wa katiba ya sasa na hiyo mpya juu ya hao wasanii.

Ok wasanii msikubali kutumia katiba mpya bado ni mwiba kwenu na vizazi venu.

Watch out, don't vote
 
Unaposema kuwa hajazungumzia kipengele kinachowagusa wasanii na hiki?

Tumieni sasa nafasi yenu kuwafikia wananchi kwa weledi na usahihi. Waifahamu Katiba Inayopendekezwa, wajiandikishe na kuipigia kura hapo ifikapo Aprili 30, 2015. Ni ukweli usiopingika kuwa Katiba Inayopendekezwa imesheheni haki za makundi mbalimbali bila kusahau kundi la wasanii na haki zenu zilizofafanuliwa vizuri katika Ibara ya 59 ya Katiba Inayopendekezwa. Hii inamaanisha kwamba wasanii kwa mara ya kwanza kilio chenu kuhusu ulinzi na haki zetu kikatiba umezingatiwa. Hivyo kazi zenu za ubunifu zitaweza kulindwa kikatiba
 
Unaposema kuwa hajazungumzia kipengele kinachowagusa wasanii na hiki?

Tumieni sasa nafasi yenu kuwafikia wananchi kwa weledi na usahihi. Waifahamu Katiba Inayopendekezwa, wajiandikishe na kuipigia kura hapo ifikapo Aprili 30, 2015. Ni ukweli usiopingika kuwa Katiba Inayopendekezwa imesheheni haki za makundi mbalimbali bila kusahau kundi la wasanii na haki zenu zilizofafanuliwa vizuri katika Ibara ya 59 ya Katiba Inayopendekezwa. Hii inamaanisha kwamba wasanii kwa mara ya kwanza kilio chenu kuhusu ulinzi na haki zetu kikatiba umezingatiwa. Hivyo kazi zenu za ubunifu zitaweza kulindwa kikatiba

Hiyo ibara inasemaje? Kusema ipo ibara 59 ndio nini?

Hotuba ingelenga hiyo ibara kwa kuwachambulia.

Kwa maana hiyo anakili wasanii hawana haki yao kwa sasa?

Wahi ubwabwa Mbezi
 
Ibara imetambua haki za wasanii kubuni na kusimamia haki zao. Imeweka wazi kuwa kutakuwepo na sheria zitakazotungwa kuhakikisha wasanii wanalindwa
 
Back
Top Bottom