Waziri Nundu aipiga ‘stop’ Majembe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Nundu aipiga ‘stop’ Majembe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Dec 25, 2010.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,261
  Likes Received: 19,389
  Trophy Points: 280
  Waziri Nundu aipiga ‘stop’ Majembe Send to a friend Friday, 24 December 2010 20:40 0diggsdigg

  [​IMG]Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu.

  Fidelis Butahe na Zulfa Msuya
  WAZIRI wa Uchukuzi, Omari Nundu ameitaka Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), kusitisha mkataba wake na Kampuni ya udalali ya Majembe ifikapo Desemba 31 mwaka huu. Taarifa hiyo itakuwa ya furaha kwa madereva wa mabasi yafanyayo safari zake ndani ya miji na yale yaendayo mikoani baada ya kupambana na maofisa wa Majembe kwa muda mrefu, wakilipishwa faini kubwa, kuwekwa mahabusu na kuzuiwa kufanya shughuli zao kwa muda mrefu na hivyo kupunguza "hesabu".

  Wamiliki na madereva wa mabasi walipinga mara kadhaa uamuzi wa Sumatra kuitumia kampuni hiyo na wakati mwingine kuendesha migomo ya kutoa huduma za usafiri, wakidai kuwa maofisa wa kampuni hiyo ya udalali hawaelewi vizuri masharti ya leseni za usafirishaji. Walidai kuwa maofisa hao wa Majembe waliwalipisha hadi faini ya Sh250,000 kwa madai ya kufanya makosa ya kukiuka masharti ya leseni, na kushauri polisi ndio waendelee na jukumu lao la kawaida la kusimamia sheria hizo.

  Kilio chao kilimfikia waziri ambaye pia ameagiza kuwa wapigadebe waondoke katika vituo vyote vya mabasi nchini, huku akizitaka mamlaka husika kabla ya Januari 15 ziwe zimeandaa utaratibu wa kuwatambua wafanyakazi na wakala wa makampuni ya mabasi. Kutokana na tamko hilo kuanzia Januari Mosi mwakani Majembe, ambayo imekuwa ikitumiwa na taasisi nyingi za serikali, haitajihusisha tena na kazi hiyo na badala yake Sumatra imetakiwa kuandaa wafanyakazi kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.
  Waziri Nundu aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuwa “haiwezekani kila kazi ifanywe na Majembe tu... tulikaa na Chama cha Wamiliki wa Mabasi (Taboa), pamoja na Chama cha Wamiliki wa Daladala (Darcoboa) na walitoa mapendekezo yao na haya ndiyo majibu yake”.

  Alisema: “Kutokana na utata uliojitokeza katika ukaguzi wa madaraja ya mabasi kwa kutumia Majembe, niliagiza Sumatra kusimamia wenyewe zoezi hilo na walishaanza tangu Desemba 9 mwaka huu. Kwa hiyo kuanzia Desemba 9 Majembe hawasimamii tena ukaguzi wa madaraja ya mabasi.” Akionekana kukerwa na jinsi Majembe inavyopewa zabuni na taasisi tofauti, Waziri Nundu alisema: “Kuhamisha watu katika nyumba, Majembe; udalali wa magari, Majembe; kila kitu Majembe. Kampuni hii ina kazi zake bwana, sasa katika hili Sumatra na Jeshi la Polisi ndio watakaohusika na utekelezaji,” alisema Nundu.

  Kuhusu wapiga debe ambao wanalamikiwa kuwa wanapewa vitambulisho na baadhi ya mawakala na kushirikishwa kwenye vikao vya maamuzi huku wenye mabasi wakitengwa, Nundu alisema serikali imeagiza kwamba waondoke katika vituo vyote vya mabasi nchini mara moja.
  Alisema kuwa mamlaka zinazohusika ziandae utaratibu wa kuwatambua wafanyakazi na wakala wa makampuni ya mabasi ikiwa ni pamoja na kuwatafutia vitambulisho maalum. “Najua kwamba hili suala la wapigadebe limekuwa kero ya muda mrefu, kuanzia sasa waanze kutafuta njia mbadala ya kujipatia kipato, wakiamua kuchakalika watakuwa matajiri wakubwa, lakini kwa sasa hamna ruhusa tena.

  Mpiga debe anafikia hatua ya kumpiga ‘kabari’ dereva wa basi, hii ni sawa kweli,” alihoji Nundu. Akizungumzia suala la nauli za mabasi Nundu aliagiza zoezi la kupitia nauli ambalo linasimamiwa na Sumatra, lifanyike haraka iwezekanavyo na likamilike ifikapo Januari 31 mwakani na kuiagiza Sumatra ikutane na wamiliki wa mabasi kujadili maombi yao kabla ya kufanya kikao cha wadau wote wa usafiri nchini.
  “Kuna suala la vikao vya wadau wa Sumatra kuwa na wajumbe ambao si wasafirishaji na wasioelewa usafirishaji; mpango wa sasa wa kuwahusisha watoa huduma za usafiri na walaji uendelee. Hata hivyo Sumatra wakutane na wamiliki kwanza kujadili kero zao kabla ya kukutana na wadau wote,” alisema Nundu.

  Alisema kwamba licha ya baadhi ya mabasi kugundulika kuzidisha uzito ni muhimu zoezi la upimaji mabasi liendelee ili kukidhi matakwa ya sheria ya usalama barabarani pamoja na kulinda miundombinu ya usafiri. Kuhusu matuta, Waziri Nundu alisema: “Matuta barabarani yamekuwa kero na ni chanzo kingine cha ajali, lakini bado kuna umuhimu kuwa na matuta ya barabarani kama njia ya kuhakikisha kuwa madereva wanapunguza mwendo kasi.
  "Wizara ya Uchukuzi kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi tutachukua hatua muafaka ili kuhakikisha ujenzi wa matuta haya unafuata viwango,” alisema Nundu. Kuhusu mapendekezo ya Taboa kwamba bidhaa za mabasi ya abiria zinazoingizwa nchini zisamehewe kodi, Nundu alisema kuwa pamoja na kuwa misamaha ya kodi ni kivutio cha uwekezaji, lakini inaathiri mapato ya serikali hivyo serikali italiangalia suala hilo ili kuhakikisha haliathiri mapato yake.

  Pia alizungumzia mapendekezo ya Darcoboa kuhusu nauli ndogo ikilinganzishwa na gharama kubwa za uendeshaji na akasema wameagiza kuitishwa kwa mkutano wa wadau na marekebisho ya bei yawe yamekamilika nchi nzima ifikapo Januari 31 mwakani. “Walilalamikia pia suala la kutozwa faini kubwa kuliko makosa wanayofanya, hivyo Wizara kwa kushirikiana na Sumatra, wadau na mwanasheria mkuu kupitia upya adhabu hizo kabla ya Juni 2011,” alisema Nundu.
   
 2. smati

  smati Senior Member

  #2
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Who are majembes.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,261
  Likes Received: 19,389
  Trophy Points: 280
  Kuhamisha watu katika nyumba, Majembe; udalali wa magari, Majembe; kila kitu Majembe
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  ...and who is behind Majembe?
   
Loading...