Mhe Dr. Joyce Ndalichako heshima kwako na pole na majukumu ya kila siku.
Mhe waziri napenda kutumia jukwaa hili kuwasilisha malalamiko na kilio cha wanafunzi wengi wanaosoma Taasisi ya elimu ya watu wazima( Institute of Adult Education) iliyopo maeneo ya maktaba, Upanga.
Mhe waziri siku za hivi karibuni watendaji wa Taasisi hii wameibua mtindo wa kudai rushwa ya ngono/fedha kwa kutumia loophole ya kuzuia ama kukosea kwa makusudi majumuisho ya matokeo ya wanafunzi. Mchezo huu mchafu unaratibiwa na Mtendaji wa examination room ambaye jukumu lake kubwa ni kucompile matokeo ya wanafunzi na kuyatoa kwa wakati kwa wanafunzi. Ndugu huyu ambaye jina lake linaanzia na herufi N amekuwa akifanya huu mchezo kwa kukosea makusudi na kuanza kusumbua wanafunzi.
Ajabu zaidi ni kwamba hata Mkuu wa mafunzo wa Taasisi bwana M na Registrer bwana B pia wamekuwa hawana huwezo wa kuchukua hatua yoyote dhidi ya bwana N N pindi wanapoletewa kesi za figisu figisu za matokeo zinazofanywa na bwana N. Victim wa hizi hila za bwana N wengi wao wamekuwa ni wasichana wadogo kwa kuwa ni kundi ambalo yeye kwa mawazo yake anahisi ni rahisi kulirubuni kupitia mbinu zake hizi chafu.
Mhe waziri kwa niaba ya wanafunzi wa Taasisi ya elimu ya watu wazima tunakuomba uanzishe uchunguzi mara moja ikiwezekana pia uhoji hata wanafunzi ambao wameadhirika na uchafu wa huyu bwana N.
Ahsante