Waziri Mwigulu Nchemba aiomba USAID kuelekeza msaada wa dola bilioni 1.3 za NGO's kwenye miradi ya kipaumbele ya Serikali ya Awamu ya Sita

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
EF98094E-AAEC-40DD-92CF-7750637D39FC.jpeg

Na. Eva Valerian, WFM- Dodoma

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameliomba Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani – USAID, kuelekeza kiasi cha msaada wa dola za Marekani bilioni 1.3 sawa na zaidi ya shilingi trilioni 3 inazotaka kuipatia Tanzania kupitia Asasi za kiraia, katika kipindi cha miaka 5 ijayo, zielekezwe kwenye miradi ya kipaumbele ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Dkt. Nchemba ametoa maombi hayo Mjini Dodoma, alipofanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada ya Kimataifa la Marekani (USAID), Bi Kate Samvongsiri.

Alilishukuru Shirika hilo kwa uamuzi wake wa kutoa kiasi hicho cha fedha kupitia Asasi za Kiraia (NGOs) katika kipindi cha miaka mitano ijayo lakini akaeleza umuhimu wa miradi iliyokusudiwa kutekelezwa na asasi hizo za kiraia kuelekezwa katika vipaumbele vya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwemo sekta za afya, elimu, kilimo, na mingineyo itakayochochea ukuaji wa uchumi.

“Tunapoandaa ushirikiano mpya na mipango mipya tunaomba mzingatie vipaumbele vya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambayo amewekeza nguvu kubwa, sambamba na yale mnayofanya kwenye sekta ya afya, elimu, kilimo, mazingira, pamoja na sekta zingine”Alisema Dkt. Mwigulu

Dkt. Mwigulu alisema kwa sasa Mhe Rais anajenga vituo vingi vya afya na hivi karibuni ataajiri watumishi wengi wa sekta hiyo, pamoja na sekta zingine ambazo anazifanyia kazi kama sekta ya elimu na kuiomba USAID kuelekeza fedha hizo ambazo nitapitia kwenye mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), kwenye maeneo hayo.

“Mfano, vituo vya afya vingi vimejengwa na watumishi wataajiriwa, mnaweza mkaweka nguvu kwenye vitendea kazi ambavyo bado havijakamilika ili huduma ziwe zinapatikana na lengo la Serikali pamoja na malengo mliyonayo ya kuendeleza huduma za jamii ambalo mnalo liweze kutimia” Alisema Mwigulu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani -USAID, Bi Kate Samvongsiri, alisema kuwa wanapenda kushirikiana na Serikali ya Tanzania na watakaa pamoja na kuangalia shughuli zinazofanyika katika sekta hizo za elimu, afya, kilimo, maji pamoja na zingine na kuona namna watakavyoziwezesha.

Uhusiano kati ya Tanzania na Shirika hilo la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani USAID, limekuwa na uhusiano wa zaidi ya miaka 50, na kwamba tarehe 30 Septemba, 2016, Shirika hilo lilisaini mikataba mitatu ya msaada yenye thamani za zaidi ya dola za Marekani milioni 635.5, zilizotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii, program ambayo itafikia tamati mwezi Septemba, 2022.
1648236949806_3.jpg

Viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kikao kwa njia ya mtandao kati ya Wizara na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Bi. Kate Samvongsiri, jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise, Kamishna Idara ya Madeni Bw. Japhet Justine, Kaimu Kamishna Idara ya Sera Bw. William Mhoja na Kamishna Msaidizi Idara ya Sera Bw. Mbayani Saruni.
1648236966159_4.JPG

Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Bi. Kate Samvongsiri (juu kulia) pamoja na ujumbe wake, wakiwa katika Kikao na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kwa njia ya Mtandao.

Pia, soma=> Dkt. Mwigulu: Sijasema fedha za AZAKI ipewe Serikali
 
Nilitaka kustuka sana niliposoma hiyo mistari miwili ya kwanza, na kujiuliza: Mungu wangu, tumeuza kitu gani hadi hawa watoe dola kiasi kile kwetu?

Kumbe ni kwa miaka mitano?

Wanaopata mshiko wa aina hiyo kila mwaka kutoka huko huko wanajulikana ni washirika wao wa 'kimkakati' wanaotambulika kama "strategic partners", wengine wakiwa ni majirani zetu hapa.

Moyo ulikwenda mbio sana, lakini sasa umetulia. Hizi ni ahadi tu katika hiyo miaka mitano. Huenda hata nusu yake iwe haijatimizwa katika muda huo
 
Ila watanzania mna vichwa vibovu kabisa. Hivi nyie watu akili zenu mnajielewakweli? USAID ina programs zake Dunia nzima na programs hizo hutekelezwa katika mataifa mengi tu duniani. Sasa serikali ya Tanzania kuiomba USAID kutekeleza miradi katika sekta za kipaumbele , shidanini hapo?
Mkuu, elewa hizo hela hazilengwi serikalini. Madilu mwenyewe amekuwa ni mshamba kutojua hivyo.
 
Ila watanzania mna vichwa vibovu kabisa. Hivi nyie watu akili zenu mnajielewakweli? USAID ina programs zake Dunia nzima na programs hizo hutekelezwa katika mataifa mengi tu duniani. Sasa serikali ya Tanzania kuiomba USAID kutekeleza miradi katika sekta za kipaumbele , shidanini hapo?
Kwa akili yako upewe pesa ndefu hivyo freely.
Halafu jiulize kila msaada wanasingizia huduma za kijamii I.e elimu, afya na maji. Lakini shida iko pale pale miaka nenda.
 
Nilitaka kustuka sana niliposoma hiyo mistari miwili ya kwanza, na kujiuliza: Mungu wangu, tumeuza kitu gani hadi hawa watoe dola kiasi kile kwetu?
Kumbe ni kwa miaka mitano?

Wanaopata mshiko wa aina hiyo kila mwaka kutoka huko huko wanajulikana ni washirika wao wa 'kimkakati' wanaotambulika kama "strategic partners", wengine wakiwa ni majirani zetu hapa.

Moyo ulikwenda mbio sana, lakini sasa umetulia. Hizi ni ahadi tu katika hiyo miaka mitano. Huenda hata nusu yake iwe haijatimizwa katika muda huo

Umesoma pia kuwa huo mkataba ulisainiwa 2016?
 
Ila watanzania mna vichwa vibovu kabisa. Hivi nyie watu akili zenu mnajielewakweli? USAID ina programs zake Dunia nzima na programs hizo hutekelezwa katika mataifa mengi tu duniani. Sasa serikali ya Tanzania kuiomba USAID kutekeleza miradi katika sekta za kipaumbele , shidanini hapo?
Mkuu,
Pesa za corona huduma za kijamii
Hizo za hapo juu huduma za kijamii
Ziara za ulaya huduma za kijamii
Arabuni huduma za kijamii.....

Ila tembea Tanzania hizo huduma za kijamii hazionekani. Aibu sana.
 
View attachment 2165902

Na. Eva Valerian, WFM- Dodoma

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameliomba Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani – USAID, kuelekeza kiasi cha msaada wa dola za Marekani bilioni 1.3 sawa na zaidi ya shilingi trilioni 3 inazotaka kuipatia Tanzania kupitia Asasi za kiraia, katika kipindi cha miaka 5 ijayo, zielekezwe kwenye miradi ya kipaumbele ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Dkt. Nchemba ametoa maombi hayo Mjini Dodoma, alipofanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada ya Kimataifa la Marekani (USAID), Bi Kate Samvongsiri.

Alilishukuru Shirika hilo kwa uamuzi wake wa kutoa kiasi hicho cha fedha kupitia Asasi za Kiraia (NGOs) katika kipindi cha miaka mitano ijayo lakini akaeleza umuhimu wa miradi iliyokusudiwa kutekelezwa na asasi hizo za kiraia kuelekezwa katika vipaumbele vya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwemo sekta za afya, elimu, kilimo, na mingineyo itakayochochea ukuaji wa uchumi.

“Tunapoandaa ushirikiano mpya na mipango mipya tunaomba mzingatie vipaumbele vya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambayo amewekeza nguvu kubwa, sambamba na yale mnayofanya kwenye sekta ya afya, elimu, kilimo, mazingira, pamoja na sekta zingine”Alisema Dkt. Mwigulu

Dkt. Mwigulu alisema kwa sasa Mhe Rais anajenga vituo vingi vya afya na hivi karibuni ataajiri watumishi wengi wa sekta hiyo, pamoja na sekta zingine ambazo anazifanyia kazi kama sekta ya elimu na kuiomba USAID kuelekeza fedha hizo ambazo nitapitia kwenye mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), kwenye maeneo hayo.

“Mfano, vituo vya afya vingi vimejengwa na watumishi wataajiriwa, mnaweza mkaweka nguvu kwenye vitendea kazi ambavyo bado havijakamilika ili huduma ziwe zinapatikana na lengo la Serikali pamoja na malengo mliyonayo ya kuendeleza huduma za jamii ambalo mnalo liweze kutimia” Alisema Mwigulu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani -USAID, Bi Kate Samvongsiri, alisema kuwa wanapenda kushirikiana na Serikali ya Tanzania na watakaa pamoja na kuangalia shughuli zinazofanyika katika sekta hizo za elimu, afya, kilimo, maji pamoja na zingine na kuona namna watakavyoziwezesha.

Uhusiano kati ya Tanzania na Shirika hilo la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani USAID, limekuwa na uhusiano wa zaidi ya miaka 50, na kwamba tarehe 30 Septemba, 2016, Shirika hilo lilisaini mikataba mitatu ya msaada yenye thamani za zaidi ya dola za Marekani milioni 635.5, zilizotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii, program ambayo itafikia tamati mwezi Septemba, 2022.
View attachment 2164409
Viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kikao kwa njia ya mtandao kati ya Wizara na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Bi. Kate Samvongsiri, jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise, Kamishna Idara ya Madeni Bw. Japhet Justine, Kaimu Kamishna Idara ya Sera Bw. William Mhoja na Kamishna Msaidizi Idara ya Sera Bw. Mbayani Saruni.
View attachment 2164410
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Bi. Kate Samvongsiri (juu kulia) pamoja na ujumbe wake, wakiwa katika Kikao na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kwa njia ya Mtandao.

Pia, soma=> Dkt. Mwigulu: Sijasema fedha za AZAKI ipewe Serikali
Dah hizi PhD nyingine ni mgando kabisa, wao Serikali si wanakusanya Kodi so si waendelee kukusanya hizo kodi tena nyingine hutoka kwa hizo asasi ambazo anataka wasipewe pesa.

Hajua kwamba sekta binafsi ndio mwajiri mkubwa dhidi ya serikali?! Asasi zina mchango mkubwa kwa serikali pia kama kutekeleza miradi, ajira, kodi na kadha wa kadha... kuzinyima fursa au kuzipunguzia fursa ya fedha ni kutikisa mchango wa asisa hizo ktk ajira, miradi na kodi nk.

Ndio yaleyale miradi yote itekelezwe na mashirika ya serikali so makandarasi binafsi yafanye kazi gani?!!

Yaani fedha za wahisani kwa asasi ziende serikalini na hayo ma NGO yafanye kazi gani?!

Aibu sana kwa huyo Dkt uchwara... nadhani hajui struggles za NGO amuulize Mhe. SSH!! boss wake maana yeye pia ni zao la hizo asasi!!
 
Safi sana Prof
 
Dah hizi PhD nyingine ni mgando kabisa, wao Serikali si wanakusanya Kodi so si waendelee kukusanya hizo kodi tena nyingine hutoka kwa hizo asasi ambazo anataka wasipewe pesa.

Hajua kwamba sekta binafsi ndio mwajiri mkubwa dhidi ya serikali?! Asasi zina mchango mkubwa kwa serikali pia kama kutekeleza miradi, ajira, kodi na kadha wa kadha... kuzinyima fursa au kuzipunguzia fursa ya fedha ni kutikisa mchango wa asisa hizo ktk ajira, mirad vui na kodi nk.

Ndio yaleyale miradi yote itekelezwe na mashirika ya serikali so makandarasi binafsi yafanye kazi gani?!!

Yaani fedha za wahisani kwa asasi ziende serikalini na hayo ma NGO yafanye kazi gani?!

Aibu sana kwa huyo Dkt uchwara... nadhani hajui struggles za NGO amuulize Mhe. SSH!! boss wake maana yeye pia ni zao la hizo asasi!!
Huyu Mwigulu akili zake sio nzuri.
 
Back
Top Bottom