Lanlady
JF-Expert Member
- Feb 27, 2019
- 1,916
- 6,526
Hebu fikiria mtu unaongeza salio unakatwa sh 100 au zaidi, ambayo kiuhalisia hakuna huduma uliyojiunga.
Mbaya zaidi ukipiga simu ya huduma kwa wateja haipokelewi na endapo ikipokelewa unaambiwa kuna huduma umejiunga.
Ni huduma gani hizi ambazo mtu anajiunga bila kujua?
Na wala hajawahi hata kujiunga!
Na maelezo ya kujitoa, unapewa namba amabayo nayo unakatwa zaidi ya sh 100.
Wakifanya hivi kwa wateja elfu 10 kwa siku si tayari wana hela ya chai? Huu ni wizi!
Baadhi ya wateja tuna hali mbaya kiuchumi, hiyo sh 100 ni kubwa sana.
Tafadhali, tunaomba mitandao ya simu, hasa HALOTEL, waache wizi!