Waziri Mwijage: Uhaba wa Sukari umetushtukiza

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,075
114,591
Mhe.Mwijage waziri wa Viwanda amehojiwa na Radio One Radia asubuhi ya leo, kuhusu uhaba wa sukari unaoendelea nchi nzima.

Akijibu kwa kujiamini anasema Uhaba wa Sukari umewashtukiza.Ukizingatia wao ni wapya na ndio wanajipanga.Pia amekazia kuwa uhaba wa sukari umesababishwa na msimu wa uzalishaji kukoma katika viwanda vya sukari!

Asante Mwijage kwa kuonyesha rangi halisi ya Serikali yenu
 
TARIME tunapata sukari toka kenya,kilo sh.2000/ poleni ambao kilo mnaipata kwa 4000-5000 endelea kuisoma namba.mmeipenda wenyewe.
 
Anashangaa nini wakati boss wake anatoa kauli za kukurupuka za kuzuia vibali za kuagiza sukari nje yeye alikuwa wapi?
 
Mwijage utulie soon utakuwa mzigo sasa hivi! Usijotoe akili na kuropoka! Heri utulie kabisa!! Kwanza ulikuwa wapi wewe kama waziri mwenye dhamana kazi zako zikawa zinafanywa na DC na RC pamoja na Rais?

Wewe ndio wa kumshauri Rais asikurupuke, kosa lako hili kukubali vibali kuzuiwa wakati hatujajipanga!!! Hatujakuona unaamka sasa kumekucha?
 
Serikali iliahidi sana kwamba haitatuangusha ila kwa hili la sukuari nadhani imeanza kutuangusha huku nilipo hata uwe na elfu 10 hakuna pakuipata hiyo sukari.
 
Kwani ni nani aliyesababisha hii taharuki ya sukari? Waziri aseme ukweli kwani wizarani hakuna makatibu wakuu na washauri wengine?

Ama imefikia kuwa wakuu hawawaamini ushauri wa walio chini yao?
 
Mhe.Mwijage waziri wa Viwanda amehojiwa na Radio One Radia asubuhi ya leo, kuhusu uhaba wa sukari unaoendelea nchi nzima.
Akijibu kwa kujiamini anasema Uhaba wa Sukari umewashtukiza.Ukizingatia wao ni wapya na ndio wanajipanga.Pia amekazia kuwa uhaba wa sukari umesababishwa na msimu wa uzalishaji kukoma katika viwanda vya sukari!!!....Asante Mwijage kwa kuonyesha rangi halisi ya Serikali yenu

Sasa huyu mbona hajatumbuliwa au ni mtu wa karibu sana...
 
Back
Top Bottom