Waziri Mkuu Majaliwa na uhalali wa maamuzi hadharani

ntemintale

JF-Expert Member
Sep 6, 2016
952
1,872
Tumeshuhudia Waziri Mkuu Majaliwa, akikemea hadharani, watuhumiwa (Innocent Till Proved Guilty Under the court of law) Kwa Mujibu wa Vyanzo vyake. Watuhumiwa Hao Wa makosa mbalimbali, Ni watendaji Wa Kada za Chini Na za kawaida, Hasa Tamisemi, Elimu. n.k.

Japo kukemea kunarekebisha Tabia, lakini Kuna tatizo lililojificha ndani ya tatizo.

Mosi, Waziri Mkuu Ni Mtendaji Mkuu Wa shughuli zote za kila siku za Serikali. Je, Yeye Kama Mkuu, anakuwa wapi kusimamia na kuhakikisha Kuna Udhibiti (checks & controls) ndani ya Serikali, mpaka tunayoaminishwa kuwa Ni madudu yanatokea?

Pili, Kama taarifa anazopata Ni sahihi, Je Hao wanaopaswa kukamata, kushitaki Na kutoa haki wanakuwa wapi, mpaka wasubirie aje yeye amtaje mtuhumiwa, ambaye bado hajafikishwa mahakamani, kuwa Ni mkosaji?

Je, hizi Sio staged events (matukio ya kupangwa) ili kutuhadaa Sisi wananchi?

Je, mahakama ikimkuta mtuhumiwa Hana hatia, Waziri Mkuu atarudi Tena kutupa taarifa kuwa yule mtuhumiwa niliyemhukumu hadharani Hana hatia. Je pernality damage anayoifanya Kwa mtuhumiwa itafidiwa namna gani?

Je, Mamlaka ya Waziri Mkuu, ya kuwajibishana ndani Kwa ndani yamekuwa hafifu namna hiyo mpaka yapewe nguvu Na vyombo vya habari?

Je, Kuna muunganiko Mzuri kweli Kati ya Mamlaka ya Waziri Mkuu Na Mawaziri, Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu Na Manaibu Makatibu Wakuu Wa Wizara husika? Wao wanakuwa wapi kukemea hayo, au wanamuacha aje atengeneze Jina Kwa wananchi?

Je, hizi ni kampeni za kuniaminisha kwa wananchi kuwa ni mchapakazi?

Nawasilisha.
 
Hivi unafikiri hiyo kazi ni rahisi?,hebu kuwa mpole kidogo
Kwa Mamlaka ya Waziri Mkuu, anayo nguvu kubwa kuwawajibisha watendaji ndani Kwa ndani bila kupiga makelele. Uchunguzi unafanyika, ushahidi unapatikana, mtu anakamatwa, anafunguliwa kesi, anahukumiwa Na mahakama Kwa haki, anatumikia kifungo.

Hapo Sasa hata akienda Hadharani kumtaja mhusika ambaye tayari kahukumiwa inakuwa Na mshiko. Hii ya kutangaza mtuhumiwa ambaye bado hajathihitishwa Na mahakama kuwa Ni mkosaji, tenahadharani, Kisha unatoa Amri akamatwe, Kuna kasoro ndani ya Nia Thabiti.

Na Tena unakuwa umejibebesha Mamlaka ya Mahakama YA kuhukumu mtuhumiwa, ambaye endapo atathibitika Hana hatia, Basi unakuwa umesababisha personality damage kubwa, at the expense ya kujibebea umaarufu.
 
"ndugu wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM......katika serikali yangu Kuna watu wanalegalega, hawaendi na kasi yangu. Naomba Kibali chenu nikaipange serikali yangu" Hii ni kauli ya Samia Suluhu Hassan katika mkutano mkuu wa CCM Dodoma.

Nadhani kauli hii imemtia wenge Waziri Mkuu, ameanza kuzunguka ili "ajiokoe". Kwa kufanya hivyo, anaandaa matukio, halafu anafanya anavyofanya
 
Hii Nchi ina mfumo ukiofeli maana unategemea uadilifu binafsi wa mtu Sasa kwenye jamii hao waadilifu Ni wachache wanazidiwa na waovh wengi kwa msingi huo muadikifu 1 ataonekana Ni kikwazo kwa wengi Majizi..

Bila kuweka syastem zinazofanya kazi na hapa Katiba itoe Nguvu Wananchi wamchague Mkuu wa Mkoa na wawe na nguvu ya kumuondoa pindi Mambo yakiharibika Tena bila mlolongo Ni just petition kadhaa Basi, Mkurugenzi tunuajiri sie wenyewe asiletwe na Tamisemi maana Madiwani hawana nguvu yeyote kwake.

Lakini huu upuuzi wa kutegemea watu wakupe taarifa ndio uje kujiongelesha na kuwataka wakuchunguza wafanhe kazi Yao haina tija yeyote..

Kwa hili Serikali ya CCM inatukosea sana.
 
Kuna udhalilishaji na kiki, nchi nyingi haziongozwi namna hii (kudhalilisha,kufokea hadharani),na inawezekana Wanakosea lakini hamna mtu wa kuwarekebisha viongozi wavunjao sheria za kiutumishi.

Wengi wafanyao hivi walimuiga mwendazake,ukifuatilia awamu zilizopita viongozi walikuwa hawaingilii majukumu ya watendaji,wala kuwadhalilisha watumishi walio chini yao mbele ya kamera.

Kwani viongozi hawana utaratibu wa kufanya kazi mpaka wasubiri kamera ma vyombo vya habari ili kuonyesha mapungufu ya kiutendaji yaliyopo Serikalini?

Viongozi wamesahau agenda za kuwahudumia na kuwapa majibu ya matatizo yanayowakabili wananchi (ukosefu wa huduma ya maji, barabara,kupanda bei bidhaa mbalimbali bila udhibiti,) badala yake wanafanya maigizo hadharani.

Viongozi wajue yote haya yafanyayo hadharani wananchi wanawachora tu (Viongozi badala ya kutoa majibu ya kero za wananchi,kiongozi anaenda kutoa matamko,kufokea watumishi walio chini yake mbele ya kamera huku akijua anavunja sheria,kanuni na taratibu za nchi),na kusahau wajibu wa nafasi walizopewa.
 
"ndugu wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM......katika serikali yangu Kuna watu wanalegalega.....hawaendi na kasi yangu...
Utapangua safu na Safu Ila Kama Hakuna system zinazofanya kazi Ni kazi bure.

Ufisadi aliuibua PM kwa taarifa yenu uliofanywa chini ya Mwendazake na Wala sio mgeni na umejulikana toka kitambo Ila Hakuna Cha kufanya maana DED wa Sumbawanga mfano ni ndugu wa Magufuli na Ni nyoka..

Kuweka maafisa usalama wa vyeo vya Juu kwenye Ngazi za maamuzi ni upuuzi maana wakipiga Pesa huna Cha kuwafanya hao hao ndio unategemea taarifa kutoka kwao.

Mfano wa mwisho DED wa Kahama alinunua Shangingi kwa makusanyo ya Halmashauri mil.450 na Mwendazake hakuwa na Cha kufanya zaidi ya kijisemesha ooh ameongza makusanyo na blaa blaa za kipumbavu kisa Ni manyoka hao wakipiga Hakuna wa kuwagusa.
 
Kuna udhalilishaji na kiki, nchi nyingi haziongozwi namna hii(kudhalilisha,kufokea hadharani),na inawezekana Wanakosea lakini hamna mtu wa kuwarekebisha viongozi wavunjao sheria za kiutumishi...
Huwa wanafanya hivyo kwa minajiri ya kujikosha kwa Wananchi wajinga wasio na uelewa..

Na huku Ni kufeli kwa system na iko hivyo Nchi nzima..
 
Maswali yako nimeyapenda. Unachosema ni kweli kabisa Nami pia nilishawaza hilo.

Kwa kweli kinachoendelea ni WM kujitafutia uwanja wa kujionyesha kuwa ni mchapa kazi. Kama ni kweli kwa nini amejikita kwa watu wadogo wadogo wa ngazi za chini.

Angeaminika zaidi pale atakapowaibua wale Wateule wanakula kwa urefu wa kamba zao.
 
Maswali yako nimeyapenda. Unachosema ni kweli kabisa Nami pia nilishawaza hilo...
Lazima ajikite kwa watu wa chini kwa sababu huku ndiko Kuna miradi ambayo watu wa kawaida wanaiona na pia ndiko anaweza kukutana naonkwa kiki nk.

Wakubwa hawali kwa kuja kununua material fake no wao mradi ukija wanavuta chao mapema nyie mnaachiwa msala na Hakuna ushahidi wa kuwakamata hata nae anajua Hilo..
 
Kama kuna zawadi mtu yeyote aweza kutupatia sisi watanzania ni kujenga mifumo ya uthibiti isiyoyumba

SIO KWA LICHAMA CCM ! Majizi Hayo hayataki udhibiti ! Hakuna mwana ccm hata mmoja asiye mwizi! Japokua na wale wa vyama vingine wanaweza kua wezi pia maana pia ni wa TZ
 
Back
Top Bottom