WABHEJASANA
JF-Expert Member
- Jun 22, 2011
- 4,225
- 869
Habari wakuu?!
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya nchi Emmanuel Nchimbi amesema Damu ya Mchungaji Mathayo Kachira aliyeuawa katika mapigano kati ya Wakristo na Waislamu yaliyotokea Jumatatu wiki hii katika Mji Mdogo wa Katoro wilayani Chato Mkoani Geita,itumike kuleta Amani juu ya mgogoro wa Uchinjaji.
Nchimbi ametoa kauli hiyo muda mfupi uliopita wakati wa mazishi ya mchungaji huyo ambayo yamefanyika nyumbani kwake Buselesele,na kuhudhuriwa na mamia ya watu ambao ni waumini wa madhehebu ya kikristo.
Amewataka wachungaji na maaskofu kuhubiri Amani,na kuwakemea wachungaji wote ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuchochea mgogoro wa nani mwenye mamlaka ya kuchinja kati ya Waislamu na wakristo ambao uliibuka hivi karibuni,huku akisema kwamba serikali itaendelea kusimamia amani ili kuepusha nchi kuingia kwenye vurugu.
Hata hivyo mmoja wa wachungaji waliokuwa wakishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Mchungaji Mathayo,akihubiri wakati wa kuuaga mwili wa marehemu(Mchungaji),alisisitiza kwamba wakristo wataendelea kuchinja nyama kwa ajili ya mahitaji yao,na kwa kuanza wanaanza leo kwenye msiba huo.
Kuachiwa kwa mchungaji huyo Isaya Ikiri wa kanisa la TAG na mwenzake Daud Merdad wa kanisa la PAG kulikuja kufuatia barua iliyoandikwa na umoja wa makanisa ya Kikristo tarehe 11 mwezi huu kwenda kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Paul Leonard wakimtaka kuwaachia wachungaji hao mara moja kwa vile hawahusiki katika tukio hilo.waliachiwa jana jioni.
Katika Tamko la umoja wa madhehebu ya Kikristo iliyosomwa mbele ya Waziri Nchini na umati wa watu waliokuwa wamehudhuria mazishi ya Mchungaji huyo,wamewataja kwa majina watu wawili waliohusika na kumchinja mchungaji Kachira na kuimba serikali kuwakamata mara moja.
Katika hali ya kungaza hakukuweo na kiongozi yeyote wa Kiislamu aliyekuwepo kwenye mazishi hayo,na habari za kina zinaeleza kwamba hata waumini wa kiislamu hawakuweza kuhudhuria mazishi hayo hata wale majirani zake na marehemu.