Waziri Nchemba afuta utaratibu wa wakimbizi toka nchi jirani kuingia nchini

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,621
8,411
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amefuta utaratibu wa wakimbizi toka nchi jirani kuingia nchini. Ilikuwepo ruhusa ya watu kuingia nchini wakiwa katika kundi lakini sasa itabidi wapitie ukaguzi na wakubalike kuwa wakimbizi kweli ndio waruhusiwe kuingia nchini.

Kuna watu waliruhusiwa kuingia kutokana na kuwepo kwa tension ya kisiasa katika nchi zao lakini sasa tension hakuna tena na kuna watu wanaingia kwa kigezo cha kuwa ni wakimbizi kumbe wamekimbia njaa katika nchi zao.


 
Warundi inawahusu sana hii!!! Wanaingia wengi kweli kupitia mpaka wa Kabanga. Juzi jamaa angu alikutana na basi km saba hivi zimewabeba toka kambi ndogo ya Rukole, Ngara wakipelekwa kambi kubwa huko Kigoma
 
Na huo ndio utaratibu wa kimataifa... hata ivyo nchi huwa inamamlaka ya kuamua kwanza kama kuwapa ruhusa ya kuingia ama lah... Mashirika kama Unhcr yapo kusaidia na kuangalia haki zao kama zinafuatwa lakini pia kuwasaidia katika mambo ya haki zao makazi vyakula nk.
 
Back
Top Bottom