vipik2
JF-Expert Member
- Nov 24, 2011
- 2,803
- 2,185
Vipi kichapo cha jana stroke bado una ndoto za mchana ha ha ha ha ha ha ha!.Kikao cha Ole Medeye ndiyo kilitibua mambo kwa taarifa yako.
[h=2]
Wana jamvi,
kuna kikao ambacho kinaendelea muda huu kwenye ukumbi wa Arusha Technical College.
Awali kikao hicho kiliitishwa kama kikao cha wazee wa kimasai yaani Malaigwanan.
Baada ya muda agenda ya kikao kikawekwa mezani, ambapo Waziri Ole Medeye ndiye alikuwa mzungumzaji mkuu katika kikao hicho, akawaambia wazee kuwahamisisha vijana na akina mama wa kimasai kuhakikisha ccm inashinda kwenye uchaguzi wa jumapili.
Mzee Moja akasimama, akasema wao walijua ni kikao cha kimila, kumbe ni kikao cha kisiasa. Akasema wao kama malaigwanan jukumu lao ni kuwafundisha vijana na jamii uadilifu, siyo chama gani wakipigie kura. Mzee Mwingine akasema mbona mnatuletea mambo ya Monduli?
Ole Medeye akatetea point yake kuwa lengo ni kurudisha uongozi wa arusha kwa wenyeji, na anaomba wazee waungane na ccm kumpinga mbunge Lema ambaye ni Mchaga. Ole Medeye amewaambia kuanzia sasa wenyeji (wamasai) wasiwauzie tena viwanja wageni hasa wachagga, na wakatae kutawaliwa na wachagga kuanzia sasa.
Mzee wa kimasai mwingine akasema wao hawako tayari kufanya ubaguzi wa kikabila, kwasababu na wao pia wamehamia sehemu tofauti na wamejenga, wengine ni viongozi mpaka nje ya nchi kama Ole Naiko.
Ndugu wanajamvi,
Hii ndiyo siasa safi ya ccm kuwagawa watu kwa kabila na dini zao, wameishiwa hoja badala yake wameamua kuwatenganisha kwa tabaka.
Kikao kinaendelea tutawajuza. Ila Wazee wamekataa kuandamana kumpinga mbunge Lema. Kuna vijana wengi sana wapo kwenye kikao, nadhani baada ya muda mgawo ukianza kutembea tutasikia kauli ya vijana wenzetu.
Hivi ninapotuma taarifa hii, kuna taarifa nyingine kuwa OCD ameagiza Red Brigade pamoja vijana wote wenye element ya chadema kukamatwa na kuwekwa ndani mara moja.
Hiyo shughuli kimsingi ilishaanza tokea jana usiku baada ya kikao cha OCD na Viongozi wa CCM chini ya uenyekiti wa Stephen Wassira na Ole Medeye kilichofanyika SG Resort
Nitaendelea kuwajuza kinachojiri kwenye kikao cha technical