G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,591
- 36,004
Nimesikitika baada ya kubaini kuwa swala la kutokurusha bunge 'live' lilikuwa ni wazo binafsi la waziri Nape Nnauye mbele ya viongozi na wabunge wa CCM kwa madai kuwa kuonyeshwa kwa bunge 'live' kumekuwa kukiigharimu CCM nakuifanya ichukiwe mbele ya watanzania.
Nape Nnauye baadaye alienda bungeni na kutoa sababu zisizo na mashiko eti kuonyesha bunge 'live' kunaigharimu serikali mabilioni huku kukiwa na kauli mbiu ya kubana matumizi kusiko na tija!
Hivi TBC1 kuonyesha mi-documentary isiyo na kichwa wala miguu ni bora kuliko kuonyesha bunge live? Muda ambao TBC1haionyeshi bunge imekuwa inaonyesha vipindi vya ajabu ajabu visivyo na maana yoyote kwa jamii ambayo ndiyo inawalipa mishahara hawa watu! Hiki ni kituo cha watanzania na wanatakiwa kutoa ushirikiano kwa watanzania! Siyo kituo binafsi cha Nape Nnauye
Sasa Nape Nnauye atueleze anapoonyesha 'live' hotuba za rais Magufuli TBC1 wanalipwa na nani? Hoja ya kubana matumizi kwa TBC1 imefafanuliwa vipi?
Kama hoja ni kubana matumizi basi kuliko kuonyesha vitu visivyo na faida yoyote kwa jamii bora wangezima mitambo wasiwe hewani muda huo!
Kama kituo cha TBC1 hakiwezi kuwa na ushirikiano na watanzania kwa shinikizo la Nape Nnauye basi hakuna sababu ya kuwalipa kodi zetu wakala mishahara! Wajiendeshe kibiashara ili wajilipe mishahara kutokana na biashara zao! Pia hatuoni faida ya Nape Nnauye kama waziri kwa jamii maana hana kazi na jamii! Hatuwezi kuwalipa watu ambao hawapo kwa ajili ya watanzania!
Kwa staili hii watu wasipolipa kodi kwa moyo mmoja wataulizwa??