Waziri Muhongo kukataa Bunge kujadili tetemeko la ardhi Bukoba

Dec 10, 2015
22
70
Ndugu Watanzania, mimi Mbunge wa Bukoba mjini Wilfred M Lwakatare kwa niaba ya wananchi ninaowawakilisha; nachukua fursa hii kupitia andiko langu la wazi kuwashukuru kwa maombi na dua, michango ya hali na mali hasa kipindi tulipopatwa na tetemeko Septemba 10 2016.

Kwa kipekee nivishukuru vyombo vya habari vilivyoujulisha umma hali ya wanakagera na tukapata kuchangiwa misaada mbalimbali kutoka kwa wadau ndani na nje ya nchi. Jopo zima la madiwani liliwasaidia wananchi kwa hali na mali, ikiwepo hata kuweka mahema katika nyumba zetu ili wananchi wapate ahueni.

Tulifarijika na ujio wa Mh Edward Lowassa, Mh Freeman Mbowe, Mh Kassim Majaliwa katika hatua ya kutusaidia na mapema mwaka huu ujio wa raisi Magufuli.

Kilichonipelekea kuandaa waraka huu ni uwajibikaji wa serikali ambao unatupa mashaka makubwa wanaBukoba, tukihisi kutengwa na serikali ya awamu ya tano.

Hii inadhihirishwa na ujio wa Raisi mapema mwaka huu (miezi mitatu baada ya tetemeko), wananchi wa Kagera kutokufikishiwa misaada iliyochangwa kwa ajili yao, serikali kupuuza maombi yangu ya kuomba wanaKagera kupewa msamaha wa kodi katika vifaa vya ujenzi ili wananchi wajenge na kurekebisha maafa katika mejengo na nyumba zao.

Niliiomba serikali itume wataalamu kutoka NHC ili kuwashauri wananchi wajenge vipi nyumba zao ili kuepukana na maafa makubwa kama yaliyojitokeza na hata kushauri vifaa visivyo na gharama katika kujenga nyumba zao. Pia nikaieleza serikali juu ya maafa ya kisaikolojia yaliyowapata wananchi, na kuomba wataalamu kupitia wizara ya afya kufika na kuwapa wananchi msaada wa kisaikolojia lakini hatukufanikiwa. Tuliyoambulia ni serikali kuelekeza pesa yote ya michango katika miundombinu ya serikali jambo ambalo mpaka na kesho na vizazi vijavyo vya wanaKagera vitaihoji serikali.

Tetemeko lililotokea juzi, usiku wa tarehe 30 Mei 2017 halikuwa kali kama lilopita japo limeacha madhara ya nyufa katika nyumba za wananchi na hali ya mshituko,sintofahamu kwa wananchi. Leo nilipoliomba Bunge lijadili kwa dakika ishirini tu hali tete iliyoko Kagera, waziri Sospeter Muhongo amekataa kwa kusema kazi imeshafanywa na kikosi cha tetemeko na ripoti tatu zimeshatolewa ukiwepo mtambo mkubwa wa kitaalamu umeletwa Bukoba.

Mimi kama muwakilishi sina taarifa ya yote haya na baada ya muda mfupi nilipokea andiko lililoandikwa na kusainiwa na Proff Muhongo mwenyewe kwamba patakuwa na kikao cha kamati ya tetemeko kuwasilisha ripoti yake 17 Mei 2017. Nimeambatanisha andiko hilo katika uzi huu.

Mimi kama muwakilishi wa wanaBukoba, nimepokea andiko hilo kama hatua ya serikali kuchukulia hali yetu kiwepesi sana na inatupa mashaka kama kweli serikali ina nia ya dhati katika kutusaidia wanaKagera. Inanipa taabu nikirejea ziara ya raisi John Pombe Magufuli katika jumbo la Hai wiki jana ambako alitamka kuwasamehe wanaHai kwa kutokumchagua. Je, ndivyo anataka wanaBukoba wamwombe msamaha ili serikali iweze kujali hali za wanaBukoba?

Andiko hili kutoka kwa Proff S Muhongo, linanipa wasiwasi mwingi mno. Mualiko huu wa kuhudhuria kikao kitakacholeta kikosi cha tetemeko kuipa halmashauri ya Bukoba ripoti, mualiko usio na muhuri wala format ya barua za serikali yenye kuongozwa kwa mfumo mzuri wa mawasiliano. Hii imenishtua sana na inatupa tafsiri ya tofauti kabisa sisi wanaKagera.

Nichukue fursa hii kuviomba vyombo vya habari viumulike mkoa wa kagera na watu wake ili tuweze kuiamsha serikali juu ya matatizo na hali tete ya wanaKagera baada ya tetemeko la mwaka jana na matetemeko madogo mengine yamekuwa yakifuata baada.

Ndugu watanzania na wanaKagera kwa ujumla, serikali inalo jukumu la kutuhakikishia raia wake usalama na kutusaidia tunapopatwa na maafa. Sisi wabunge jukumu letu linaishia kuishauri na kuikumbusha serikali kutekeleza wajibu wake kwa wananchi.

Ofisi za wabunge ziko bega kwa bega na wananchi katika mambo machache lakini sehemu kubwa ni ya serikali kwa sababu inatumia kodi zetu kutekeleza wajibu wake.

MUNGU AWABARIKI WANAKAGERA, MUNGU AIBARIKI TANZANIA.

Imetolewa na
Wilfred Lwakatare – Mb Bukoba Town.
 

Attachments

  • AndroVid_Slide_01.mp4
    17.6 MB · Views: 32
Jamani wakazi wa Bukoba mmemkosea nini rais mpaka mnanyanyasika kiasi hiki??

Hiyo takataka mfano wa barua aliyoandika Muhongo ni dharau kubwa sana kwa wakazi wa Bukoba.

Hii ni mwafaaa part 2.

Tafadhali media ziamie Bukoba kama zilivyoamia Kolomije, nendeni Bukoba muangazie dunia jinsi sehemu ya nchi ilivyotengwa na kufanywa kuwa kisiwa cha mateso kwa kosa la kuuchagua upinzani.
 
Mheshimiwa mb Rwakatare, nakupongeza sana kwa namna unavyojitahidi kushughulikia janga la tetemeko lilowakumba wana Kagera.
Masikitiko yako ni masikitiko wa Watanzania walio wengi wenye utu na wanaojali na kuthamini umoja na mshikamano wa Taifa letu na utu kwa ujumla. Jamii forums ni miongoni ya mitandao ya kijamii iliyopaza sauti zao kulalamikia kitendo cha serikali kutofikisha michango ya wadau mbalimbali kwa walengwa. Kwa ufupi awamu hii ya 5 ya uongozi wanajua wenyewe ni wapi wanalipeleka taifa hili kwani tumeshuhudia vitendo na matamshi ya kuvunja moyo kama ilivyotokea Kagera na Klm wakati wa ziara ya mwenye mamlaka ya kusema na kutenda lolote. NAKUOMBA USIFE MOYO ENDELEA KUPAZA SAUTI YAKO BILA KUCHOKA, UTAVUNA KWA WAKATI WAKE
 
Mkuu Lwakatare ni kipi hukijui kuhusu unyama wa ccm ? Hivi umesahau jinsi walivyotaka kukumaliza na ile kesi ya kizushi ya ugaidi ?

Wewe ni mbunge , hebu ifanye ofisi yako iwe mratibu wa misaada ya wana Kagera , weka utaratibu tuko tayari kuchangia .

CCM ina roho mbaya mno !
 
Mh Rwakatare mpaka sasa utakuwa umepata picha kamili jinsi CCM hii ya awamu ya tano ilivyo MAKATILI.

Wewe tu Mh walikukosa kosa wakati ule na ile kesi feki ya ugaidi.

Shida hapo ni moja tu kwa wana Kagera kuchagua upinzani. Na tunajua Kagera nzima walishinda UKAWA.. Mama Tibaijuka alicheza rafu za kufa mtu ndio akatangazwa mshindi.

Cha kufanya ni kama alivyo shauri Mkuu Erythrocyte hapo juu iongezee ofisi yako wewee mbunge wa Bukoba mjini na ndio iratibu michango ya wana Kagera.

Sisi watanzania bila kujali tofauti zetu tutachanga.
Kwa heshima yako Mh naomba niwasiliane na wewe inbox kwa maelekezo zaidi.

Hii nchi yetu wote jamani.
 
Mh Rwakatare mpaka sasa utakuwa umepata picha kamili jinsi CCM hii ya awamu ya tano ilivyo MAKATILI.

Wewe tu Mh walikukosa kosa wakati ule na ile kesi feki ya ugaidi.

Shida hapo ni moja tu kwa wana Kagera kuchagua upinzani. Na tunajua Kagera nzima walishinda UKAWA.. Mama Tibaijuka alicheza rafu za kufa mtu ndio akatangazwa mshindi.

Cha kufanya ni kama alivyo shauri Mkuu Erythrocyte hapo juu iongezee ofisi yako wewee mbunge wa Bukoba mjini na ndio iratibu michango ya wana Kagera.

Sisi watanzania bila kujali tofauti zetu tutachanga.
Kwa heshima yako Mh naomba niwasiliane na wewe inbox kwa maelekezo zaidi.

Hii nchi yetu wote jamani.
Kupitia kwa mbunge hata mimi nitatoa mchango wangu.
 
Siamini kama shetani yupo, lakini kama yupo basi ni Magufuli.

Rais anashindwa hata kutoamaneno ya faraja tu kwa wananchi wake?
 
Mie binafsi huwa naamini mkoa wetu ulitengwa na serikali zote. Niliwahi kusema kama Serikali ya Tanzania haikuwahi kuuhitaji mkoa wetu ni vyema wangemuachia M7 akauchukua kuliko kuifanya igeuke jehanamu ya watu walio hai.

Mh. Lwakatare nimelipenda wazo lako na ihusihe Ofisi yako sie tuko tayari, tuiache serikali iendelee na kuifanya Kagera sehemu ya mateso lakini ipo siku. Naamini ipo siku tu
 
Back
Top Bottom