DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Waziri Mkuu wa mpito nchini Nepal Sushila Karki ameapa kufuata matakwa ya waandamanaji ya kukomesha ufisadi nchini humo wakati alipokuwa anaanza kazi yake rasmi baada ya kushika wadhifa huo..
Sushila, Waziri mkuu wa kwanza mwanamke Nepal aliye na umri wa miaka 73, alichukua nafasi hiyo baada ya maandamano ya vijana wa Gen Z kumuondoa madarakani mtangulizi wake Khadga Prasad Oli na amepewa jukumu la kuirejesha nchi katika hali ya utulivu kuelekea uchaguzi mkuu ndani ya miezi sita ijayo.
Maandamano hayo yalianza Septemba 8 baada ya serikali kufungia mitandao kadhaa ya kijamii ambapo baadae maelfu ya vijana hao waliojaa hasira waliingia barabarani kupinga pia kile walichokiita ni ufisadi na umasikini.
Soma Pia: Waziri Mkuu wa Nepal ajiuzulu kufuatia maandamano makubwa dhidi ya ufisadi yaliyopelekea vifo vya watu 19