Waziri Mkuu Majaliwa, wanaovuka mipaka bila kutambuliwa na mifumo ya TRA na Uhamiaji ni kubwa sana, nchi inaibiwa

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
890
4,140
Mhe. Waziri Mkuu naomba nikushirikishe mbinu zinazotumiwa na walafi kutorosha Mali za umma kwenda nje. Wezi na mitandao Yao wanaotoroka nchini wameshtuka awapiti airport wanapita kwenye mipaka mfu iliyo wazi ambavyo TRA na Uhamiaji wamelala.

Naamini wapo watu wanalipwa maeneo haya yasiwe na mfumo na wanakata mrabaha mkubwa huko juu waendelee kutorosha Tanzanite kupitia Tarakea, waingize na kutorosha gold kupitia Rukwa na Katavi, watoroshe mapato kupitia maeneo yaliyoachwa bila kuwekewa mifumo na kwenda kutakatisha fedha nje.

Fanya tathimini mipaka mingapi wageni na Watanzania wanatumia mifumo kama ya viwanja vya ndege? Ukianzia bandari ya Dar utaona udhibiti wa mizigo kutoka Zanzibar unavyofanyika ; hii ikupe picha ya hali ilivyo huko mikoani.

Je, wanaokwamisha mifumo isifungwe wanafanya nini ofisini? Mnapataje taarifa za wasafiri na mizigo inayoingia nchini? Unafahamu idadi ya magari yanayoletwa na kudump-wa Tanzania kisha wahusika wanarejea kwao? Unafahamu bidhaa kiasi gani zinaingizwa kutokea bandari ya Dsm nakuzungushwa kwenda nje ya nchi kisha kurejeshwa nchini?

Naamini Unayo nguvu na mamlaka ya kumsaidia Mhe. Rais kwa kuangalia mianya ya upotevu wa mapato ya nchi kupitia mipika yetu na kufunga mifumo madhubuti

NI fedhea kuangaika na EFD kwa walala hoi huku mkiacha mipaka bila udhibiti......mtazidi kuwanyonya Watanzania kwa makodi mengi huku wageni wakimataifa wakishirikiana na Watanzania wakiendelea kuingiza magendo nchini na kunufaika na soko letu.

Wapo wageni na Watanzania wengi wanaingia na kutoka nchini Bila kuingizwa kwenye mifumo mipakani Kwa Sababu hakuna mifumo.

Fanya dhiara yakushtukiza kwenye mipaka yetu uone Hali ilivyo na namna serikali inavyopata hasara kubwa Kwa kuruhusu magendo ya madeni, rasilimali za Taifa, magari na vyakula.
 
Wapo wageni na Watanzania wengi wanaingia na kutoka nchini Bila kuingizwa kwenye mifumo mipakani Kwa Sababu hakuna mifumo.
Kiutani naweza sema walivaa Buibui kama Lema.

Ila basi, wale wenye kuleta haya madhara hasi ni hao maharamia wa nje ambao kiuahlisia ni matapeli wanaojivika "Wawekezaji".

Na ndio hao hao wenye nia na uwezo wa kutoa Rushwa.....pamoja na kuwa mla rushwa naye pia ni mhujumu hawa "Wawekezaji" uchwara wakomeshwe.

Asipendwe mtu wala kupewa upendeleo kwa sababu ya rangi yake ya ngozi au lugha anayotumia. Tuache ulimbukeni-wa makusudi.
 
Nilidhani utakuja na orodha yenye majina ya hiyo mipaka na namna niaje zinavyo toroshwa.

By the way, hata ukimsanua unajuaje kama mfumo wa zamu hii ni wezeshi na rafiki kwake?
 
Nilidhani utakuja na orodha yenye majina ya hiyo mipaka na namna niaje zinavyo toroshwa....
By the way, hata ukimsanua unajuaje kama mfumo wa zamu hii ni wezeshi na rafiki kwake...??
Umenena vyema, ila sina uhakika kama utaeleweka kirahisi kutokana na jinsi ulivyow asilisha maoni yako.

Waziri Mkuu anayeliliwa hapa, yeye ni nani hadi achukue jukumu dhidi ya watu ambao wanayo ruhusa kufanya wanayofanya?
 
Mhe. Waziri Mkuu naomba nikushirikishe mbinu zinazotumiwa na walafi kutorosha Mali za umma kwenda nje. Wezi na mitandao Yao wanaotoroka nchini wameshtuka awapiti airport wanapita kwenye mipaka mfu iliyo wazi ambavyo TRA na Uhamiaji wamelala.

...
Waache wafanye ivo,..TRA na Uhamiaji wanaboa kwa Urasimu,..
 
Umenena vyema, ila sina uhakika kama utaeleweka kirahisi kutokana na jinsi ulivyow asilisha maoni yako.

Waziri Mkuu anayeliliwa hapa, yeye ni nani hadi achukue jukumu dhidi ya watu ambao wanayo ruhusa kufanya wanayofanya?
Haiwezekani wezi na majambazi yaliyotamalaki nchini haya julikani, yanajenga mahekalu na apartments Kigamboni
 
Naamini wapo watu wanalipwa maeneo haya yasiwe na mfumo na wanakata mrabaha mkubwa huko juu waendelee kutorosha Tanzanite kupitia Tarakea, waingize na kutorosha gold kupitia Rukwa na Katavi, watoroshe mapato kupitia maeneo yaliyoachwa bila kuwekewa mifumo na kwenda kutakatisha fedha nje.
Tulitegemea PM aje na takwimu za watu walokamatwa na kuwekwa ndani badala ya kulalamika jukwaani
 
Nchi kawaida yake, mifumo yote inapaswa kuwa macho!

Kuna watu huwa wanalia saana kuhusu uhuru wa Vyombo vya Habari, sasa wako huru, lakini je, wamefanya nini juu ya haya? Wapo kimya

Mkuu wa nchi, Wananchi, vyombo vya usalama, Vyombo vya Habari n.k, kila mmoja akushika zamu yake, nchi itakuwa salama

Nchi hii ni yetu sote, tukiamua, tunaweza
 
Yeye ndio mtendaji mkuu wa Serikali halafu analalamika,sisi ambao hatuna lolote tufanye nini sasa?

?
 
Nilidhani utakuja na orodha yenye majina ya hiyo mipaka na namna niaje zinavyo toroshwa....
By the way, hata ukimsanua unajuaje kama mfumo wa zamu hii ni wezeshi na rafiki kwake...??
Hata huyu anayejulishwa mna uhakika atashuguulikia? Mara ngapi anakamata watu anawatangaza dhambi zao hadharani halafu stori inakufa Kifo cha mende siku hiyo hiyo?
 
Wa identify maeneo yenye matatizo na wa employ manpower ya kutosha.
 
Serikali yenyewe Inastua Sua kuajiri hao watu wanategemea nini? Watumishi wa TRA na Uhamiaji wanatakiwa kuongezwa Ili wafikie maeneo yote ,hii Nchi ni kubwa.
 
Huyu ni mtendaji mkuu WA serikali, anawajibika kujua serikali imetoboka wapi aweze kuziba penye nyufa.

Tusipomshirikisha atatoa wapi mikakati yakuziba mianya?
 
Back
Top Bottom