Waziri Ummy: Deni kubwa la matibabu ya nje lililoibuliwa na CAG halihusu Serikali ya Magufuli tu,ni malimbikizo ya nyuma

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Leo tena waziri wa Afya bi Ummy Mwalimu ameendelea "kujibu" report ya CAG.Waziri Ummy anasema eneo la deni la matibabu ya nje lililotajwa na CAG sio la awamu ya Tano,bali ni mrundikano wa madeni ya miaka ya nyuma,na hivyo serikali ya awamu ya tano isibebeshwe kana kwamba deni hilo limepatikani ndani ya miaka miwili ya uongozi wa awamu ya Tano.

Waziri Ummy anasema ili kukabiliana na deni hilo,serikali ya awamu ya tano kupitia wizara yake imesitisha ulipaji wa deni hilo mpaka wapate uhakiki,kwamba hili deni za zaidi ya mabilioni linahusisha nini hasa?Serikali inataka kujua kama deni hilo ni mjumuisho wa dawa,malazi na "Consultation Fee?".Serikali itakapojiridhisha basi ndio itaanza kulipa deni hilo.

Maana kuna uwezekano mtu akaondoka hapa kama kiongozi wa serikali,anasema anakwenda kutibiwa moyo,lakini kumbe anakwenda kupata huduma ya kupandikiziwa mimba sababu ya matatizo ya uzazi,kitu ambacho katika "packages" ya matibabu yanayofadhiliwa na serikali nje ya nchi,hili la kupandikizwa mimba sio sehemu ya "packages" hizo.

Ummy Mwalimu anasema ili kuondoa kabisa mambo ya kwenda kutibiwa nje,serikali ya awamu ya Tano imeboresha Hospitali ya Muhimbili hasa kitengo cha Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambapo sasa watu wengi wanafanyiwa upasuaji hapo,pia serikali sasa imeongeza nguvu katika huduma ya kupandikiza figo,hivyo watu hawatalazimika kwenda nje ya nchi na hivyo kupunguza na baadae kuondoa kabisa gharama za kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Hawa watu wanaambiwa lakini hawataki kusikia kabisa,huyu Harrison naye ni mwanasheria mkubwa tu,tena wa kiwango cha PhD lakini anakwepeshakwepesha hoja ya msingi,kwamba wao sio maafisa masuhuli,hivyo hawapaswi kujibu,Naibu Spika naye sbb kawekwa pale na muhimili wa serikali,basi hasimamii misingi ya bunge lake,anatetea tu upande wa serikali.

Haya mambo wanaelezea waandishi wa habari si ya kitaalamu,wanapiga tu siasa,hawabanwi kwa maswali,ni kuongea tuuu,na hakuna "data" wanazotoa zaidi ya maneno tu.Ndiyo maana sheria ilitaka PAC na LAAC ndio waipokee report hii toka kwa Maafisa Masuhuli,na hawa maafisa masuhuli wangekutana na maswali ya wabunge wanaounda hizi kamati,sasa hawa waandishi wa habari baadhi yao wasio hata na semina ya namna ya kuisoma na kuichambua report ya CAG wanauliza nini?

Afisa Masuhuli ni afisa mwenye mamlaka ya juu na wajibu wa kusimamia na kutoa taarifa kuhusu matumizi ya fedha zilizotolewa kwa taasisi yake kutoka hazina baada ya kuidhinishwa na bunge. Kwa kiingereza wanaitwa "Accounting Officers".

Hili jina halimaanishi kuwa ni wahasibu, hapana.Linamaanisha kwamba wao ndiyo wawajibikaji wakuu katika taasisi- "they are accountable of every shilling".

Hata katika marejesho ya masurufu na maduhuli, ni afisa masuhuli ndio yuko accountable kwa CAG kuhusu matumizi mabaya ya masurufu na maduhuli.

Wengi wanafikiri mawaziri ndio "mabosi" kule mawizarani, kumbe wao ni mabosi kisiasa tu,nguvu ziko kwa Katibu Mkuu, ambapo waziri lazima amuone ili kujipatia fungu la ziada.Sasa hii awamu ya Tano,hawa mawaziri wanakuja hadharani tena kwa waandishi wa habari na kununua Airtime kwenye Tv hawaoni kiwa ni uvunjaji wa sheria?Kwani wasiwasi wao ni nini?Yaani ni hiyo 1.5T ndio inawatoa jasho hivi?Waseme tu waliepeleka wapi na waache nafasi ya bunge kupitia PAC na LAAC iwahojinna kuwabana maafisa masuhuli

Hii kujibujibu ni kutaka kusema hii serikali haina wezi??Kwanini wanavunja utaratibuuu?Halafu kila mtu akija anasema "Sehemu kubwa ya hii report ya CAG ni ya miaka ya nyuma,hadi July 2017,lakini baada ya hapo,serikali ya awamu ya tano imebadilisha sana mambo".Kwanini wanaitoa serikali ya Awamu ya Tano katika hizi tuhuma za CAG.

Soma: Ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka ulioishia 30 juni, 2017, imejaa madudu
 
Mbona umeshikia sana bango hili swala, hapa ndipo unapopatia ujira wako nini? Mbowe & Co. wanaiba Mabilioni wengine mmekalia kumpigia makofi, achaneni na Raisi na Serikali yetu, you can go hang!
 
Wewe barafu punguza kurefusha mdomo mnataka muongee pekee yenu...mueneze uongo na hamtaki watu wajibu hoja.....mnataka nyie muongee peke yenu wengine wasiseme......Lazima watoe maelezo kwa sababu kuna hatua zimesha chukuliwa sio lazima kuwasubiri makatibu wakuu...

Kwakuwa mliligeuza hili jambo ni la kisiasa hasa ninyi na hamtaki wenzenu waongee mtulie sasa watu wajibu hoja kama sio za kweli mseme sio kujificha kwenye kichaka cha makatibu wakuu
 
"Maana kuna uwezekano mtu akaondoka hapa kama kiongozi wa serikali,anasema anakwenda kutibiwa moyo,lakini kumbe anakwenda kupata huduma ya kupandikiziwa mimba sababu ya matatizo ya uzazi"

Nimenukuu. Hahahaha just hahaha. Hili sio dongo kweli?
 
Ukishaona Kiongozi anajibu tuhuma kwa ama kufanya reference ya awamu zilizopita au kuzisingizia bila kujibu ' Hoja ' za msingi kwa wakati uliopo jua huyo ni hasara kubwa si tu kwa Familia yake na Koo yake bali hata kwa Tanzania nzima kama pia siyo dunia nzima.
 
You my Teacher anamtetea Mzee, unakumbuka You my Teacher ulimsemea Mwali kwa mzee kuwa hakuheshimu sasa Mwali amepata kazi kubwa kanda ya Afro.
You my Teacher ulikutana na Mwali kwenye mkutano kule nchi flani na ukamwambia yaliyopita yamepita, kumbe ule umbea wako You my Teacher ulikuwa baraka kwa msichana Mwali.

You my Teacher mzee hatakuwa na hii nafasi milele.
 
Mbona umeshikia sana bango hili swala, hapa ndipo unapopatia ujira wako nini? Mbowe & Co. wanaiba Mabilioni wengine mmekalia kumpigia makofi, achaneni na Raisi na Serikali yetu, you can go hang!
Deni hilo ni pamoja na Mimba ya kichinda ya Mke wa BASHITE. Deni hilo pia linahusu Serikali za nyuma zilizokuwa chini ya CHADEMA, CUF, PPT MAENDELEO NA NCCR
 
Wewe barafu punguza kurefusha mdomo mnataka muongee pekee yenu...mueneze uongo na hamtaki watu wajibu hoja.....mnataka nyie muongee peke yenu wengine wasiseme......Lazima watoe maelezo kwa sababu kuna hatua zimesha chukuliwa sio lazima kuwasubiri makatibu wakuu...
Kwakuwa mliligeuza hili jambo ni la kisiasa hasa ninyi na hamtaki wenzenu waongee mtulie sasa watu wajibu hoja kama sio za kweli mseme sio kujificha kwenye kichaka cha makatibu wakuu
Wewe nawe umekuwa kama washindiliwa , tunataka Maafisa Masuuli ndio wajibu Hoja sio blah blah za Mawaziri aina ya MPINA
 
Serikali haina awamu. mbona hawajajenga ikulu mpya kwa ajili ya awamu ya tano.Pia CAG hakusema deni la awamu ya tano. bali amesema deni la serikali ya Tz tena kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017. Watu wengi Tz wana wanavyeti lakini elimu wameacha shuleni na vyuooni.
Wapo tayari kusema lolote ili wamfurahishe,wapendwe zaidi.
 
Back
Top Bottom