Zurii Member Mar 6, 2012 64 24 Apr 4, 2012 #1 Waziri Ngeleja akisakata rhumba kwa kukata kiuno. Mbunge wa Afrika Mashariki, Dk. Amani Walid Kabouru (kushoto) na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Joyce Masunga wakisakata muziki. Akihutubia wananchi kwenye kampeni hiyo. WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja, mwishoni mwa wiki iliyopita alijikuta akitoa shoo ya bure baada ya kupanda jukwaani, kisha kusakata muziki. Waliompa sapoti ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Dk. Amani Walid Kabouru na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Joyce Masunga ambao nao waliserebuka stejini. Ngeleja alifanya hivyo katika eneo la Mwembe Sangara, Kirumba,wakati wa kuhitimisha kampeni za kumnadi aliyekuwa mgombea udiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Kirumba Jijini Mwanza, Jackson Robert Masamaki mgombea ambaye alibwangwa na Bahati Kahungu aliyekuwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita. Kana kwamba yupo kwenye steji ya bendi ya Twanga Pepeta, Ngeleja aliendelea kunogesha kampeni hizo kwa takribani dakika 10 akisakata rhumba na kuwaacha hoi wananchi, kabla ya kuhutubia kuomba kura kisha akamaliza kwa staili ile ile aliyopandia jukwaani kwa kucheza muziki. HABARI/PICHA: MASHAKA BALTAZAR, MWANZA
Waziri Ngeleja akisakata rhumba kwa kukata kiuno. Mbunge wa Afrika Mashariki, Dk. Amani Walid Kabouru (kushoto) na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Joyce Masunga wakisakata muziki. Akihutubia wananchi kwenye kampeni hiyo. WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja, mwishoni mwa wiki iliyopita alijikuta akitoa shoo ya bure baada ya kupanda jukwaani, kisha kusakata muziki. Waliompa sapoti ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Dk. Amani Walid Kabouru na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Joyce Masunga ambao nao waliserebuka stejini. Ngeleja alifanya hivyo katika eneo la Mwembe Sangara, Kirumba,wakati wa kuhitimisha kampeni za kumnadi aliyekuwa mgombea udiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Kirumba Jijini Mwanza, Jackson Robert Masamaki mgombea ambaye alibwangwa na Bahati Kahungu aliyekuwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita. Kana kwamba yupo kwenye steji ya bendi ya Twanga Pepeta, Ngeleja aliendelea kunogesha kampeni hizo kwa takribani dakika 10 akisakata rhumba na kuwaacha hoi wananchi, kabla ya kuhutubia kuomba kura kisha akamaliza kwa staili ile ile aliyopandia jukwaani kwa kucheza muziki. HABARI/PICHA: MASHAKA BALTAZAR, MWANZA
Kongosho JF-Expert Member Mar 21, 2011 35,999 24,175 Apr 4, 2012 #3 duh, mbaba ana uno huyu, lol, utadhani kalikonekti gridi ya taifa.
Safety last JF-Expert Member Mar 24, 2011 4,227 1,389 Apr 4, 2012 #4 Kweli ccm sera zimeisha ....,sasa huyo mzee wa megawati amegeuka ngwasuma
M Mkandara JF-Expert Member Mar 3, 2006 15,772 8,958 Apr 4, 2012 #5 Safety last said: Kweli ccm sera zimeisha ....,sasa huyo mzee wa megawati amegeuka ngwasuma Click to expand... Dahh nimecheka hadi nashindw akuandika.. Toka sasa Ngeleja atajulikana kwa jina la - mzee wa Megawati, ngwasuma..
Safety last said: Kweli ccm sera zimeisha ....,sasa huyo mzee wa megawati amegeuka ngwasuma Click to expand... Dahh nimecheka hadi nashindw akuandika.. Toka sasa Ngeleja atajulikana kwa jina la - mzee wa Megawati, ngwasuma..
BADILI TABIA JF-Expert Member Jun 13, 2011 32,772 23,163 Apr 4, 2012 #6 nilijua nitakuta video anasakata. Kumbe mi still picture, sijaona kiuno hapo....
Anko Sam JF-Expert Member Jun 30, 2010 3,200 820 Apr 4, 2012 #7 Safety last said: Kweli ccm sera zimeisha ....,sasa huyo mzee wa megawati amegeuka ngwasuma Click to expand... Ameshindwa kumwaga Megawati wakati huu wa mgao amekalia kunengua jukwaani! kweli wameishiwa sera!
Safety last said: Kweli ccm sera zimeisha ....,sasa huyo mzee wa megawati amegeuka ngwasuma Click to expand... Ameshindwa kumwaga Megawati wakati huu wa mgao amekalia kunengua jukwaani! kweli wameishiwa sera!
MAMA POROJO JF-Expert Member Nov 22, 2007 4,974 785 Apr 4, 2012 #8 wajukuu wa cameron viuno vinawapa tabu sana mkiona tu mnatoa tafasiri za uingereza hapo ni mwanza jamani
wajukuu wa cameron viuno vinawapa tabu sana mkiona tu mnatoa tafasiri za uingereza hapo ni mwanza jamani
Daudi Mchambuzi JF-Expert Member Nov 25, 2010 62,204 128,022 Apr 4, 2012 #9 kata mauno bila sera wala hoja za msingi alafu angukia pua.
toghocho JF-Expert Member Mar 16, 2011 1,172 198 Apr 4, 2012 #10 viuno mauno, anafanya nini pale wizarani, si aende akudo?
T TKO Member May 14, 2010 18 3 Apr 4, 2012 #11 Labda akiendele kukizungusha kiuno sana ataweza ku produce megawati 1...... Atakua ametusaidia sana.
The Boss JF-Expert Member Aug 18, 2009 49,111 115,905 Apr 4, 2012 #12 labda wanajiandaa na life after 2015.. wanajifunza new skills....lol
K kikura Member Apr 4, 2012 13 3 Apr 5, 2012 #13 Daudi mchambuzi said: kata mauno bila sera wala hoja za msingi alafu angukia pua. Click to expand... nimeshangaa amekua kama sharobaro flani waziri mima kitumbo nje
Daudi mchambuzi said: kata mauno bila sera wala hoja za msingi alafu angukia pua. Click to expand... nimeshangaa amekua kama sharobaro flani waziri mima kitumbo nje
Mamndenyi JF-Expert Member Apr 11, 2011 40,607 52,336 Apr 5, 2012 #14 nazidi kuamini kuwa ccm ina vichaa wengi.