Waziri mkuu Kassim Majaliwa anakutana na watalii kutoka nchini China katika Hoteli ya mount meru. WACHINA HAWA NI WALEVI

Dripboy

JF-Expert Member
Mar 22, 2019
3,178
4,603
Kutoka hotel ya Mount meru watalii waliotua nchini kutoka nchini China wakipata chakula cha usiku huku Mgeni rasmi akitarajiwa kufika wakati wowote kuanzia hivi sasa.
Cha kushangaza hawa wachina ni walevi wanakunywa Kilimanjaro premium lager, Serengeti, Senator na vileo vingine vikali.
-----------------------------------------------------
Tunafahamu sote waziri mkuu ni muislamu kwa imani na yuko katika mfungo wa ramadhani hii imekaaje kiimani au ni sawa tu kushirikiana na walevi wenzetu hawa naona wamechangamka kwelikweli.
------------------------------------------------------
UPDATE:
22:17 Waziri mkuu Kassim Majaliwa anawasili.
22:23 Utambulisho umeanza
22:24 Jaji mihayo amekaribishwa kuzungumza
22:29 Waziri wa utalii Dkt Hamis kigwangala anakaribishwa.
22:35 Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa afrika ya mashariki Prof. Palamagamba Kabudi anazungumza.
▶Ameanza kujigamba kuwa aliitembelea china October
▶Watu wa china ni marafiki wetu wa jadi (All weather friends)
▶ 22:42 Prof palamagamba anawakaribisha sana ndugu zetu hawa kutoka China.
---------------------------------------------------------
22:49 Wachina wanatupa Burudani weeeee acha niserebuke zangu hapa.
22:54 Waziri mkuu anakaribishwa kuzungumza na Hadhira.
▶Anaanza kwa kuwatambua Viongozi mbalimbali waliopo Ukumbini
▶ Anawakaribisha kwenye Ardhi ya Kilimanjaro, Serengeti na Zanzibar.
▶Wanapewa ahadi ya kushuhudia Ukarimu wa watanzania, Tanzania ni nchi yenye vivutio vya asili sio vya kuandaliwa.
▶Kivutio chao cha kwanza kukitembelea itakuwa Ngorongoro Crater na baadaye mlima Kilimanjaro, MLIMA KILIMANJARO UPO TANZANIA TU, UKITAKA KUUZUNGUKA, KUUONA, NA KUUPANDA LAZIMA UJE TANZANIA.
⏩22:59Ni zamu ya kuinadi Serengeti sasa.
Waziri mkuu anamalizia hituba yake kwa kusisitiza kuendelea kwa mahusiano mazuri kati ya Tanzania na China.
Mwisho kabisa anahitimisha kwa kuwakaribisha Tanzania na "Nchi" ya Zanzibar.
Anamaliza kwa kusema "xièxie” yani Ahsante.
 
Kutoka hotel ya Mount meru watalii waliotua nchini kutoka nchini China wakipata chakula cha usiku huku Mgeni rasmi akitarajiwa kufika wakati wowote kuanzia hivi sasa.

Cha kushangaza hawa wachina ni walevi wanakunywa Kilimanjaro premium lager, Serengeti, Senator na vileo vingine vikali.

-----------------------------------------------------
Tunafahamu sote waziri mkuu ni muislamu kwa imani na yuko katika mfungo wa ramadhani hii imekaaje kiimani au ni sawa tu kushirikiana na walevi wenzetu hawa naona wamechangamka kwelikweli
Watalii wa kizungu wapo Zanzibar mida hii wanakata kilevi kama kawaida. Nenda ukawafukuze.
 
Utalii unahusu matumizi ya fedha kwenye bidhaa mbalimbali ikiwem pombe!! Sasa mnataka watalii halafu hamtaki wafurahie utalii wenu kisa nyie mnashinda njaa
 
Utalii unahusu matumizi ya fedha kwenye bidhaa mbalimbali ikiwem pombe!! Sasa mnataka watalii halafu hamtaki wafurahie utalii wenu kisa nyie mnashinda njaa
😝😝😝 Sisi wazee wa laga hatuna shida mkuu shida ipo kwa wenye imani yao
 
Walevi
Kivipi? Mgeni alikija kwako akataka kununua ulivo navyo utamwita mlafi?? Wanaongeza pato la tAifa acha kuwaita walevi
Imani ya wenzetu mkuu kipindi hiki hairuhusu mambo ya ulaji haya
 
kuna muislamu aina mbili . aina ya kwanza ni mwislamu ambaye yeye katoa shahadu kuwa mwislam lakini yupo tu pombe kwake kawaida kusali hasali wanawake.chochote kibaya yeye yupo tu : aina ya pili ni yule muislamu aliye shahadia na kufuata nguzo za kiislamu 5 na nguzo za imani 6 huyo anaitwa muislam muumin: sasa waziri mkuu au kigwangala ndio kwenye kundi la 1 . wao sio waislamu muumin. maana sheria ya dini ukikaa na mtu anayekunywa pombe hata kama wewe hunywi mungu anakuhesabu na wewe umeshiriki sasa vipi hawa ndugu zetu wapo kwenye pombe na huu mwezi mtukufu pamoja na watalii . mungu kawapa mtihani je unanipenda mimi au unaipenda kazi yako na dunia
 
Ni kiongozi wa Taifa, inabidi ashushie kidogo na Smirnoff Black ice waziri mkuu wetu kafanya kazi kubwa sana kuanzia siku ya msiba wa mengi hadi leo karoho kawe kwatu
 
Back
Top Bottom