Nyakarungu
JF-Expert Member
- May 1, 2011
- 472
- 377
Dr Hamis Kigwangala na Katibu Mkuu Wizara ya Afya mna maslahi gani na jipu la NTLP lina usaha limeichafua Nchi na nyie mjiandae kuumeza usaha wake au kuutapika.
Nianze maandiko haya kwa kutoa tahadhari, jipu linaloonyesha dalili za kupasuka na likakosa kitu chenye ncha kali kulipasua, ipo siku litakuadhiri mbele za watu, kwani hata nguo yako tu uliyovaa ikiligusa litatumbuka na kukuchafua hadharani.
Leo naleta kwenu jipu hili lililolimbikiza bacteria (Abscessical Bacteria) kwa muda mrefu na kwa kuwa alikosekana mtumbuaji mwenye tahadhari leo linatumbuka hadharani kwa kuguswa na mate yake mwenyewe kwa sababu liko kwenye ulimi kabisa, hivyo usaha utamwagika na sijui kama mwenye jipu ataumeza ili kuficha aibu ili ahuharishe baadae kimyakimya au atautapika hadharani tumshangae.
Kwa ufupi mimi ni mpelelezi wa kujitolea naifanya kazi hii katika idara yeyote bila kujali lolote zaidi ya kutaka usafi katika idara za huduma kwa jamii, naitwa ‘NYUNDO YA CHUMA’
Mradi wa kifua kikuu na ukoma wenye tawi tanzu la kifua kikuu na ukimwi umekuwa ukifadhiliwa na watu wa marekani CDC kwa miaka kadhaa, CDC wamekuwa wakitoa pesa kwa ajili ya utafiti, mafunzo, tiba na vitendea kazi vingine, ili kuimarisha afya ya jamii, hasa kwenye upande wa kutokomeza kifua kikuu na ukoma, zoezi ambalo limefanikiwa sana ukanda wa kusini mwa jangwa la sahara.
CDC ndio mzazi na mlezi wa watu walioathirika kwa kifua kikuu na ukimwi, bila CDC huduma kwa watu hawa zingekuwa duni na zaidi sana tungewapoteza watu wengi sana kwa kukosa pesa za kuendeshea mafunzo na kupata vitendea kazi vya kutolea huduma na dawa.
CDC hutoa pesa kwa taasisi na nchi ambayo inatekeleza sawa na malengo, ikiwa tutakeleza ipasavyo ufadhili wao utaendelea kwa kiwango cha juu zaidi, na endapo tutaonekana kuyumba na matumizi yasiyoeleweka ufadhili utayumba pia.
Mpaka sasa Tanzania ikiwa na Mradi huu wa National Tb and Leprosy Program (NTLP) unaosimamiwa na wizara ya afya tumeshafeli na kushusha thamani ya umahili na elimu za watendaji wetu na taifa kwa ujumla, lakini pia uaminifu kwa wafadhili tumeupoteza kwa sababu mwaka jana NTLP ilipewa dola za kimarekani million 2, lakini tumeporomoka mpaka kupewa dolla za kimarekani 750,000/- na pengine hili jipu tunatakiwa tulitumbue likiwa mdomoni mwa aliyelilea na kumlazimisha ameze usaha wake ili akaharishe kimya kimya chooni kwake kuepusha kipindupindu mitaani.
Chanzo cha kuporomoka kwa kiasi hicho ni mtu mmoja tu anaitwa Beatrice Mtayoba ambaye ndiye mratibu wa mradi huu kitaifa, huyu mama ndiye chanzo cha matatizo yote katika mradi huu, anaitumia ofsi kwa manufaa yake binafsi kwa mfano;-
Amefanikiwa kuwakatisha tamaa watumishi wengine tamaa kwa kubuni njia mbalimbali za namna ya kuiba fedha za wafadhili kwa kuibua vimiradi vya hovyohovyo ambavyo anakuwa anashindwa kuvitolea maelezo
Kwa hali hiyo baadhi ya watumishi walianza kugomea mipango yake, lakini mwenzao kwa ufundi wake wa kiasili aliweza kuwahujumu mpaka wengine wakaacha kazi wenyewe na kutafuta maeneo mengine
Uwezo wake kiutendaji ni mbovu sana lakini alifanikiwa kumshika mwanasheria wa wizara ya afya Patricia Maganga akawa ndiye mshauri wake mkuu na kumzunguka katibu mkuu wa wizara,
Alifanikiwa kuwahujumu baadhi ya viongozi wenzake waliokuwa wakifanya mambo yaende kama yalivyopangwa, mfano alimhujumu Dr Nyamkala aliyekuwa mratibu wa kifua kikuu na ukimwi kwa kuzuia miradi iliyokuwa imeelekezwa na wafadhili kwa mwaka mzima akiwa anaikwamisha, huku akishirikiana na mwanasheria wa wizara ya afya Ndugu Patricia Maganga ambae amekuwa akishirikiana nae kwa kila mbinu chafu dhidi ya watumishi wenzake kwa sababu wana mahusiano yao ya siri kwa maana ya kunufaika na pesa hizi za miradi kwa sababu ili katibu mkuu wa wizara atie saini pesa za miradi zikachukuliwe ni lazima mwanasheria wa wizara ahusike, hivyo Bi. Betrice amekuwa akimtumia vilivyo na mambo yao yamenyooka huku wakiumiza wananchi waliotegemea kupata huduma safi na zenye weledi, hivi sasa takwimu za watu wanaoumia kwa kifua kikuu ni wengi kulinganisha na kipindi cha nyuma.
Lakini Bi. Beatrice ili afanikiwe kuwa salama na acheze michezo yake vizuri alimuondoa mwajiriwa wa mradi ambaye alikuwa Mratibu wa mradi wa kifua kikuu na ukimwi na kumzunguka kwa mgongo wa nyuma kupitia mwanasheria mkuu wa wizara wakafanikiwa kumwajiri kwenye nafasi hiyo mdogo wake wa kinasaba Dr. Wenzekoyi ambaye mpaka sasa cv yake ina utata hana uwezo kabisa wa kusimamia mradi huu, nay eye ni sababu namba mbili ya kupunguziwa ufadhili kwa sababu takwimu za mradi zimeshuka kabisa hana ubunifu, hafanyi kazi za maana zaidi ya kufanya kazi ya kutafuta wataalamu wa kuandika proposal ya namna ya kuchota pesa za mradi, ameanza kazi miezi kadhaa iliyopita lakini sasa ana gari V.8 hata kwa akili ya kawaida tu haingii akilini.
Hata mshahara anaolipwa ni aibu tupu na ni usaha tele, kwa mfano ukilinganisha na Nyamkala aliyefanya kazi miaka 9 alianza na mshahara wa 2mil kwa mwezi akafikia kiwango cha kulipwa 4.8mil kwa mwezi (hii ni performance based), lakini kwa huyu kibaraka wa Bi.Beatrice inashangaza kumuona ameanza tu na kiwango cha 4.8mil akiwa na miezi 2 tu kwenye mradi bila hata kuona performance.
Ilipoulizwa Bi. Beatrice aligeuka mbongo kiasi kwamba huyu kibaraka wake analipwa na allowance ya ziada 2mil ukijumlisha na mshahara wake 4.8+2=6.8mil ni aibu sana hii. Hili lilisimamiwa na mwanasheria mkuu wa wizara ya afya Maganga.
Bi. Beatrice ni fundi wa fitina alianikiwa kuwapa stress watumishi kadhaa akiwemo aliyekuwa Ass. Accountant Bwana Kidawa na aliyekuwa mtaalamu wa physiotherapy Doris waliamua kuacha kazi kwa hiari zao kwa kuona uozo huu uliokuwa unadhalilisha taaluma zao.
Lakini pia Bi. Beatrice ana akiba ya mtu anayeitwa Basila Dolla mwenye asili ya Somalia habari nyepesi zinasema kuwa huyu msomali ni Serengeti boy wake, huyu ni mkuu wa kitengo cha maabara na vipimo, huyu ndiye mtaalamu wa kuchonga dili za njia za panya kwa sababu anajua mbinu za kukwepa mitego kwa sababu ana mkono huko juu, na Bi. Bite amekuwa akimtumia kama mkono wake wa kazi.
Mungu apewe shukrani kwa sababu penye uozo bado pana kona yenye unafuu kidogo, ndani ya NTLP bado wapo watumishi wanaoishi kwa uvumilivu sana kiasi kwamba wanatamani mradi huu upinduliwe utawala ubadilike na mateso wanyoyapata waishe,
Bwana Msuya ambaye ni mwasibu mkuu wa mradi amekuwa mwiba kwa Bi. Beatrice na amekuwa akizuia ujinga mwingi ambao huyu mama amekuwa akitaka kuufanya, lakini sasa Bwana Msuya anaelekea kustaafu mwezi wa tano mwaka huu (05/2016) ambapo NTLP inahitaji mwasibu mpya
Bi. Beatrice ameshapanga majeshi yake sawasawa kwa ajili ya kumwajiri ndugu Lutashobya Lucas ambaye kwa sasa anafanya kazi katika taasisi binafsi ili iwe njia yake kukomba mboga zote.
Maswali
Ni usingizi gani katibu wa wizara umelala mpaka uchezewe na mwanasheria wako kiasi hicho?
Ni dharau kiasi gani tunayodharauliwa ikiwa pesa za mradi essential huu wa kifua kikuu na ukimwi tunapata zinaishia midomoni mwa walafi na hatimaye tunawekwa kwenye orodha ya walafi tunaochezea pesa za wangonjwa?
Waziri kesho utajitambulisha mbele ya mataifa kuwa wewe ni waziri wa afya wa Tanzania?
JE, utashangaa ukizomewa, kumbe kosa ni kutoona mambo ya kipumbavu kama haya?
Kwa sasa watu wenye maambukizi ya ukimwi wanaugua kifua kikuu wengi sana kwa sababu huduma kwao imeporomoka kisa ulafi wa Bi. Beatrice na watu wake
Kwa sababu mtu mwenye maambukizi ya ukimwi kinga zake hushuka na tahadhari ya magonjwa nyemelezi isopochukuliwa kifua kikuu huibuka na kumuua mtu.
USHAURI
Waziri Hamisi na katibu mkuu wa wizara ambao wote ni Technical leader (Madaktari) wasimame kidete kutumbua jipu hili na wahakikishe mwasibu mpya anapatikana kwa njia sahihi na vigezo na sio huyu mama kumwajiri mkono mwingine wa kukombea mboga.
Naitwa NYUNDO YA CHUMA NITAENDELEA KUFUNUA KILA IDARA, JIANDAENI WIZARA YA Mifugo mjiandae.