Waziri Mwijage akiri serikali ilikuwa inaficha: Dangote wanataka gesi ya bure, hawatawapa

kamishna wa madin tz bwana kafum kasema, walimuahd kuwa watampa ges, uwanja na makaa ya mawe bure jamaa akakubal akaja kuwekeza, katbu wa nshat na madn kasem dangote anataka makaa ya mawe kwa 4$ na selkar inauza 5.14$ kwa unit 1 ko wakatofautia, wazir anasema jamaa anataka ges bure na ha2wez kumpa bure anunue. watanzania haiitaj PHD kutambua kuwa viongoz we2 hawana utash waku2ongoza. MKEMIA nae ndo anaharb kil cku
 
Waziri wa viwanda na biashara baada ya kudanganya jana kuwa hawana tatizo lolote na Dangote kufuatia kusimamishwa kwa uzalishaji wa saruji leo amegeuka na kukiri walikuwa wanaficha.

Amedai kuwa Dangote anataka apewe gesi ya bure lakini hawatatoa kwa kuwa hiyo itakuwa ni upendeleo na makampuni mengine hayatachezewa fair.

Amesa makampuni yote yanapaswa kutumia makaa ya mawe hapa nchini ili kuwe na usawa kwa kila mtu kwa kuwa soko moja



Ikumbukwe:
Jana mwijage aliongea kwa confidence kabisa kuwa hakuna tatizo kati ya serikali na Dangote na akalaani tabia ya watanzania kuzusha mambo ili kuogopesha wengine


Endeleeni hivo hivo 2020 imekaribia
 
Waziri anakiri kudanganya halafu anaendelea kukalia ofisi ya Uma!?
Hii nchi tunataniana sana, halafu wanalazimisha watu tuwe wazalendo wakati wao ndio mabingwa wa kuua uzalendo.
 
Kama ilikuwa hivyo basi ni kosa. Katika industry moja huwezi kuwa na incentive package tofauti tofauti. Tanzania Portland Cement, Mbeya Portland Cement, Nyati na Camel wapo kwenye cement industry inabidi wapate equal treatment kama Dangote. Itakuwa si busara mmoja apate preferential treament ambayo wengine hawapati. As a country we have to design predetermined incentive packages based on economic sectors and not for individual investors.
kwani hao wengine waliwai kutaka preferential treatment wakanyimwa?
 
Haya makaa ya mawe ni ya nani? Hivi soko huria maana yake nini? Haya makaa nadhani ya mtu fulani ambaye anataka kulazimisha Dangote amnunuze. Ni kama gesi ya Mtwara tu.

Mie sikubali kuwa ati ile ni gesi ni yetu wakati baada ya serikali kufikisha bomba Dar tu, bei ya umeme inapanda. Serikali inaambulia kodi lakini isiseme kuwa eti ni yetu. Makaa yale ni ya kampuni ya mtu fulani na serikali inaambulia kodi. Serikali isimfanyie huyu mtu biashara ila iachie sera ya soko huria ifanye kazi.

Kama ni bei ashushe ili anunuzwe kwa kushawishi na si kutumia rungu la serikali. Kama gesi ile ingekuwa yetu umeme ungeshuka.

Dangote aruhusiwe kununua makaa kule atakako mradi tu azalishe sementi kwa bei inayokubalika, alipe kodi stahiki na aendelee kutoa ajira kwa watanzania.

Habari ya kuwa amnunuze mwenzetu makaa yake ya mawe tuachane nayo!

Pia Dangote amekuwa akiuza sementi yake kwa bei ya chini inayomjali mtumiaji maskini. Isije ikawa hii ni mbinu ya washindani wake kumvuruga ili waendelee kuuza sementi kwa bei ya juu kivile!
Arguments zako ziko poa sana kaka.
 
Hawa jamaa wote majipu tu. Kwahyo alikuwa anatuficha ili iweje??? Kma makaa ya mawe yapo ya kutumika zaidi ya miaka 200, kwann wasipunguze gharama kwa wote wanaoyatumia ili wapambane kwny beinza cement zao sokoni....!!! Cement ikiwa juu, mtu wa chini anafaidikaje sasa??? NONSENSE..!!
 
Hi nchi imekosa kiongozi,dangote ni mfanyabiashara mkubwa hawezi kushindwa kununua gesi ya mtwara ila nilichogundua damgote alidanganywa na maccm kuwa atauziwa gesi kwa bei ndio maana akajenga mtwara,sasa alipoingia bwana john pumba magugu akagundu mkwere anahisa nyingi,ndipo dangote akajikuta kwenye uwanja wa mapambano,lakini isiwe shida,dangote kaamua kuagiza makaa ya mawe A.kusini basi wa mwache,kitendo cha kulazimisha dangote anunue makaa ya mawe kutoka mgodi wa makaa ya mawe ambayo Ben mkapo anaumiliki ,niwazi bwana JPM analenga kulitajirishwa Ben mkapo,kiufupi Tanzania si salama kwa uwekezaji,na hakufai kutokana na sasa za maji taka
Kwa hiyo hapo ni mchuano nani ni nani, duh hii nchi yataka moyo kuielewa.!
 
Mtu mwongo ni muongo milele hata akitokea siku akasema ukweli bado ataonekana muongo. na ndio shida ya viongozi wetu wengi.mfano mwingine ni yule 'prof. Muongo'.
 
Atake gesi ya bure kwani yeye kichaa?
waziri sema tulimuahidi kumpa gesi ili kumvutia awekeze ila sasa tumemgeuka.

Kama wale waliopita waliahidi gesi ya bure kwa maslahi yao imekula kwao. Kama hawataki makaa yetu pia watajijua. Bahati yao ardhi wamepewa bure lakini land rent na property tax yetu walipe.
 
Mkuu huwezi kuwa na packages tofauti tofauti. Itakuwa shida
Mkuu nakubaliana nawe kabisa kwa mantiki ya 'lavel playing field'
Lakini anayesema hayo ndiye yule yule aliyetuficha ukweli.

Tunamwamini vipi kama hatudanganyi kuhusu packages? Kuna uwezekano kabisa ni njia ya kumpaka matope, vinginevyo kwanini waziri wa serikali afiche ukweli?

Pili, Dangote alipokuja alijua mazingira ya nishati nchini. Ni mtu mwenye uwezo mkubwa
Huyu ni mtu ambaye deal zake zipo London kwa wajanja wa uwezekaji na pesa za dunia

Kuna uwezekano kulikuwa na makubaliano, alijua yataheshimiwa na serikali
Tuliona akipokewa na viongozi na kupewa kila msaada

Hivyo dhana kuwa anataka vya bure si kweli na hatuikubali. Kwa utajiri wa Dangote kutaka vya bure ni next to impossible, labda rahisi lakini si bure! no!

Tatu, serikali imezua zua mambo. Mara gesi mara makaa mara mitambo mibovu
Kama kuna tatizo serikali isingehangaika haingaika hadi waziri akiri kusema 'uongo'

Tazama video mbili hapo juu halafu uvae viatu vya mwekezaji, utaju nini kinaendelea

Hizo video ni embarassment ya hali ya juu sana kwa nchi

Nne, ukitaka kuliona suala na uzito wake ,wanaotuambia viwanda wamekaa kimyaaa

Wanajua kuna maswali kuhusu makubaliano ya awali kati ya serikali na Dangote


Kuna tatizo kubwa sana, tunachokiona na mhangaiko tu ya kuficha ukweli
Tusifukue makaburi
 
Mkuu chukua chupa ya value nakuja kulipa
Huyuu Dangote wanae mshadadia is nothing nakwambia hamnaa chochote pale hamna weledi ni ujanjaa ujanja
Wamejaza wahindi tuuu na hakuna faidi tunayoo ipata watanzania zaidi ya hizo ajira tu
Kwanza Dangote ni mfanyabiasharaa kaja kijanja janjaa sana
Kiukweli haingii akilini apate gesi, ardhi. Lime stone hat gypsam nayo aseme anataka yeye kuimport hakuna nchii mfilisi namna hiyoo
Aksante magufuri wetu for this aisee
Wekeni akiba ya maneno mnapo deal na waziri mficha "ukweli"!
 
Kunaweza kuwa na ukweli katika hili. Makaa ya mawe ya hapa yanasemekana hayana ubora wa kutosha. Hivyo yanaweza pia kuongeza gharama za uzalishaji. Kwani akiagiza kutoka nje anatumia pesa ya serikali?
Lazima yatumike!!!! kama hayawaki vizuri tutawashia mafuta ya taa na tutatafuta idadi ya watu wa kupuliza mpaka yawake
 
Kumuamini Mhaya, ni sawa na kumuamini SHETANI..!!

Mpiga sound huyu..!!
 
Back
Top Bottom