Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awataka Mawaziri kusitisha ziara za ukaguzi wa miradi ili kupambana na Corona

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka mawaziri kusitisha ziara zao za ukaguzi wa miradi ya maendeleo mbalimbali na badala yake majukumu hayo yaelekezwe kwa Wakurugenzi ikibidi kwa Makatibu wakuu wa Wizara.

Waziri Mkuu amewata Mawaziri hao angalau kwa asilimia 75 ya ziara zao zielekezwe kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID-19

Mawaziri hakikisheni katika kipindi hiki ziara za kwenda kukagua miradi zielekezwe kwa wakurugenzi ikibidi kwa makatibu wakuu, mawaziri mnatakiwa mjikite katika kukinga Taifa na corona,” alisema Majaliwa.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati yupo kwenye Kikao na Mawaziri na Makatibu jijini Dodoma.
 
Agizo sahihi kwa wakati sahihi na linalopaswa kuendelezwa hata baada ya corona kwani sidhani kila ziara wanazofanya zina ulazima wa wao kuzifanya.
 
Mbona Mbona Ndugu makonda kaibukia stendi ya mabasi ,tena akiwa hajavaa hata vifaa vya kujilinda na Corona ,na kuanza kuwa tukana watu wengine,huku kawakusanya wanahabari uchwala wakimshangilia.
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka mawaziri kusitisha ziara zao za ukaguzi wa miradi ya maendeleo mbalimbali na badala yake majukumu hayo yaelekezwe kwa Wakurugenzi ikibidi kwa Makatibu wakuu wa Wizara.

Waziri Mkuu amewata Mawaziri hao angalau kwa asilimia 75 ya ziara zao zielekezwe kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID-19

Mawaziri hakikisheni katika kipindi hiki ziara za kwenda kukagua miradi zielekezwe kwa wakurugenzi ikibidi kwa makatibu wakuu, mawaziri mnatakiwa mjikite katika kukinga Taifa na corona,” alisema Majaliwa.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati yupo kwenye Kikao na Mawaziri na Makatibu jijini Dodoma.
Hizo sio ziara za kukagua miradi bali za kutafunia posho, miradi inakuwa na consultants wake ndio wasimamizi.
 
Back
Top Bottom