Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,409
- 13,260
Waziri wa habari aliyepita alilifungia gazeti la MWANAHALISI kwa muda usio julikana ingawa baadaye mahakama ili liruhusu baada ya kushinda kesi. Lakini wakati likiwa kifungoni habari ziliendelea kutoka kupitia njia nyingine kama kupitia mitandao hasa Mwanahalisi on line na baadaye gazeti jingine lijulikanalo kama MAWIO
Alipoingia waziri Nape yeye akadhani kufuta gazeti ndio kufungia habari. Akalifuta MAWIO lakini habari zimeendelea kutoka kama kawaida kupita magazeti mengine kama MSETO na mitandao.
Ninacho taka mawaziri wanaoshika wizara ya habari na utamaduni wajue ni kuwa wanaweza kufungia na kufuta magazeti, TV na redio lakini lakini hawezi kufungia au kufuta habari. Hata sasa wamejitahidi kuzuia matangazo ya bunge lakini yote yanayojadiliwa huko bungeni yanapatikana kwa urahisi kutokana na kukua kwa teknolojia. Mimi nawashauri waache kupambana na wakati na kuitia hasara serikali kwa kupambana na vyombo vya habari.