Waziri Mkuu Majaliwa na Kagera RC Chalamila Kwangu Mimi Mashujaa wa Ajali ni Marubani na siyo huyu Majaliwa Jackson wenu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,551
108,888
Baada ya Kuzisikia Shuhuda za Wahanga ( ambao Kihabari kama Tasnia ) hawa tunawaita Reliable Source ukiachana na zile mbili za Authority na Credible Sources GENTAMYCINE nasema Mashujaa Wakuu ni Marubani ( Captain na First Pilot ) kwa waliyoyafanya hata kabla Ndege haijaangukia Ziwani huko Bukoba ( Mkoani Kagera ) kwa Watani Wapendwa na Washamba Wahaya.

Shuhuda wa Kwanza....

"Tukiwa Angani zaidi ya mara Nne Rubani alikuwa akitupa taarifa juu ya hali ya Ndege na hatua anazozichukua hasa kutafuta Msaada kutoka Control Tower na uwezekano wa kwenda Mwanza baada ya Tairi za Ndege Kugoma kutoka na kwakweli alijitahidi mno kiasi kwamba hata kule Kuwasiliana nasi Abiria kila mara kulitusaidia kushusha Presha zetu na kutuweka sawa Kisaikolojia na kwakweli japo nimepona ila nimesikitika sana kusikia kuwa Marubani wale wazuri wote hatunao tena duniani ila Mwenyezi Mungu atawalipia zaidi kupitia Familia zao zilizobakia duniani"

Shuhuda wa Pili......

"Sijawahi kuona Marubani Mashujaa kama tuliokuwa nao. Baada ya Rubani kuona hajibiwi ipasavyo na Watu wa Control Tower akaamua kutumia Akili yake ya ziada na ya Kiuweledi ambapo alituzungusha Kwanza Angani kisha akatafuta muelekeo wa Kina kifupi na ambapo pia kulikuwa na Wavuvi wengi akiwa na lengo kuwa hata kama akiipeleka Ndege Ziwani basi msaada wa haraka ungepatikana kutoka kwa Wavuvi kitu ambacho nadhani amefanikiwa kwa 75% ila kilichomkwamisha tu Ndege kumzidi Nguvu na Kutua vibaya hasa ule upande Wao wa Cockpit ya Ndege"

Mjumuisho wangu wa Kimtizamo kama GENTAMYCINE baada ya Kuzisikia na Kuzitathmini kwa Kina hizi Shuhuda Kuu Mbili ni kwamba kama Rubani angepata Msaada mkubwa kutoka kwa Mamlaka ( Control Tower ) na Uratibu wa haraka wa Watu wa Uokoaji na Zimamoto huenda Wao Marubani na hata wale Abiria wengine 17 wasingefariki na Kuwalilia kama hizi Kimajonzi.

Vile vile GENTAMYCINE nimegundua kuwa pamoja na kwamba sasa anayesifika ni Muokoaji Majaliwa Jackson huku akipewa Fedha na Mali kama Zawadi ila kupitia Shuhuda yake Mwenyewe nimegundua kuwa hata Yeye ni sehemu ya Kusababisha Vifo vya Waliokufa kwa kutofuata Maelekezo ya Kiufundi aliyokuwa akipewa na Marubani na badala yake akawa hayafuati na anafuata yake Kienyeji Kienyeji hivyo kuharibu utaratibu mzima wa Kuokoa bila madhara Abiria wote ndani ya Ndege.

Sijashangaa pia kumsikia Muokoaji Majaliwa Jackson aliposema kuwa kuna muda kila alipokuwa akijitahidi Kuokoa na Kuwasiliana kwa Ishara na Marubani na Yeye kufanya yake ( ya Kienyeji Kienyeji ) Wao ( Marubani ) kwa Utaalam na Uzoefu wao wa Uokoaji wakagundua kuwa Jamaa ( Majaliwa Jackson ) ameshakosea pakubwa na hawatopona huku Maji yakiwa yameshaingia kwa Uwingi katika Cockpit yao wakaamua Kumpungia tu mikono ya Kumuaga kuwa hawatopona na Wanakufa huku Kiushujaa kabisa na kwa Kutii Kiapo chao cha Urubani wakimtaka Muokoaji Majaliwa Jackson akawaokoe Abiria ambao ni Wengi na aachane na Wao ambao walikuwa Wawili tu.

Hivyo basi GENTAMYCINE nina Ombi Kubwa kwa Waziri Mkuu na Mkuu wa Mkoa wa Kagera na wale Wadau wa Kutoa Misaada na Michango kuwa hata Familia za hawa Marubani ( ambao Kwangu Mimi hawa ndiyo Mashujaa hasa hata kuliko huyo Majaliwa Jackson wenu ) nazo zipewe Misaada mingi na mikubwa ya Fedha na Mali kwani nina uhakika kuwa bila ya Jitihada zao za kutotua Ardhini ambako Ndege yote ingelipuka na Kuungua vibaya sidhani kama huyu Dogo Muokoaji Majaliwa Jackson angeokoa Mtu na badala yake angetoka patupu tu na kuendelea na Ukapuku ( Umasikini ) wake aliokuwa nao awali kama nilionao nami pia.
 
Baada ya Kuzisikia Shuhuda za Wahanga ( ambao Kihabari kama Tasnia ) hawa tunawaita Reliable Source ukiachana na zile mbili za Authority na Credible Sources GENTAMYCINE nasema Mashujaa Wakuu ni Marubani ( Captain na First Pilot ) kwa waliyoyafanya hata kabla Ndege haijaangukia Ziwani huko Bukoba ( Mkoani Kagera ) kwa Watani Wapendwa na Washamba
Mama isihaka acha wivu na majaliwa kama vipi nikupe namba yake awe boyfriend wako
 
Yaan Genta majaliwa anakuumiza roho
Na Mmoja wa Dereva wake ( katika Msafara wake ) anasema ana hamu ( shauku ) ya kunijua Mimi ni nani na kwanini namuandana mno Yeye halafu ni mwana Simba SC Mwenzangu.

Kwanini namchukia ni kwamba ni Muongo ( a Liar ) wa Kiwango cha Kimataifa halafu huwa anapenda Kukurupuka Kuzungumzia Jambo tena Nyeti ambalo hana Utaalam nalo na wanaompa hufanya hivyo Kumsakizia tu Ili akosee na aonekane ni Kituko na hata Kudharaulika kama ninavyomdharau ( tunavyomdharau ) ila hajishtukii tu.

Abadilike.
 
Baada ya Kuzisikia Shuhuda za Wahanga ( ambao Kihabari kama Tasnia ) hawa tunawaita Reliable Source ukiachana na zile mbili za Authority na Credible Sources GENTAMYCINE nasema Mashujaa Wakuu ni Marubani ( Captain na First Pilot ) kwa waliyoyafanya hata kabla Ndege haijaangukia Ziwani huko Bukoba ( Mkoani Kagera ) kwa Watani Wapendwa na Washamba Wahaya.
Wivu umekujaa
 
Huyo kijana angeingia uoga wa kwenda kuwaokoa hao watu 24 sasa hivi si tungekua tunalia zaidi?

Jitafakari
Marubani wangeamua liwalo na liwe na kuipeleka Ndege Ardhini na ilipuke na Abiria wote Wafe na Kuungua vibaya hivi sasa tungekuwa tunacheka?

Huna Akili jitafakari.
 
Marubani wangeamua liwalo na liwe na kuipeleka Ndege Ardhini na ilipuke na Abiria wote Wafe na Kuungua vibaya hivi sasa tungekuwa tunacheka?

Huna Akili jitafakari.
Marubani ile ni taaluma yao na ndio uwezo wao ulipoishia hapo lakini kijana akaendeleza walipoishia na kuokoa maisha ya watu 24, huyo tayari ni Shujaa na haliwezi kubadilika hilo,

Wewe mwenye akili nenda kamtoe kwenye jeshi la uokoaji
 
Kwa nafasi yake na kwa alichofanya anastahili pongezi tena kubwa, pengine angeamua kupuuza na kuacha kufanya alichofanya saizi angekuwa miongoni mwa watu wanaolaumiwa na hata wewe pengine ungekuwa miongoni mwa watoa lawama, nina hakika pengine hasingetoka hata mmoja hata huo ushahidi ulonukuu usingepata kwa hao majeruhi au idadi ya majeruhi isingekuwa kama ilivyo sasa.
 
Marubani ile ni taaluma yao na ndio uwezo wao ulipoishia hapo lakini kijana akaendeleza walipoishia na kuokoa maisha ya watu 24, huyo tayari ni Shujaa na haliwezi kubadilika hilo,

Wewe mwenye akili nenda kamtoe kwenye jeshi la uokoaji
Nawewe sasa uzae watoto kama shujaa majaliwa sinkuendesha kampeni zako hapa za kupelekewa motoo na majike wenzako
 
Back
Top Bottom