Waziri Mwakyembe aitumia salamu Bakita

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amelitaka Baraza la Kiswahili la Taifa(BAKITA) kuongeza kasi ya kusimamia maendeleo ya Kiswahili Kimataifa.

Akizungumza leo, Jumanne Agosti 15 alipotembelea ofisi za baraza hilo, amesema Lugha hiyo ina fursa nyingi ikiwamo kutoa ajira nje ya nchi, lakini anashangazwa kuona baraza hilo linasuasua kutumia fursa zilizopo.

Amesema Kiswahili ni lugha ya pili barani Afrika inayotumiwa na taasisi za kimataifa na nchi nyingi hivyo ni muhimu kuongeza tija ya ukuaji wake ikiwamo kutoa mafunzo kwa walimu na wakarimani watakaoendeleza lugha hiyo.

"Mahitaji ya Kiswahili yameongezeka sana, nilitegemea kuona Bakita mnafanya kazi kama mchwa.. ni lazima tubadilike kwelikweli katika utendaji kazi, "amesema Mwakyembe.

Amelitaka baraza kuandaa takwimu za wahitimu wenye shahada ya lugha ya Kiswahili wasio na ajira ili wapewe nafasi ya kufundisha lugha.

Aidha, Waziri Mwakyembe ameahidi kusaidia kuliinua baraza hilo kwa kutatua changamoto zikiwamo za majengo, uhaba wa watumishi pamoja na bajeti.


mwananchi
 
Back
Top Bottom