Waziri Mkuu Majaliwa: Akiba ya chakula iliyopo nchini iendelee kudhibitiwa

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,488
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, KASSIM MAJALIWA meagiza akiba ya chakula iliyopo nchini iendelee kudhibitiwa ili kuepukanana hatari ambayo i naweza kujitokeza kutokana na maeneo mengi nchini hajaanza kupata mvua. Undani wa habari hii angalia hiyo hapo chini Video



My take;
Mahindi ni zao la chakula. Mazao ya biashara ni kama pamba, kahawa, katani, mpira, n.k. Wafanyabiashara walionunua mahindi yote kwa wakulima na kuyahifadhi kwa lengo la kutengeneza uhaba wa zao hilo kwa wananchi ili wawauzie kwa bei wanazotaka, siyo wahujumu uchumi? Hivi hawa wana tofauti gani na wale walionunua sukari yote na kufungia kwenye magodown ili watu wainunue kwa bei ya juu? Can you imagine bei ya kilo ya mchele iko sawa na bei ya kilo ya mahindi? Watu wanakufa njaa tuache mzaha.

Serikali ipange bei ya mahindi ili kunusuru watu japo wao ndio wenye makosa kwa kuuza kiholela. Mwananchi aliyekuwa na shida akauza mahindi aliyovuna kwa tsh 200 leo anapata wapi tsh 1000 ya kununua mahindi hayo? Hii biashara ya kufa kufaana haifai.
 
Uthibiti tani elfu 90?......


Kwanini mwezi wa sita Serikali ilikataa kununua chakula kwa wakulima?........
 
Wafanyabiashara walionunua mahindi yote kwa wakulima na kuyahifadhi kwa lengo la kutengeneza uhaba wa zao hilo kwa wananchi ili wawauzie kwa bei wanazotaka, siyo wahujumu uchumi
wataje ili watumbuliwe

tumechoka sasa
 
Full mkurupuko
JK alikua anatoa kiasi cha mahindi toka hifadhi ya taifa ili kudhibiti bei,sasa huyu Majaliwa sijui hata ana mkakati wowote
Kenya waliiona hali hii mapema wakanunua mahindi yetu hata walipokuwa wanavuna,sisi viongozi wetu wanawaza kununua ndege
 
mkuu tunahitaji kuwepo kwa mkakati wa kudumu kwa ajili ya kuondokana na haya majanga ya ukame.Tunahitaji kuwa na storage ya chakula kwa zaidi ya miaka 5 ili kuweza kufanya watu wasiwe na tatizo la njaa.Sisi kwa ujumla wetu tunahitaji roadmap na mkakati wa kutumu na siyo mikakati ya kuzima moto kwa ajili ya kuweza kuweka storage ya Mafuta,Chakula na Pia kuwepo na vyanzo vya kudumu vyanishati
 
Back
Top Bottom