Waziri Mkuu Majaliwa, njoo Tanga usikilize kero za Wananchi

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
2,377
3,154
Huu ni ujumbe kwa mh. Majaliwa Kassim waziri mkuu wa serikali ya awamu ya tano.
Maumivu na uchungu alivyovipata Moro akifika Tanga anaweza akashangaa na hatimaye kulia kabisa

Ukija kwenye migogoro ya ardhi,utasikitika maana ilianza kutengenezwa na mkurugenzi,maafisa ardhi na mwanasheria wa jiji. Wameuza viwanja vya watu na kubadili hati za viwanja na kuwaacha watu katika hali ya sintofahamu.

Ukija kwa idara nyingine utashangaa sana,wanafanya kazi kwa mazoea wanalindana wao kwa wao hawajali haki za wenzao bali wanaangalia mambo yao
Wakazi wa Tanga walio wengi hawawajui viongozi wao kama vile mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya nk hivyo inamaanisha kero hazitatuliwi maana hata wakati wa kero za ardhi wakaazi wa maeneo yenye kero hawakuruhusiwa kuwaeleza viongozi wao kero hizo

Hii nikwasababu RC alibariki zoezi la kuuza viwanja kwa mara ya pili tena kwa mita za mraba(square miter) bila hata kuwasikiliza wananchi wala baraza la madiwani kujadili na kuwafikishia wananchi. RC nae ninadhani alidanganywa na mkurugenzi akajikuta amefanya makosa makubwa. Ninadhani kama utawaacha wengine lakini mkurugenzi katika hili hutovumilia matatizo yake na jamaa zake bwana ardhi anayeitwa Tonny na mwanasheria wa jiji

Mh Majaliwa ukifika Tanga tembelea maeneo ya Pongwe,Kasera,Masiwani,Amboni,Nema,Mkulumuzi. Usikubali wakakujazia watu kwenye uwanja wa Tangamano.
Usikubali pia wakakuzonga ukidhani wanaupendo sana. Kwenye vikao vya ndani watakudanganya kama alivyodanganywa Lukuvi na akajikuta anaacha mgogoro wa ardhi ukiwa mkubwa zaidi kuliko alivyo ukuta maana aliridhia watu waliojenga walipe kwamara ya pili. Yaani zimepigwa dili za ardhi hadi usiku ardhi imeuzwa ikimaanisha kukithiri kwa rushwa miongoni mwao

Waandishi wa habari pia nitatizo maana hawaripoti haya mambo ingawaje wanaitwa kwenye vikao vya kero za wananchi bali kidogo ITV wanauthubutu.Hapo kila mwenye utashi atajua sababu ni zipi maana kila mtu anao uelewa wake

Mh waziri mkuu fanya ukaribie Tanga yaani kero ni nyingi, ukifika tembelea mitaa kadhaa wala wasikuzonge na maneno,wakajifanya ni makada watiifu na wafia chama,ukiwaelewa hivyo watakua wamekuwahi

Wapo mawaziri wanafika Tanga na wanaondoka bila hata kuyagusa matatizo ya wananchi kwakuwasikiliza. Wanaondoka kama walivyokuja wanaambiwa Tanga nisafi

Mh majaliwa njoo usaidie kufanya usafi hasa wa jiji zima na mkoa kwa ujumla maana kama umestaajabu ya Moro ya Ta yatakuliza kabisa

Nimawazo yangu,nisishambuliwe
 
Yssni ingekua vyema hata akaja kwa kuwashitukiza maana wapo wanaojivunia kwamba hata wakija hawatakua na uthubutu wa kukemea, nadhani wana mbinu za kuwafanya viongozi watulie
Tatizo kubwa Tanga watumishi wengi wa Serekali wana njaa sana hadi wanashirikiana na watu wenye visenti kuwazulumu masikini hicho kidogo walichojaliwa!!
 
Tanga wamehiludisha nyuma kwakweli kwamfano kijiji kama mapojoni hakina humeme kabisa
 
Back
Top Bottom