Waziri Mpango: Ubinafsishaji wa Airtel kutoka TTCL, uligubikwa na ukiukwaji mkubwa wa Sheria, Kanuni na Taratibu

Sio airtel tu kuna mambo mengi mheshimiwa anataka ayaweke sawa. Blaablaa ni nyingi mno katika taifa hili changa. JPM kaza kamba
 
Kila siku mnasema nchi inufaike na keki ila badala ya keki mnaleta mawe yaliyorembwa kama keki. Kwendeni huko!

Kwenye madini mumeleta vurugu tupu, TPA nako mkaharibu haribu. Sasa mnageukia makampuni ya biashara! The silent killers!
Hivi bwana mkubwa si alisema tunaichukua airtel sasa imekuwaje tena tujadiliane tupate haki..

Wapumbavu natafuta kiki hawa
 
Ndugu usitegemee Jipya nawasikitikia tu wadanganyika wengi wanavyoimbishwa mapambio
....mimi nilifikiri inapotoka Startment na waliohusika wamesharukiwa kumbe blah blah Work
Hilo nalifahamu sana! Hizi lugha za "lazima tuhakikishe Watanzania wanapata haki zao" tushazisikia sana enzi za Makinikia Season 1&2
 
Sasa anachokiongea huyu potato na alichokiongea rais na wale wazee wa ttcl si kitu kile kile?
Da Mange embu mpe lile tusi ulilompaga kamanda Siro
 
Kama mabilioni ya makinikia na ya kuonyesha nia njema yalivyopita, japo inaskitisha, hili nalo litapita!! Watanzania tutabaki kumeza mate tu!!!! Kuoneana aibu kukri I third! Hata waliohusika katika mambo tunayoambiwa ni ya hovyo wamefanywa siri!! Tuliambiwa serikali ilikuwa inamiliki Kwa 100% Leo tunaambiwa ni 40% !!!!! bila hata kutangua rasmi taarifa na takwimu za awali!!!!
 
sasa mazungumzo ya nini kama kuna ushahidi kuwa taratibu zilikiukwa-nini maana ya serikali? unaanzaje kuzungumza na mhalifu?

Hapa serikali inatafuta faraja ya kisaikolojia tu kwani huyo mhalifu ni yenyewe na si hao wawekezaji wa Airtel. Lugha yenyewe imebadilika. Waliitwa wezi sasa wanasemekana wameonyesha uungwana wa kukaa meza ya majadiliano ili tupate win-win situation!

Hata kwenye makinikia serikali ilienda kukiri mbele ya “wezi” wa Barrick/Acacia kwamba ilifanya makosa kuingia nao mkataba mbovu; wa ovyo kabisa. Sasa wanaomba angalau waungwana wa Barrick waonyeshe “imani” kutoa chochote ili Watanzania warudishe imani kwa serikali yao ya CCM. Sie tusubiri tu kupewa angalau zile bilioni 300 za “nia njema” kwani tumeshaogopa kuwashitaki tusijeangukiwa na MIGA!
 
Jamani hizi sentensi mbili moja kutoka kwa waziri wa fedha Dr Mpango na nyingine kutoka kwa CEO wa TTCL Dr Kindamba zimenichanganya kabisa na kufifisha matumaini niliyokuwa nayo. Hizi sentensi ni tofauti au zinafanana katika jicho la kitaaluma?......nitoeni tongo tongo tafadhali maana ni mambo ya takwimu haya!
 
Tunahitaji tuone watu wakifikishwa mahakamani na kutupwa jela kwa kuisababishia serikali hasara!!!!!!!!

Ingependeza zaidi lakini ndio hivyo tena, hakuna mwenye hiyo jeuri ya kuwagusa hao watu waliofanya mambo ya “ovyo sana” na kutuingiza “mkenge”. Tusubiri tu huruma ya wawekezaji wenye 60% yao.
 
Lakini katika taarifa yake ya jana, Bharti imeonyesha mlolongo wa miamala na matukio kadhaa wakati wa ubinafsishaji ikidai kuwa hiyo inaweza ikaonyesha uwazi uliokuwapo.


Mchakato huo ni ule wa kuanzia kutafutwa kwa mwekezaji ndani ya TTCL kwa ajili huduma za simu za mkononi mwaka 2001 hadi uuzwaji wa Zain kwenda Airtel.


Taarifa hiyo inaeleza kuwa katika kila hatua, Serikali ilikuwa ikishirikishwa na kulikuwa na uwazi mkubwa na matakwa yote ya kisheria yalikuwa yakifuatwa.


“Miamala yote ilikuwa ikifanyika chini ya usimamizi wa bodi ya wanahisa wa MSI, wawakilishi wa Benki ya Dunia, Serikali ya Uingereza, Marekani, Uholanzi na Ujerumani. Makundi hayo ya watu yalishirikishwa ili kuhakikisha maadili na misingi ya utawala bora katika kampuni,” inaeleza taarifa hiyo.


Imemuomba Waziri Mpango kuipatia matokeo ya kamati hiyo kuhusiana na ubinafsishaji wake ili kama kuna hoja zozote iweze kuzijibu kwa hoja kutokana na kumbukumbu za kampuni.
 
Back
Top Bottom