tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ameagiza kuwekwa ndani kwa wakandarasi wa kampuni kutoka China ambao wameshindwa kutimiza masharti ya mkataba wa ujenzi wa barabara ingawa serikali imetimiwa wajibu wake kwa kulipa sehemu ya malipo.
Ulega amesema juhudi za kutaka vigogo wa kampuni hiyo kuja nchini na kutoa maelezo kuhusu kusuasua kwa ujenzi wa barabara waliyopewa kujenga mkoani Dodoma, zimegonga mwamba hadi sasa na sasa kuna uwezekano wa kuwafikisha mahakamani kwa kukiuka masharti ya mkataba.
Kampuni hiyo China First Highway Engineering Co. Ltd.imepewa kazi ya ujenzi wa Sehemu ya pili ya barabara ya Ntyuka- Mvumi Hospitali- Kikombo (Km 53) na ingawa tayari imepewa asilimia kumi ya malipo (kiasi cha shilingi bilioni 9.68) ujenzi umefikia asilimia mbili tu