Waziri Sitta aikosoa serikali tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Sitta aikosoa serikali tena

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 2, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema hasara ambazo taifa limepata kutokana na mikataba mibovu ni matokeo ya kasoro zilizopo katika mfumo wa utoaji wa elimu nchini.Sitta alisema hayo juzi usiku kwenye Sherehe za Maadhimisho ya miaka 10 ya Shirika la HakiElimu zilizofanyika jijini Dar es Salaam.Alisema kasoro hizo zimesababisha mfumo huo wa elimu nchini kuzalisha watendaji mafisadi, wasiokuwa na maadili katika utendaji.

  Sitta alisema sekta ya elimu ni kama imepewa kisogo, kiasi kwamba hakuna uwiano wa kiutendaji wa watu wanaohitimu mafunzo mbalimbali ikilinganishwa na vyeti vyao vinavyoonyesha kwamba walifanya vizuri darasani.

  "Tumeshuhudia miaka 10 iliyopita, serikali imeingia hasara kutokana na baadhi ya viongozi kukosa uadilifu, wakaliingizia hasara taifa kwa kusaini mikataba feki," alisema Sitta na kuongeza:"... Hayo yote ni kwa sababu ya kuipa kisogo sekta ya elimu. Hii inatoa viongozi wasiojiamini na wanaokosa maadili."
  Hii ni mara ya pili kwa Sitta kuikosoa serikali ambayo yeye ni mmoja wa mawaziri wake.

  Moja ya mambo ambayo Sitta amewahi kuipingana na serikali ni malipo ya fidia kwa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans Tanzania Ltd.Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), alitaka serikali isiilipe fidia ya Sh94 bilioni kwa kampuni hiyo akieleza kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuhujumu uchumi wa nchi.

  Katika hotuba yake juzi, Sitta alisema serikali inawajibika kuhakikisha inawekeza katika sekta ya elimu ili kuwaandaa viongozi wenye nidhamu na maadili."Tunataka viongozi wajiamini wakiwa kazini na waweze kutetea maslahi ya nchi, vinginevyo nchi itaendelea kuzalisha viongozi wajanja wajanja na wahuni tu," alisema.

  Waziri Sitta alitaka Shirika la HakiElimu kuendelea kusema ukweli na kufichua mambo yanayodidimiza elimu kwa maslahi ya watu wachache wenye nia mbaya.Alisema kwa bahati nzuri kwa sasa yupo serikalini na kuahidi kuwa balozi wa HakiElimu na kuwatetea pale watakapobezwa na kutishwa na baadhi ya watu wenye nia mbaya wanapoeleza ukweli.“Napenda kuwaambia kwamba nitakuwa balozi wenu na kuwaunga mkono na nitaendelea kuwa pamoja na nyie hadi tuhakikishe tunaleta maendeleo katika sekta ya elimu mchango wenu ni mkubwa sana,”alisema Sitta.

  Serikali ya Awamu ya Tatu ilitishia kuifungia HakiElimu na kuionya kuacha kutumia matangazo yake katika vyombo vya habari, kueneza chuki miongoni mwa watoto na vijana nchini. Matangazo ya HakiElimu ambayo yaliiudhi serikali ni pamoja na lile serikali kueleza kuwa uchumi unapanda wakati hali ya wananchi bado duni. Jingine ni lile lililoonyesha matatizo sugu ya walimu wanaofanyia kazi maeneo ya vijijini.

  Tangazo hilo lilimuonyesha mwalimu akitumia siku mbili kufuata mshahara mjini. Akitumia baskeli lakini anapofika benki anakuta mshahara bado haujaingizwa.

  Waziri Sitta ambaye alikuwa Spika katika Bunge la Tisa, alisema kila mtu anatambua mchango na umuhimu wa HakiElimu tangu kuanzishwa kwake mwaka 2001, hivyo hakuna haja ya shirika hilo kuogopa kusema ukweli katika harakati za kuboresha elimu nchini.“Ukweli ni kwamba katika nchi zilizoridhia makubaliano ya Dira ya Elimu ya mwaka 2015 na katika Jumuiya ya Afrika Mashariki tuna nchi tano, lakini Tanzania ni ya mwisho kielimu. Hali hii inatishia uhai wa nchi,” alisema Sitta.Alisema kuwa elimu bora inaweza kumbadili mtu kitabia na kiuchumi na hivyo kumfanya ajiamini.

  Hata hivyo, Waziri Sitta alisema tofauti na ukweli huo, sasa umaskini hasa kwa watu wa hali ya chini nchini, unazidi kuongezeka huku baadhi ya viongozi wasiokuwa na maadili wakiendelea kulipeleka taifa kusikokuwa na mwelekeo.

  Waziri Sitta alifafanua kuwa mtu hapimwi kwa ufaulu wa mitihani na shahada alizonazo, bali anapimwa kutokana na utendaji wake na maadili mema kazini na kuwa mstari wa mbele katika kulinda maslahi ya taifa.“Kiongozi hapimwi kwa shahada, vyeti wala kiwango cha ufaulu wa mitihani yake, maana Tanzania ina viongozi wengi wenye shahada na vyeti kibao, lakini wanayofanya viongozi hao wenye shahada, wote tunayajua,” alisema.

  Awali, akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya HakiElimu Joaquine De-Mello alisema hadi wanapoadhimisha miaka hiyo kumi tangu kuanzishwa kwa shirika hilo, Hakielimu imepitia changamoto nyingi ikiwamo vitisho wanapojaribu kueleza ukweli.

  “Tumepitia milima na mabonde maana siku zote mtu anayeeleza ukweli anaonekana ni mchochezi, lakini baadhi ya watu wametambua mchango wa HakiElimu na baadhi yao hadi sasa hawatambui mchango wetu katika harakati za kuleta maendeleo ya elimu nchini,” alisema De-Mello.

  Alizitaja changamoto nyingine inazoikabili HakiElimu kuwa ni upatikanaji wa taarifa katika taasisi zinazosimamiwa na serikali.Alisema baadhi ya watendaji katika taasisi hizo, hawataki kueleza ukweli wakidhani HakiElimu inataka kupotosha jamii."Sisi lengo letu siyo kupotosha, tunataka kuielimisha jamii na kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu na wanafunzi kupata elimu yenye manufaa na kumwezesha kujiajiri na kuajiriwa," alisema.

  De-Mello alitaja kikwazo kingine cha maendeleo ya elimu nchini kuwa ni baadhi ya viongozi kutaka kuchanganya elimu na siasa…"Hii ni hatari katika maendeleo ya elimu ambayo ndiyo mhimili wa kila jambo duniani."
   
 2. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  wewe mtu kashindwa wizara ya mawasiliano na uchukuzi eti anapewa elimu unategemea nini hapo sababu elimu ndio uti wa mgongo kwa kila taifa tusubiri tu mpaka nchi imfie mtu mikononi mwake
   
 3. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Wednesday, 02 March 2011 00:04

  Gedius Rwiza

  Chanzo: Mwananchi
   
 4. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  nawakubali sana hawa haki elimu...mwiba kwa serikali
  unaikumbuka ile ya Kinjeketile Ngwale,mwalimu anajibu "hivyohivyo"
   
 5. M

  Marytina JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Naam!
  jk na mazimwi wengine like Chenge,RA,EL walidhani kwa kumwondoa kwenye kiti cha uspika watakuwa wamemfunga mdomo.
  Siasa za leo zinamtaka mtu awe mkweli ili hata kama atafukuzwa CCM ukubalike CDM.
   
 6. A

  AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sita endelea kuwaambia ukweli mpaka watakapojirekebisha
   
 7. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Ni kweli alichosema sitta hata mimi ninaamini kabisa kuwa, ufaulu wa watoto wetu siku hizi ni wa kiujanja ujanja wazazi wanashiriki katika wizi wa mitihani na kutengeneza vyeti feki matokeo yake wahitimu wanakuwa mafisadi tangu shuleni.TUMEKWISHA
   
 8. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nashindwa kuelewa Samueli SITA kuendelea Kuwa katika chama ambacho Mzee wa Vijisenti ni mwenyekiti wa Nidhamu. Naamini hapati usingizi kuwa katika chama ambacho uovu kwao ni ujanja.
   
 9. W

  WildCard JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Alipanga nyumba ya dola elfu nane kwa mwezi alipokuwa Spika. Mkataba gani huo kwa nyumba za Dodoma? Maslahi na mafao ya sasa ya Wabunge ameyasimamia yeye kwa nchi masikini kama hii. Wabunge wamekuwa wakilipwa posho sitasita naye akitazama tu. Mnafiki kweli huyu baba.
   
 10. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kaza buti sitta walikuchakachua kwenye uspika wakadhani watakua salama endelea kuwasha moto hivyo hivyo.
   
 11. M

  MAPINDUZI75 Member

  #11
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Waziri Sitta arusha tena kombora Serikalini

  [​IMG] Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta

  Gedius Rwiza
  WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema hasara ambazo taifa limepata kutokana na mikataba mibovu ni matokeo ya kasoro zilizopo katika mfumo wa utoaji wa elimu nchini.Sitta alisema hayo juzi usiku kwenye Sherehe za Maadhimisho ya miaka 10 ya Shirika la HakiElimu zilizofanyika jijini Dar es Salaam.
  Alisema kasoro hizo zimesababisha mfumo huo wa elimu nchini kuzalisha watendaji mafisadi, wasiokuwa na maadili katika utendaji.

  Sitta alisema sekta ya elimu ni kama imepewa kisogo, kiasi kwamba hakuna uwiano wa kiutendaji wa watu wanaohitimu mafunzo mbalimbali ikilinganishwa na vyeti vyao vinavyoonyesha kwamba walifanya vizuri darasani.

  "Tumeshuhudia miaka 10 iliyopita, serikali imeingia hasara kutokana na baadhi ya viongozi kukosa uadilifu, wakaliingizia hasara taifa kwa kusaini mikataba feki," alisema Sitta na kuongeza:"... Hayo yote ni kwa sababu ya kuipa kisogo sekta ya elimu. Hii inatoa viongozi wasiojiamini na wanaokosa maadili."
  Hii ni mara ya pili kwa Sitta kuikosoa serikali ambayo yeye ni mmoja wa mawaziri wake.

  Moja ya mambo ambayo Sitta amewahi kuipingana na serikali ni malipo ya fidia kwa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans Tanzania Ltd.Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), alitaka serikali isiilipe fidia ya Sh94 bilioni kwa kampuni hiyo akieleza kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuhujumu uchumi wa nchi.

  Katika hotuba yake juzi, Sitta alisema serikali inawajibika kuhakikisha inawekeza katika sekta ya elimu ili kuwaandaa viongozi wenye nidhamu na maadili."Tunataka viongozi wajiamini wakiwa kazini na waweze kutetea maslahi ya nchi, vinginevyo nchi itaendelea kuzalisha viongozi wajanja wajanja na wahuni tu," alisema.

  Waziri Sitta alitaka Shirika la HakiElimu kuendelea kusema ukweli na kufichua mambo yanayodidimiza elimu kwa maslahi ya watu wachache wenye nia mbaya.Alisema kwa bahati nzuri kwa sasa yupo serikalini na kuahidi kuwa balozi wa HakiElimu na kuwatetea pale watakapobezwa na kutishwa na baadhi ya watu wenye nia mbaya wanapoeleza ukweli.“Napenda kuwaambia kwamba nitakuwa balozi wenu na kuwaunga mkono na nitaendelea kuwa pamoja na nyie hadi tuhakikishe tunaleta maendeleo katika sekta ya elimu mchango wenu ni mkubwa sana,”alisema Sitta.

  Serikali ya Awamu ya Tatu ilitishia kuifungia HakiElimu na kuionya kuacha kutumia matangazo yake katika vyombo vya habari, kueneza chuki miongoni mwa watoto na vijana nchini. Matangazo ya HakiElimu ambayo yaliiudhi serikali ni pamoja na lile serikali kueleza kuwa uchumi unapanda wakati hali ya wananchi bado duni. Jingine ni lile lililoonyesha matatizo sugu ya walimu wanaofanyia kazi maeneo ya vijijini.

  Tangazo hilo lilimuonyesha mwalimu akitumia siku mbili kufuata mshahara mjini. Akitumia baskeli lakini anapofika benki anakuta mshahara bado haujaingizwa.

  Waziri Sitta ambaye alikuwa Spika katika Bunge la Tisa, alisema kila mtu anatambua mchango na umuhimu wa HakiElimu tangu kuanzishwa kwake mwaka 2001, hivyo hakuna haja ya shirika hilo kuogopa kusema ukweli katika harakati za kuboresha elimu nchini.“Ukweli ni kwamba katika nchi zilizoridhia makubaliano ya Dira ya Elimu ya mwaka 2015 na katika Jumuiya ya Afrika Mashariki tuna nchi tano, lakini Tanzania ni ya mwisho kielimu. Hali hii inatishia uhai wa nchi,” alisema Sitta.Alisema kuwa elimu bora inaweza kumbadili mtu kitabia na kiuchumi na hivyo kumfanya ajiamini.

  Hata hivyo, Waziri Sitta alisema tofauti na ukweli huo, sasa umaskini hasa kwa watu wa hali ya chini nchini, unazidi kuongezeka huku baadhi ya viongozi wasiokuwa na maadili wakiendelea kulipeleka taifa kusikokuwa na mwelekeo.

  Waziri Sitta alifafanua kuwa mtu hapimwi kwa ufaulu wa mitihani na shahada alizonazo, bali anapimwa kutokana na utendaji wake na maadili mema kazini na kuwa mstari wa mbele katika kulinda maslahi ya taifa.“Kiongozi hapimwi kwa shahada, vyeti wala kiwango cha ufaulu wa mitihani yake, maana Tanzania ina viongozi wengi wenye shahada na vyeti kibao, lakini wanayofanya viongozi hao wenye shahada, wote tunayajua,” alisema.

  ...SITTA AMESHIKA NYADHIFA NYINGI SANA KATIKA SERIKALI YA TANZANIA YOTE HAYO HAYAKUYAONA AU NDO ANAWANIA 2015 URAIS
  TAFAKARI
   
 12. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  hayo mambo ya 2015,hivi hawa wazee wataachia lini ngazi?Wametuharibia nchi kwa muda mrefu sasa.Mfumo wetu wa elimu ni mbovu,na rushwa huchangiwa sana na umasikini sio ubovu wa elimu,watu wengi walio madarakani ni product of colonial education system.....
   
Loading...