Waziri Mkuu na mbao za madawati: tusije ongeza tatizo

Mwanagenzi

JF-Expert Member
Sep 11, 2006
723
241
Waziri Mkuu na mbao za madawati: Tusije ongeza fursa za rushwa

Katika hotuba yake ya bajeti, Waziri Mkuu ameagiza kuwa kuanzia sasa mbao zinazokamatwa (vijijini/na halmashauri/maliasili) zisiuzwe bali zitumike kutengeneza madawati mara moja.

Nimepata maswali kadhaa juu ya mapendekezo haya na ninachelea kuwa inawezekana uamuzi huu ukachochea ufisadi badala ya kuupunguza ambalo nadhani ndiyo nia yake. Kwa mfano:

Je, kila aina ya mbao inafaa kutengenezea dawati?

Mbao zinaposafirishwa huwa zimechanwa au kuchakatwa kwa vipimo tofauti tofauti. Siamini kama utengenezaji wa madawati utatumia mbao za vipimo vyovyote.

Mbao zitakusanywa kwa muda gani ili kuhakikisha madawati kadhaa yanapatikana? Mara nyingi mbao zinapotoka msituni huwa hazijakauka vema kiasi cha kufaa kutengenezea samani.

Kuna hatari ya mbao zinapokusanywa na kukaa bila ya kufahamika lini zitatumika kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

Nashauri badala ya kutumia mbao zinazokamatwa kutengenezea madawati papo hapo au mara moja, basi mbao hizo zitaifishwe na halmashauri (ambao watazipangia matumizi kadri ya mahitaji na kwa wakati muafaka – pengine zaweza kufaa kwa boriti za kujengea zahanati na si kuchongea madawati).
 
Back
Top Bottom