Waziri mkuu Kassim Majaliwa: Tutakomesha rushwa ya ngono vyuoni

Ninashauri UDSM wasahihishe mitihani ya UDOM na UDOM wasahihishe mitihani ya UDSM . Na vyuo vingine vifanye hivyo hivyo.
 
Waziri mkuu Kassim Majaliwa wakati akizungumza kwenye kongamano la kupinga unyanyasaji wa kinjinsia nchini amesema serikali imedhamiria kukomesha rushwa ya ngono vyuoni kwani kwa sasa imekithiri na kuwafanya vijana wa kike wakose uhuru wa kusoma.
Serikali imeamua kuanzisha madawati ya jinsia vyuoni yatakayoshughulikia hali hiyo.

=========

Waziri mkuu, Kassim Majaliwa leo Alhamisi Novemba 25, 2021 amezindua mwongozo wa uanzishwaji wa madawati ya jinsia kwenye vyuo vikuu na vya kati.

Mwongozo huo unalenga kukomesha vitendo vya rushwa ya ngono vinavyoelezwa kushamiri kwenye taasisi za elimu ya juu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Majaliwa amesema nguvu kubwa inatakiwa kuongezwa katika kukabiliana na tatizo hilo linaloathiri vijana wengi wa kike.

Majaliwa amesema vita dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia inapaswa kushirikisha watu wote wanaochukia vitendo hivyo.

Amebainisha hatua ya kuanzishwa kwa mwongozo inaweza kuwa mwarobaini wa kumaliza tatizo hilo la unyanyasaji kwa mabinti waliopo vyuoni.

Ameeleza taasisi za elimu ya juu ni maeneo ambayo mara kadhaa Serikali imekuwa ikipata taarifa za uwepo wa vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.

“Tunahitaji Watanzania kuthamini maisha ya kila mmoja wetu, tunataka kila Mtanzania awe huru, anayesoma asome kwa uhuru."

“Ninaendelea kusisitiza uanzishwaji wa madawati ya jinsia kwenye vyuo vyote. Hii ni ajenda na ilani ya CCM nasisitiza haki na usawa na kuwalinda Watanzania dhidi ya ukatili wa kijinsia," amesema akitumia fursa hiyo kuwataka wadau wa masuala ya jinsia kutumia siku 16 kujadili upungufu wa sheria ili ziboreshwe.

“Maboresha haya yakiletwa yatafanyiwa kazi kwa haraka yakifika bungeni, tunataka Watanzania wote waishi kwa matumaini makubwa."
 
Sawa Yuko sahihi ,lakini madawati ya njisia sio suruhu ya hili tatizo,suruhu ya hili Jambo ni kuondoa mamlaka ya wahusika katika ufaulu wa wanafunzi,na kuwe na mtihani mmoja na msimamizi wa huo mtihani awe Baraza la mitihani,

Yaani iwe Kama tunavyofanya huku mashuleni,uwepo wa madawati ya jinsia hata Kama yatakuwa 100 kwa chuo lakini bado ufaulu wa mwanachuo uko mikononi mwa lecturer bado sio siruhu
University duniani nzima hakujawahi kuwa na mitihani ya Necta. Labda Tanzania tuanzishe
 
Tanzania tukianzisha ina hasara gani? Kuliko kuwa na wasomi wa degree za kuvuana nguo na kichwani ni hewa
Kuna baadhi ya regulations ni za dunia nzima huwezi kujianzishia tuu ilimradi. Halafu course za chuo ni tofauti na Kwa kila chuo. Kumbuka vyuo hivyo hawasomi watanzania tuu kuna hata foreigners
 
Mabaraza wakiwa na msimamo tutafanikiwa

Sio Kweli hakuna kufanikiwa kabisa...
Kitendo cha Mwl kuwa Yeye ndio anaeshikilia Ufaulu wa Mwanafunzi hahaha
Ngoja Nikuambie kitu...
Yaani Unavyoongea ni Kama Hujawahi soma Chuoni....vyuo vyetu hivi vya hapa bongo
Au ni kama unasema ni kama vile wewe ni mdingi unafanya Kazi UN uko bussy huelewi Kinachoendelea ktk familia Maadam wanakula!
Hata kama Mabaraza ya Chuo sijui,Sijui kukata rufaa,Hao Wanaofanikiwaga ni wachache sana,
Kwanini umpe Mtu mamlaka Maisha ya Mtu?
Halafu unasema eti ooh kuna Mabaraza,Sijui kuna nini sijui,
Ndio maana Form six safi sanaa hakuna Kujuana!
Unajua Sawa tume copy mfumo wa Elimu ya Juu toka Ulaya(Western)
Sio Kila Kitu cha Kukopy, wenzatu tamaduni zao ni ngumu hata tuu kumsogelea mwanafunzi,Kiufupi wenzetu wana maadili mnooo!
Sisi hakuna Uadilifu!
Mtu anakuambia eti mwl asiemwadilifu aripotiwe au Kuna Kamati,Sijui baraza
Ujinga tuu huo!
Mpaka wazungu wakibadilisha mfumo ndio na sisi tuta copy labda!
Jamaa yangu wa chuo flani alikuwaga anawatafuna sanaa Wanafunzi na Ana Maadili mnooo!Huwezi mdhania!na Yupo kwenye baraza pia!
 
Back
Top Bottom