Waziri Mpango: Ubinafsishaji wa Airtel kutoka TTCL, uligubikwa na ukiukwaji mkubwa wa Sheria, Kanuni na Taratibu

Kinachoshangaza ni kuwa tumeambiwa yalifanyika mambo ya hovyo na ya aibu lakini hatujaambiwa ni nani aliyehusika na mambo hayo ya hovyo!! Pia tumeambiwa yatafanyika mazungumzo! Tunafanya mazungumzo na kampuni iliyofaidika na mambo ya hovyo!! Hatujaambiwa watu watakaowajibishwa kutokana na mambo hayo ya hivyo! Tatizo ni kuoneana haya! Mambo haya ya hovyo hufanywa na watu ambao tumeaminishwa kuwa ni wa maana sana!!!
 
sasa mazungumzo ya nini kama kuna ushahidi kuwa taratibu zilikiukwa-nini maana ya serikali? unaanzaje kuzungumza na mhalifu?
Hayo ndo maajabu! Unafanya mazungumzo na watu waliojimilikisha Mali ya umma kwa njia ya hovyo kabisa!! Business as usual!!!
 
Maamuzi mengi yenye msukumo wa kisiasa hayafuati taratibu na sheria na umekuwa utamaduni serikalini ambapo mafisadi hutumia mwanya huo.
Hata hivyo, wengi hufikiri maelekezo ya mkuu wa serikali ni ruhusa ya kukiuka sheria, hiyo ni dhana potofu kabisa.
Maelekezo yote ya kisera yanayotoka juu ni lazima yatafsiriwe na kutekelezwa kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazokuwepo wakati huo.
Tusishangae hata baadaye watumishi wa serikali ya awamu ya tano wakipandishwa kizimbani na hata kufungwa kwa kutofuata taratibu na sheria katika utekelezaji wa siku kwa siku wa kazi zao.
 
Kila siku mnasema nchi inufaike na keki ila badala ya keki mnaleta mawe yaliyorembwa kama keki. Kwendeni huko!

Kwenye madini mumeleta vurugu tupu, TPA nako mkaharibu haribu. Sasa mnageukia makampuni ya biashara! The silent killers!
mkuu umenichekesha sana
 
Mbona taarifa haijaenda mubashara leo? Mi nilijua kesho asubuhi tukiamka zile gari za wakurugenzi tutazikuta zina plate namba zimeanza na SU na pale mbele ya jengo inalala bendera ya taifa, kumbe wanabembeleza mapunjo ya hisa walizouza kwa hiari yao wenyewe na mikataba ipo
 
Kila siku mnasema nchi inufaike na keki ila badala ya keki mnaleta mawe yaliyorembwa kama keki. Kwendeni huko!

Kwenye madini mumeleta vurugu tupu, TPA nako mkaharibu haribu. Sasa mnageukia makampuni ya biashara! The silent killers!
Adi sasa company zote za wazalendo zimesha porwa pesa za mitaji yao sijuwi tuna kwenda wapi wengine wameuza majengo yao ili kulipa pesa TRA !!
 
Duh sijui hawa waliosaini hii mikataba wanaishi mbinguni au wametoka kwenye hi serikali ya chama cha mapinduzi? Mana n ivioja vitupu coz haijawahi kutokea serikali nyingina kuongoza taifa hili ni serikali ileile ya chama chamapinduzi mana waliorizia haya madudu ni wale wanaopigiwa zumari tuwache wapunzike hawa ni wazee wastafu bora watwambie tu wakaungame kanisani na misikitini tuweke mariziano ya kitaifa alafu tuanze moja na katiba ya Warioba bila hivyo tutaishia kuvuananguo na kuchukuliana hatua kwa kubaguana tu lazima tutafakari kama taifa linalotaka kusongambele kwa pamoja
 
Serikali imesema ubinafsishaji wa Kampuni ya Airtel uligubikwa na ukiukwaji wa heria, Kanuni na Taratibu. Mazungumzo kufanyika ili nchi ipate haki yake.

> Kwasasa Serikali inamiliki 40% ya hisa za Kampuni hiyo ambayo inamiliki 60% ya hisa zilizobaki

> Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Kabudi amewasilisha Kanuni za Sheria ya Madini namba 7 ya mwaka 2017 kama alivyotakiwa kufanya hivyo kabla ya Ijumaa na Rais Magufuli

> Vitabu na nyaraka hizo zimepokelewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi
Upuuzi uliopitiliza maana ubinafisishaji ulifanywa na serikali ya CCM. Vipi mashirika mengine na hasarra tulizovuna?

Makosa ya kukataa ushauri wa wataalamu yanaendelea hadi leo kwa sababu ya viongozi wa kuchongwa wasio na taaluma. Mifano Dr Magu mtaalamu wa korosho anatufanyia maamuzi ya nchi kisiasa na uchumi badala ya korosho. Aliyeamua na kusimamia ubinafisishaji wa TTCL hadi kuwa Airtel ni Dr pia ndani ya CCM.

MSITUZENGUE
 
Yaani ukiwasililiza hawa CCM unaweza kudhania nchi hii ilikuwa chini ya CDM au chama kingine kwa miaka 56 iliyopita.

Haya ngoja tuone hicho chetu kwenye airtel. Hivi kwenye madini tumeshapata chetu?

Natania tu mjomba!
Kabisaa
 
Mambo Kama haya maccm wawe wanaambiana wao kwa wao huko lumumba, wanatutamanisha tuseme halafu watukamate kwa uchochezi
 
Kuhusu hizo kanuni, hatujui ilikuwaje katika utawala huu wa ubabe wa JPM, imechukua miezi 7 kanuni hazijaandikwa. lazima kulikuwa na sababu kubwa na pengine ya msingi. lakini leo zimeandaliwa ndani ya siku mbili tatu. kuna siku tutajua sababu...
Hukuelewa taarifa za awali. Tafuta rejea kabla ya kuchangia hoja yako.
 
Kwaakili kama hizi sioni ni kwavipi wajinga mtaisha

Mkuu bora umeona hicho alichosema huyo jamaa na kutoa dukuduku lako. Nimeiona hiyo post yake nikachoka, nilikuwa najiandaa kumpa ukweli wake, nashukuru umewakilisha mawazo yangu tena vizuri kuliko ambavyo ningemjibu.
 
Back
Top Bottom