Waziri SMZ apinga Muungano wa serikali mbili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri SMZ apinga Muungano wa serikali mbili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makaimati, Jul 15, 2011.

 1. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [h=2]Waziri SMZ apinga Muungano wa serikali mbili[/h]Na Mwinyi Sadallah

  Waziri wa Kilimo na Maliasili wa Zanzibar, Mansoor Yussuf Himid, amevunja ukereketwa na kusema mfumo wa serikali mbili katika sura ya Muungano umepitwa na wakati na kwamba, sasa unaruhusu kuwapo kwa serikali tatu.

  “Hapa mpango wa serikali moja hatutaki kulisikia. Mfumo huu butu wa serikali mbili. Sasa basi twende kwa jambo, ambalo kila mmoja wetu analizungumza, la serikali tatu na mengineyo,” alisema Mansoor katika mchango wake kwa makadirio ya bajeti ya Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati.


  Alisema sura ya sasa ya Muungano imegeuka ndoana kwa Zanzibar na inatumika kuwa uwanja wa vitisho kwa Zanzibar inapodai haki zake kama nchi iliyochangia kuundwa kwa Tanzania baada ya kuungana na Tanganyika.

  Alisema inashangaza kuibuka kwa viongozi katika Bunge la Muungano kushikia bango suala la mafuta kuwa si raslimali ya Zanizbar kwa maelezo kuwa yapo katika mpaka wa bahari kati ya Tanga na Zanzibar.

  “Mimi sitaki kuwataja kwa majina, lakini niseme nawaonea huruma tu, wameishiwa. Lakini hawa ni wale wenye fikra za miaka hiyo ya kutisha Zanzibar hii kwamba wanaona kusimama bwana mkubwa, watu wanaanza kutetemeka,…huku hayo yamepitwa na wakati,” alisema Mansoor.

  Ingawa hakuwataja, lakini Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, hivi karibuni kwa nyakati tofauti kila mmoja alitoa kauli ya kukemea tabia ya kuzungumza suala la Muungano kwa jazba na kuonya kuwa kuanzisha mfumo wa serikali tatu ni kuunda mpinzani dhidi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
  Mansoor alisema ili kuondokana na vitisho vinavyotolewa dhidi ya Zanzibar, kazi kubwa inayowakabili wawakilishi, akiwamo yeye, ni kuwandaa Wazanzibari juu ya namna ya kushiriki kwa ufanisi katika utoaji maoni ya katiba mpya.
  “Tukawaelimishe na kuwaandaa Wazanzibari namna ya kujadili na kuzungumza upya makubaliano ya Muungano,” alisema Mansoor ambaye pia ni Mjumbe wa NEC, Mweka Hazina wa CCM na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar (BLM).

  Aliongeza kama wapo Wazanzibari wanaogopa kuanzisha suala hilo, kwa kauli hii yeye ndio anaanzisha mchakato huo. Kuhusu suala la mafuta na gesi asilia, alisema uamuzi uliopitishwa na BLM na Baraza la Wawakilishi (BLW) wa kuiondoa sekta hiyo katika orodha ya mambo ya Muungano ndio wa mwisho wa malumbano yanayohusu suala hilo.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2014
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
 3. N

  NJALI JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2014
  Joined: Jan 9, 2014
  Messages: 1,539
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  Wakiwa bungeni wanataka serikali mbili wakienda zanzibar wanataka serikali tatu! Mbona wazanzibar hawajiamini? Watoe tamko moja kwamba wanataka mbili tatu au moja? Kisha mambo mengine yaendelee. Wazanzibar mabingwa wa kulalama wakiwa nje ya bunge la Jamhuri. Hapo punde utasikia kauli ya sirikali ikitolewa kupinga kauli ya waziri wa utalii kuwa haikuwa ya sirikali bali ni yake binafsi. Yale yale ya MASELE NA tamko lake la barozi wa Uk.
   
 4. Zatara

  Zatara JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2014
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 549
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Nafikiri huyo waziri alifukuzwa kwa misimamo yake isiyoyumba. kwani ali
  endelea kushikilia msimamo wake. Taarifa za karibuni ni kwamba ameshajiunga na chama cha CUF.
   
 5. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2014
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 160
  ...naona huyo waziri faham zimeanza kumrudia....
   
 6. Edward Sambai

  Edward Sambai JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2014
  Joined: Nov 16, 2013
  Messages: 2,352
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  Wakiwa dodoma "mbili" wakirudi Zenji "tatu"

  Mi nashauri BMK lifanyikie Zanziba.
   
 7. k

  kupweteka Member

  #7
  Jun 17, 2014
  Joined: Feb 26, 2013
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapewe nchi labda watakula bata,kwanza nchi yao ndogo wakiamua kuijenga wanaweza
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Jun 17, 2014
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwani kuna mtu kawakataza kuijenga "nchi" yao?
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Jun 17, 2014
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kweli kajiunga na CUF, amevuna alichopanda!
   
Loading...