Kukatwa kubaya sana naona bado anafikiria ana kosa gani zaidi ya makamba.
Makamba aliachwa ili kumsindikiza the chosen one.
Kukatwa kubaya sana naona bado anafikiria ana kosa gani zaidi ya makamba.
Haya maswali nenda kamuulize Ndg Zakia meghji, Ndg Marry Nagu,Ndg Nimrod Mkono ndio watakujibu kwa ufasaha zaidi.
Mkuu naona unaweweseka unahasira za kukatwa!
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekataa ombi la
wananchi wa jimbo lake la uchaguzi la Katavi la
kumtaka agombee tena ubunge katika jimbo hilo ili kuendeleza mipango mbalimbali ya maendeleo
aliyoianzisha.
Akizungumza baada ya Ibada ya Jumapili katika kigango cha Kanisa Katoliki cha Kibaoni wilayani Mlele (Jumapili,
Julai 19, 2015), Waziri Mkuu Pinda amesema
anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopewa ya
kulitumikia Taifa akiwa Waziri Mkuu kwa miaka minane na anaamini wakati umefika wa yeye kuwaachia wengine
nafasi ya ubunge wa jimbo la Katavi.
Amesema yeye ataendelea kuwa karibu na wananchi wa
Katavi wakati wote na kwa vile atakuwa na muda wa kutosha atashiriki kikamilifu katika mikakati mbalimbali ya kuwaletea maendeleo wananchi ili waweze kujikwamua kutoka kwenye umaskini.
Mheshimiwa Pinda aliwaasa wananchi wa jimbo la katavi wawe makini katika kuchagua mbunge na madiwani na kamwe watoa rushwa na wabadhirifu wasipewe nafasi katika uchaguzi ujao.
Akimshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu, Paroko wa
Parokia ya Usevya wilayani Mlele, Padri Aloyce Nchimbi
aliwaasa wananchi wa Wilaya ya Mlele kumuenzi
Mheshimiwa Waziri mkuu, Mizengo Pinda hata
atakapokuwa amestaafu kwani bado watahitaji busara na uzoefu wake katika kujiletea maendeleo.
Waziri Mkuu yuko kijijini kwake Kibaoni, wilayani Mlele kwa ajili ya mapumziko mafupi.
Leo saa 10 jioni ndiyo mwisho wa kurejesha fomu za ubunge ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
huu ni muda wa akina wasira kuiga, sio wamekuwa ving'ang'anizi mpaka wafie humu kama mgabe.
kumbuka wasira ni mkubwa kwa pinda kwa miaka 3.
na sitta pia nae apumzike asiwe kama malecela.
hahaa! mkuu ni kweli hata mimi niliisikiliza hiyo kitambo.![]()
Kweli Mh. Wassira pia asikilize maono ya Makongoro Nyerere na wana-JF '' Ngatuka ! Nyerere, Mwinyi, Mkapa ...... wanaachia madaraka Wassira yupo...'' https://www.youtube.com/watch?v=P5etsCfXO1M