Waziri Prof. Makame Mnyaa Mbawara adhihirisha serikali kutojali Utafiti/watafiti

Lyimo

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,826
2,017
Inasikitisha kusikia kauli ya Waziri mwenye dhamana katika mawasiliano, Sayansi na technologia, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa kueleza kuwa Tanzania haina watafiti wenye sifa. Taarifa hii aliitoa kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya chuo kikuu cha Dar es salaam (Source: Mwananchi ya leo). Kutokana na kauli yake anataka wafanyakazi wote kwenye taasisi zinazoendesha utafiti wawe wenye shahada ya juu ya uzamivu (PhD), kitu ambacho si kweli. Inaelekea hata yeye licha ya kuwa Professor hajui utaratibu wa jinsi tafiti zinavyoendeshwa. Hajathamini taaluma zingine kama Shahada za uzamili (Masters), Shahada ya kwanza (Bachelor), Stashahada (Diploma) naAstashahada (Certificate/Cheti), ambao wote wanashughuli muhimu katika kufanikisha shughuli nzima ya utafiti. Pia kuna wengine hujifunza kuendesha mitambo tu ama kazi za maabara (technicians) ambao hawahitaji kufikia ngazi ya shahada ya Uzamivu. Kwa ujumla mtu mmoja/wachache wenye PhD wanaweza saidiwa na kada zote hizi kulingana na aina ya tafiti iliyopangwa.

Ni ukweli ulio wazi serikali yetu haithamini mambo ya tafiti, kwanza inatoa pesa ndogo sana (Chini ya asilimia 1) katika taasisi zake ikiwemo vyuo vikuu. Huwezi amini watafiti wengi wanategemea waandike mapendekezo (proposals) kwa wafadhili wan je ambao mara nyingi inabidi kufuata matakwa yao, hivyo matatizo ya Tanzania yanakuwa hayawakilishwi kwa kiwango stahili. Vilevile tatizo linguine kubwa la serikali yetu, ni kutofanyia kazi matokeo/mapendekezo yanayotokana na tafiti zetu. Hivyo kuna taarifa nyingi za tafiti zimebaki kwenye makabati na hata kupoteza uhalisia wake kutokana na muda kupita. Kama serikali ingekuwa na nia ya dhati ya kuwatumia watafiti waliopo, ingepiga hatua kubwa katika kutatua matatizo mbalimbali. Tumeshuhudia watafiti wengi kwenye vituo vya tafiti (tena hao wenye PhD) kutokuwa na kazi kutokana na kutokuwepo kwa nyenzo/vitendea kazi na/ama kutotengwa fungu la kuendesha shughuli hizi muhimu.

Ni wakati muafaka sasa, serikali ijifunze kuwatumia wataalamu wetu kwa uchache wao ili kuleta tija kwa Taifa. Inasikitisha kutokana nakutokuwa na mazingira mazuri ya kuwatumia wataalamu wetu, hivyo inawafanya wengi kufanya tafiti zenye matakwa ya wafadhili, kukimbia nchi na kwenda kuutumia utaalamu wao nje ama kukimbilia kwenye siasa kama tunavyoshuhudia hivi sasa. Vilevile nchi yetu haina mahusiano ya moja kwa moja kati ya taasisi za utafiti, Viwanda, Vyuo vikuu, wadau (wakulima, wafanyabiashara nk) kwa kujumla wake katika kutekeleza shughuli nzima za tafiti kama wanavyo fanya nchi za wenzetu wanaoweza kutumia tafiti kama njenzo muhimu katika kutatua matatizo mbalimbali kwenye sekta mbalimbali. Hivyo serikali isikimbilie kusema tanzania haina watafiti wenye sifa wakati haina mikakati yoyote ya kuwatumia vizuri hawa walipo.
 
kwa serikali ya CCM, mambo ya utafiti siyo priority. inajulikana kimataifa kwamba bila kuwekeza katika R&D, haiwezekani kufanya jambo lolote la maana la maendeleo katika nchi yoyote. tatizo linakuja kwamba kwa serikali inayojali zaidi matanuzi, inabidi iwekeze zaidi katika kuhonga wale wanaoweza kuibana: Wabunge - ili iweze kuendeleza matanuzi. huu sasa ni ugonjwa na dawa pekee ni watanzania wenyewe tujizatiti kupinga hayo kwa nguvu zote
 
Tanzania kinachoheshimiwa ni siasa na wanasiasa, sio taaluma na wanataaluma. Hata ukiwa profesa mwenye taaluma ya kuokoa miasha ya watu, huna maana kuliko mbunge ambaye mwenye elimu ya msingi. Kama mtafiti hathaminiwi usitegemee hata siku moja kama utafiti utathaminiwa, vitatafutwa visingizio vingi sana kupiga blaa blaa....
 
Nafikiri yeye ali..focus zaidi kwenye ubora wa tafiti!!
Ndugu, hata mie nimekuwa nikifikiri hivyo kwa muda mrefu. Ukweli ni kwamba TZ tuna watafiti wazuri sana tena world class hata kwenye field ambazo kama taifa tuko nyuma kama ICT. Tatizo kwanza tafiti zao hazifanyiwi kazi (kwa maana ya kutengeneza tools/devices-kwa upande wa ICT) na serikali, Serikali inatenga fungu dogo sana kwa ajili ya utafiti(it has always been less than 1% of total budget)-research project nyingi zinafadhiliwa na mataifa ya nje na maslahi duni kwa watafiti na ndio maana wengi wanakimbilia nje.
Unajua hapa bongo kuna researcher ambaye alikuwa anatumiwa na NASA (USA) mara kwa mara? Kuna wengine wengi, labda si busara kuwataja hapa, lakini kiujumla tunajitahidi pamoja na matatizo yaliyopo.
 
Back
Top Bottom