Waziri Mkuu Kassim Majaliwa azindua kikao cha Baraza la Taifa la Kudhibiti Dawa za Kulevya

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa azindua kikao cha Baraza la Taifa la Kudhibiti Dawa za Kulevya.

Sheria ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya isimamiwe kikamilifu.Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa atakayepokea rushwa kutoka kwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.

Mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni vita kubwa inayotakiwa kupiganwa kwa nguvu kubwa.
 
Ha ha ha.. Baraza ambalo alikuwa hajijui kama yeye ndo mwenyekiti wake.. Kila la kheri kwao kwenye mapambano haya ya kutokomeza madawa ya kulevya..
 
Baraza ambalo lipo kwa miaka kadhaa sasa lakini walikuwa hawafahamu uwepo wake!! Na utamu zaidi, sheria iliyounda hili baraza inataka kuwe na angalau vikao viwili kwa mwaka ( regular session) na pamoja na hivyo (angalau) vikao 2 kwa mwaka; bado panaweza kuitishwa vikao vingine kadri itakavyoonekana inafaa!!!

Hatimae tukaja kujuzwa indirectly kwamba kumbe tangu serikali iiingie madarakani; members chini ya PM walikuwa hawajakaa hata kikao kimoja!!!

Kwamba, Baraza lenye wajumbe ambao ni mawaziri 10+ ukiacha PM; wote hawa walikuwa hawafahamu juu ya baraza hili!!!
 
Eti kila la kheri kwao! Inamaana we hii vita we haikuhusu? Machadema bana!

Inanihusu kivipi mie..? Kwenye baraza hilo sipo, kwenye orodha aliotaja makonda sipo, halikadhalika kwenye listi mpya aliekabidhiwa Mwenyekiti mie sipo vile vile.. Halafu mie sio askari polisi wala mwanajeshi.. Hata mgambo sijawahi kupitia ntahusikaje hapo..? Mbaya kabisa wimbo huo nimeanza kuusikia karibia miaka 30 iliyopita lakini kila siku inakuwa afadhali ya jana.. Haya niambie wewe wa ccm mie nahusika vipi hapo..?
 
Hujitambui
 
Just one Question, wakati wa kampeni was this the first priority? Sheria ipo, tume ipo then why all these hustle?. Take the chil pill and concentrate uchumi wa viwanda vya mfukoni.
 
Back
Top Bottom