Waziri Mkuu: Wabunge ndio wana haki na kinga ya kujadili utendaji wa serikali bungeni, sio wananchi

Yaani mwananchi hana haki ya kuhoji halafu kwenye kuomba kura wanarudi kwa wananchi waliowaweka madarakani. Ukiwa shabiki wa CCM Lazima uwe element za utahira
Mkuu hukuwa na sababu ya kutumia lugha za kuudhi, PM kanukuu ibara fulani ktk ama katiba au sheria,
Wewe ungesema ibara hiyo haisemi hivyo alivyoelewa Mkuu...
Bali inasema hivi na hivi...
 
Mnapotosha kama kawaida yenu, hakuna mahali ambapo PM amesema wananchi hawaruhusiwi kuhoji serikali, alichokisema ni kwamba wabunge wana kinga wanapokuwa bungeni, hivyo hawawezi kushitakiwa mahakamani kwa chochote atakachosema akiwa bungeni, hata kama alichokisema ni ukiukaji wa sheria. Mwananchi kwa upande mwingine hana kinga hiyo, anaruhusiwa kuhoji serikali bila kukiuka sheria zilizopo, akikiuka sheria (eg kutukana, kukashifu, kusema uongo) anashitakiwa mahakamani.

Wewe hayo maneno umeyatoa wapi? Angalia tena hiyo clip halafu urudi useme tena. Hapa namnukuu:

1:03 “Kwanza, ibara ya 100 na 101 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imetoa haki na kinga kwa waheshimiwa wabunge ili waweze kujadili na kuhoji utendaji wa serikali kwa uhuru bila mashaka yoyote ya kuweza kushtakiwa wanapotimiza wajibu wao huo wakiwa ndani ya bunge. Kinga ya aina hiyo haijatolewa kwa mwanai-kwa wananchi yeyote yule nchini1:30 mwisho wa kunukuu.

Kauli hiyo ina maana kwamba ipo hatari ya mwananchi yeyote kushtakiwa kwa kosa la kujadili na kuhoji utendaji wa serikali. Ila sishangai sana maana siku hizi viongozi wetu inaelekea hawajui Kiswahili lugha ya taifa vizuri. Wanaongea kwa namna ambayo watu wa kawaida hatuwezi kuelewa hadi ninyi watafsiri mnalazimika kutusaidia.
 
Mkuu hukuwa na sababu ya kutumia lugha za kuudhi, PM kanukuu ibara fulani ktk ama katiba au sheria,
Wewe ungesema ibara hiyo haisemi hivyo alivyoelewa Mkuu...
Bali inasema hivi na hivi...
Ninyi watafsiri wa viongozi ndio mnadai hajatamka maneno kwamba mwananchi haruhusiwi kujadili wala kuhoji utendaji wa serikali yake...japokuwa nina hakika haipo kwenye katiba, lakini ndivyo alivyosema pale alipotamka kwamba "kinga hiyo haijatolewa kwa mwananchi yeyote yule nchini (ya kushitakiwa anapojadili na kuhoji utendaji wa serikali"
 
Naomba uweke hii clip ya Danda Kosovo. Jela ni mbaya.
Uweke na ya "Chadema msitupige mabomu" ni Watanzania wenzenu!.
Nitashukuru kama unaweza kunisadia ule wimbo tuliimba tukitoka Uganda vitani. "Na Amini amekiona kizinga cha moto, kilichomtoa nyoka pangoni mwake". Iddi Amini Jasusi tena hili joka kuu, limefanya uvamizi kuteka ardhi yetu. hatuna kazi nyingine ni kulifunza adabu, ndipo liatakapojua Tanzania ni ya watu".

Nilikaa msituni katika hali ya unyonge. Lakini nilipata nguvu kubwa na kuanza kusonga mbele baada ya kuwakumbuka ndugu zangu, familia yangu na Watanzania niliokuwa nimewaacha huku nyumbani. Walichanga ng'ombe zao, mazao yao na wakaishi maisha magumu, wakiniombea kwa Mungu nipigane vita na nirudi salama. Nilipotafakari, nikaona maisha yangu hayana thamani zaidi ya mamilioni ya Wtanzania wanyonge ambao mioyo yao yote iliangalia ujasiri na mafanikio yangu katika vita vile. Vita vya mtukula. Vita vya uzalendo!

CHAKAZA
Sijui wimbo wako unahusikaje katika hii coment yangu .. Mimi nilimaanisha kuwa huo wimbo nikiusikiliza naogopa kuikosoa serikali nisije nikaenda jela kwa hizo sifa walizoimba hao wasanii. Sasa naomba ufafanuzi wa huo wimbo wako Mkuu unahusikaje kwenye hiyo coment.
 
Eti mbunge haruhusiwi kutoa hoja zilizojadiliwa bungeni na kuzipeleka kwa wananchi!!
Kwa hiyo mbunge wetu aje jimboni kwetu, alafu tumpe hoja za kwenda kuzijadili huko bungeni na serikali, alafu akirudi Jimboni eti haruhusiwi kutupa mrejesho wa ilichosema serikali!?

Na je diwani wa kata yangu akisikiliza hoja zilizojadiliwa bungeni kupitia kwenye tv alafu akazileta kwetu wananchi tuzijadili hilo litakua kosa pia!? Na kama hilo ni kosa, basi kwanini hawafungii habari za bunge zisitoke kabisa nje ya bunge?

Nilivyotazama hii clip, nikagundua pia imebidi waonyeshe bunge live leo kwasababu walikuwa wanataka wananchi wawasikie walivyokuwa wanaongea mbovu na kuwapaka matope upinzani, na offcourse wanajua wananchi hawatapata hiyo habari vizuri kama wakiacha mpaka irekodiwe na kuwa edited usiku... Hili ni janga aisee, tanzania hatufiki popote siku za hivi karibuni.
 
Wewe hayo maneno umeyatoa wapi? Angalia tena hiyo clip halafu urudi useme tena. Hapa namnukuu:

1:03 “Kwanza, ibara ya 100 na 101 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imetoa haki na kinga kwa waheshimiwa wabunge ili waweze kujadili na kuhoji utendaji wa serikali kwa uhuru bila mashaka yoyote ya kuweza kushtakiwa wanapotimiza wajibu wao huo wakiwa ndani ya bunge. Kinga ya aina hiyo haijatolewa kwa mwanai-kwa wananchi yeyote yule nchini1:30 mwisho wa kunukuu.

Kauli hiyo ina maana kwamba ipo hatari ya mwananchi yeyote kushtakiwa kwa kosa la kujadili na kuhoji utendaji wa serikali. Ila sishangai sana maana siku hizi viongozi wetu inaelekea hawajui Kiswahili lugha ya taifa vizuri. Wanaongea kwa namna ambayo watu wa kawaida hatuwezi kuelewa hadi ninyi watafsiri mnalazimika kutusaidia.
Unachobisha hata sikijui, labda unieleweshe. Wewe unafikiri PM amekosea kunukuu sheria na kwamba mwananchi ana kinga kama ya mbunge aliye bungeni?
 
Uitoe wapi hiyo haki?? Mwisho wa haki yako ni kupiga kura tu basi na kuhusu matokeo unatakiwa uakubali yale yatakayotangazwa na Ndugu Jecha.Ole wako ulete fyoko fyoko utashughilikiwa ipasavyo.
Nyie mnachukulia mambo kirahisi sana. Mkumbuke kuwa Mbunge yeyote ana kinga tu akitoa hoja zake za kukosoa na hata kusema chochote juu ya selikari akiwa ndani ya bunge ili mradi asiwe nje ya kanuni. Ni nani na tangu lini na mtu asie bungeni kujivika ubunge ka si kutafuta uhuru uliopitiliza? Ukitoa hoja zako nje ya humo unatakiwa uwe na habari au maneno yasiyokwaza mtu mwingine vinginevyo jela inakuhusu.
 
Sijui wimbo wako unahusikaje katika hii coment yangu .. Mimi nilimaanisha kuwa huo wimbo nikiusikiliza naogopa kuikosoa serikali nisije nikaenda jela kwa hizo sifa walizoimba hao wasanii. Sasa naomba ufafanuzi wa huo wimbo wako Mkuu unahusikaje kwenye hiyo coment.

Hata mimi sikuambii kwa sababu hutaelewa. Mchana mwema!
 
Halafu baaadae utawasikia wanasema serikali ya wananchi....hahahahaaah hawa wau bhana
 
Bado sijapata jibu na sijui hii serikali inakwenda wapi? kwaana naona bado haijatulia inatapatapa sijajua kwamba hicho ndio kifo chake na inatafuta mahari pakufia.
 
PM kaeleza vizuri, ila mleta mada anataka kupotosha, mleta mada anajua kabisa mbunge akiwa ndani ya bunge,anaweza kusema Kitu chochote lakini hawezi kufunguliwa mashitaka, ata kama ni uongo, zaidi kanuni za bunge ndio zitakazo mshugulikia.. Ila hayo anayo yazungumza bungeni akiyaleta mtaani, na ikawa ni uongo anashitakiwa, mbona lipo wazi hili
Okay mkuu peleka hii kitu kwa msajili ili atakapotoa ufafanuzi azingatie Na hili....ila ni vema kauli za viongozi zikawa zinatolewa kwa lugha ya kueleweka kwa mwananchi wa kawaida....Muda wa kusubiria ufafanuzi wengine hatunao...
 
Huyo waziri mkuu amewahi kusoma katiba ya nchi ya mwaka 1977 au anaropoka kama kawaida yake
 
Sasa naanza kuelewa kwanini wanajiona wako sawa. Kumbe hawaelewi wako madarakani kwa ridhaa ya wananchi.....

This is serious, yaani wananchi hawana haki ya kuhoji utendaji wa serikali yao? Jamani tunaongozwa na watu wasio jua nani kawaweka madarakani.

Hii ndiyo maana jamaa anasema hakuna siasa hadi 2020 tumuache atekeleze ilani yake. Bila kujua hakuapa kwa ilani ya Ccm bali aliapa kwa katiba ya nchi.

Jamani wanasiasa washaurini hawa wanaojaribu uongozi. Wapi Ben, wapi Mzee Mwinyi, nchi mmeiuza kwa wasio jua mamlaka ya wananchi.
 
DU majaliwa katisha hahahahahahahahahahahahaha movie part1 ikiwa n pande za lala salama
 
Back
Top Bottom