Waziri Mkuu Pinda akataa kugombea tena Ubunge

Waziri Mkuu Pinda akataa kugombea tena Ubunge

Shobi

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2015
Posts
3,401
Reaction score
4,389
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekataa ombi la
wananchi wa jimbo lake la uchaguzi la Katavi la
kumtaka agombee tena ubunge katika jimbo hilo ili kuendeleza mipango mbalimbali ya maendeleo
aliyoianzisha.
Akizungumza baada ya Ibada ya Jumapili katika kigango cha Kanisa Katoliki cha Kibaoni wilayani Mlele (Jumapili,
Julai 19, 2015), Waziri Mkuu Pinda amesema
anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopewa ya
kulitumikia Taifa akiwa Waziri Mkuu kwa miaka minane na anaamini wakati umefika wa yeye kuwaachia wengine
nafasi ya ubunge wa jimbo la Katavi.
Amesema yeye ataendelea kuwa karibu na wananchi wa
Katavi wakati wote na kwa vile atakuwa na muda wa kutosha atashiriki kikamilifu katika mikakati mbalimbali ya kuwaletea maendeleo wananchi ili waweze kujikwamua kutoka kwenye umaskini.
Mheshimiwa Pinda aliwaasa wananchi wa jimbo la katavi wawe makini katika kuchagua mbunge na madiwani na kamwe watoa rushwa na wabadhirifu wasipewe nafasi katika uchaguzi ujao.
Akimshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu, Paroko wa
Parokia ya Usevya wilayani Mlele, Padri Aloyce Nchimbi
aliwaasa wananchi wa Wilaya ya Mlele kumuenzi
Mheshimiwa Waziri mkuu, Mizengo Pinda hata
atakapokuwa amestaafu kwani bado watahitaji busara na uzoefu wake katika kujiletea maendeleo.
Waziri Mkuu yuko kijijini kwake Kibaoni, wilayani Mlele kwa ajili ya mapumziko mafupi.
Leo saa 10 jioni ndiyo mwisho wa kurejesha fomu za ubunge ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
 
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekataa ombi lawananchi wa jimbo lake la uchaguzi la Katavi lakumtaka agombee tena ubunge katika jimbo hilo ili kuendeleza mipango mbalimbali ya maendeleoaliyoianzisha.Akizungumza baada ya Ibada ya Jumapili katika kigango cha Kanisa Katoliki cha Kibaoni wilayani Mlele (Jumapili,Julai 19, 2015), Waziri Mkuu Pinda amesemaanamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopewa yakulitumikia Taifa akiwa Waziri Mkuu kwa miaka minane na anaamini wakati umefika wa yeye kuwaachia wenginenafasi ya ubunge wa jimbo la Katavi.Amesema yeye ataendelea kuwa karibu na wananchi waKatavi wakati wote na kwa vile atakuwa na muda wa kutosha atashiriki kikamilifu katika mikakati mbalimbali ya kuwaletea maendeleo wananchi ili waweze kujikwamua kutoka kwenye umaskini.Mheshimiwa Pinda aliwaasa wananchi wa jimbo la katavi wawe makini katika kuchagua mbunge na madiwani na kamwe watoa rushwa na wabadhirifu wasipewe nafasi katika uchaguzi ujao.Akimshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu, Paroko waParokia ya Usevya wilayani Mlele, Padri Aloyce Nchimbialiwaasa wananchi wa Wilaya ya Mlele kumuenziMheshimiwa Waziri mkuu, Mizengo Pinda hataatakapokuwa amestaafu kwani bado watahitaji busara na uzoefu wake katika kujiletea maendeleo.Waziri Mkuu yuko kijijini kwake Kibaoni, wilayani Mlele kwa ajili ya mapumziko mafupi.Leo saa 10 jioni ndiyo mwisho wa kurejesha fomu za ubunge ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Biashara yake kwisha..hakuna ZZK wala yule mjinga wa kule kwake awaliopeleka ujumbe apite bila kupingwa.Makinda nae hayupo bungeni kumkinga na maswali bungeni.Kwa ujumla huyu jamaa ni mchovu sana.
 
Pinda waambie wananchi wako Wahame CCM maana hata wewe umeshushiwa heshima kwa kuzidiwa na kinda wa juzi January Makamba
 
Kauli zake za kutaka raia wema wapigwe tu zilifanya kazi ya kamati ya maadili iwe rahisi katika kukata jina lake.
 
Kama alishindwa kushirikiana nao kuwaletea maendeleo na kuwakwamua kiuchumi akiwa Mtumishi wa Ikulu kwa muda mrefu tu, Mbunge, Waziri na Waziri Mkuu atawezaje kuyafanya hayo akiwa Mwanakijiji/Mwananzengo wa kawaida?
 
Kukatwa kubaya jamani
Kama ilivyo" wapigwe tu "
 
Hawa wote ndio wale wanaopewa madaraka kama wakina Magufuli.. Mwisho wa siku hawaelewi kwanini waliingia kwenye siasa kwani wanatumikia matumbo ya wajanja wachache ndani ya serikali na kulinda maslahi yao. Keshapata kiinua mgongo chake toka kwenye hela za wavuja jasho sasa hataki tena siasa. Unafiki m'baya sana na mungu atakuja kuwapa adhabu.
 
nimekwambia usinikate..ww ukanikata..ntasusa tu ..eeh mana hakuna namna
 
Back
Top Bottom