Waziri Mwigulu Nchemba apiga marufuku safari za nje kwa wote waliotajwa kwenye sakata la mchanga

Beira Boy

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
17,978
2,000
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba apiga marufuku safari za nje ya mipaka ya nchi kwa wote waliotajwa kwenye sakata la mchanga isipokuwa kwa kibali maalum kutoka Serikalini.

======

Hakuna uzalendo zaidi ya kulinda rasilimali za Taifa, Hakuna utetezi wa wanyonge zaidi ya kulinda rasilimali zao. Hongera sana Mh.Rais kwa uzalendo wa vitendo kwa Taifa letu.

Naelekeza wote waliotajwa kuhusika hakuna kutoka nje ya mipaka ya nchi yetu isipokuwa kwa kibali maalum kutoka serikalini. Vyombo vitekeleze maagizo ya Rais kwa utimamu.

Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi.
12/06/2017
 

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,471
2,000
June 12, Rais Magufuli amekabidhiwa ripoti ya pili ya mchanga wa madini ambayo imebaini uwepo wa mikataba mibovu inayoitia hasara serikali, ambapo kamati imetoa mapendekezo 21 ikiwemo kuchukuliwa hatua kwa wote waliohusika na ubadhirifu huo.

Ripoti iliyonifikia muda huu kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amewazuia wote waliotajwa kwenye ripoti hiyo kutoka nje ya mipaka ya Tanzania hadi vyombo vya dola vitakapofanya kazi yake kwa mujibu wa agizo la Rais JPM.

Waziri Mwigulu amesema “Hakuna uzalendo zaidi ya kulinda rasilimali za Taifa, Hakuna utetezi wa wanyonge zaidi ya kulinda rasilimali zao. Hongera sana Mh. Rais kwa uzalendo wa vitendo kwa Taifa letu

Naelekeza wote waliotajwa kuhusika hakuna kutoka nje ya mipaka ya nchi yetu isipokuwa kwa kibali maalum kutoka serikalini. Vyombo vitekeleze maagizo ya Rais kwa utimamu. Waziri Mwigulu Nchemba
 

Beira Boy

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
17,978
2,000
"Mwiguru" ana mamlaka gani ya kupiga marufuku safari za watu.
Mambo ya nje ndio wangenyanganya passport zao ndio ningewaelewa.

Haya tuambie mwiguru ndio nani.
Niko nakusanya data kamili tarifa kamili naleta mkuu usiogope
 

Hplary

Member
Mar 31, 2017
68
125
Atakuwa ametumwa kufanya hivyo kwa serikali hii sidhani kama waziri mwenye dhamana ya ulinzi anaweza speed ya 4g
 

ZULUECO

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
587
250
"Mwiguru" ana mamlaka gani ya kupiga marufuku safari za watu.
Mambo ya nje ndio wangenyanganya passport zao ndio ningewaelewa.

Haya tuambie mwiguru ndio nani.
Hujui kama passport zinatolewa wizara ya mambo ya ndani idara ya uhamiaji ambayo mwigulu nchemba ndo waziri wake? Sasa mambo ya nje inahusikaje tuhabarishe,, yani nyie bana ni kupinga kila kituuu mnatia aibu
 

lutataza

JF-Expert Member
Jun 14, 2016
869
500
Kwa hiyo kama anau wezo wakupiga marufuku basi atakaye taka kwenda nje amuombe kibali
 

Beira Boy

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
17,978
2,000
Wazir wa mambo ya dan ya nchi mheshimiwa mwigulu nchemba amempongeza muheshimiwa rais kwa kaz nzur anazofanya na jitihada kubwa za kupambana na wahujumu uchumi

Vilevile amepiga marufuku kutoka nje ya mipaka na safali za nje kwa wote waliohusika na kutajwa kwenye sakata la mchanga
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom