Waziri Mkuu kadanganywa juu ya athari za kuanzisha shamba la Miwa la Bagamoyo

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
3,742
6,433
Ndugu wanajamvi,, binafsi nimesikitishwa sana na maamuzi ya Serikali ya Kukataa kuendeleza shamba la Miwa la Bagamoyo (ECOENERGY) ambalo lingezalisha tani 120,000 za Sukari kwa Mwaka na hivyo kuongeza ajira lakini kuipunguzia serikali manyanyaso ya upungufu wa Sukari nchini.

Wakati akijibu swali la hapo kwa hapo jana-19/05/2016, Mh Waziri mkuu aliulizwa ni kwanini Serikali imeshindwa kuendeleza shamba la Miwa la Bagamoyo. Yeye alijibu kuwa alishauriwa na kamati ya Bunge kuwa shamba lile likilimwa miwa basi maji kwa ajili ya wanyama wa SAADANI yatakauka. HII SI KWELI, NA MH WAZIRI MKUU KADANGANYWA KAMA VIONGOZI WA SERIKALI ILIYOPITA WALIVYODANGANYWA NA MWISHO WAKE TUMEISHIA KUNYANYASIKA JUU YA SUALA ZIMA LA SUKARI.

Kwanini kunajitihada za kupinga mradi huu wa Sukari wa shamba la Bagamoyo (ECOENERGY)

1. Wafanya biashara waliokuwa wanaagiza sukari nje watapoteza biashara. Hivyo wanatumia mbinu tofauti kukwamisha miradi mikubwa ya sukari kuanza hapa nchini.Ndo maana hakuna shamba jipya limeanzishwa Tanzania tofauti na yale yaliyoachwa enzi za Nyerere.

2. Makampuni yanaliyolima Miwa hayataki kampuni mpya kuanzisha mashamba mapya kwani wanahofia makampuni mapya kama Ecoenergy yataleta ushindani wa bei na Ubora wa Sukari nchini .
3. Nchi ambazo zinauza sukari Tanzania hazitaki kupoteza soko, hivyo zimekuwa zikitumia ushawishi kupitia mashirika kama Action Aid na kamati za Bunge kukwamisha Jitihada za Tanzania kuzalisha Sukari ya Kutosha.
4.Mradi wa Ecoenergy ni wa Ubia Kati ya Serikali na Waswiss. Kwa Serikali kuwa mbia, ingejua gharama halisi za Uzalishaji hivyo kujua bei halisi ya kumuuzia Mtanzania. Kampuni zilizopo na zinazofanya biashara ya Sukari hazitaki hilo litokee kwani watalazimika kushusha bei ili kuendena na matakwa ya Serikali juu ya bei halisi.

Lakini tujiulize, je kweli mradi huo utakausha maji ya Mto WAMI?? JIBU NI Uongo wa Kutunga kwa ajili ya kufanya Tanzania iendelee kuwa tegemeji wa Sukari.

Kama hoja hiyo inamashiko ni kwanini Shamba la Mtibwa limeachawa kuendelea kutumia maji ya Mto WAMI? Hoja hapa nikukwamisha Miradi Mipya ya Miwa Tanzania. mradi husika hauna athari zozote za kimazingira kama Mh Waziri Mkuu alivyodanganywa kwa sababu zifuatazo;

1.Shamba hilo la ECOENERGY linapakana na Bahari hivyo maji yatakayotumika ni yale maji ya mto WAMI yanayoenda kumwagikia baharini baada ya Matumizi ya nchi kavu. Maana yake ni Maji ya ziada ndo yatatumika kwa ajili ya kilimo cha miwa kwenye shamba la Bagamoyo.
2. Wakati wa Masika, Mto Wami hufurika na kumwaga maji ndani ya Shamba la Ecoenergy.Wakati tunafanya tathminin, tulingundua kuwa Kampuni itachimba Bwawa kubwa kwa ajili ya kutega maji haya ya ziada ili wayatumie kumwagilia Miwa.Na katika kilimo hiki cha miwa technologia watakayotumia ni ile ya DRIP IRRIGATION.Hivyo si kweli kwamba miwa itakausha maji ya mto WAMI

Kutokana na maelezo yangu juu, nashawishika kusema kuwa Mh Waziri mkuu kadanganyika sana juu ya suala la shamba la Miwa la Bagamoyo. Anacheza ngoma asiyoijua. Ni vizuri atumie mda mrefu kufanya utafiti.

Natoa wito pia kwa waandishi waliobobea wajaribu kufanya utafiti wa kina juu ya Suala la Serikali kukwamisha uanzishwaji wa shamba la Miwa la Bagamoyo ambalo lingezalisha Tani 120,000 Kwa mwaka.

Naomba adm muistick hii hoja ili watu waijadili kwani inaweza kusaidia taifa letu katika maamuzi.

Asanteni sana
 
utauwa mashamba ya mkapa.

swissme

SERIKALI IKIENDEKEZA MAMBO YA KUSIKILIZA WATU WALEWALE WALIOFANYA NCHI HII ISHINDWE KUZALISHA SUKARI YA KUTOSHA BASI TUSITARAJIE MABADILIKO.

SHAMBA hili la Bagamoyo lilitaka kuwekeza dolla 500 million. Na ili kiwanda kiweze kuwatendea haki wakulima (outgrowers), kiwanda amabcho kingejengwa kingetemea kupata miwa 50% kutoka kwa wakulima hivyo kutengeneza soko la miwa ya wakulima kwa uhakika. Sasa makampuni yalioyopo yanaopgopa hii kutokea kwani kama wakulima wakianza kuzalisha na kufaidika kuliko wa kulima wa kilombero na Mtibwa ina maana kampuni za kilombero na Mtibwa ziatatakiwa kufanya kama kiwanda cha ECOenergy kinavyofanya.HILI HAWALITAKI LIKTOKEE
 
Huu mradi umepigwa sana vita, shida mpk ss sijajua ni kitu gani, nilipata kuhudhuria mkutano mmoja wa hawa jamaa, wakaeleza kile ambacho wananchi wa Bagamoyo wangefaidika nacho, kuanzia umeme wa uhakika mpk ajira, hawa jamaa ilikuwa watoe mafunzo ya kilimo cha mboga mboga na matunda kwa wananchi wa bagamoyo ili waweze kuzalisha vyema na kuwauzia wafanyakazi hapo Kiwandani (kama kingeanzishwa)
Tatizo lilianzia kwa wanasiasa......kwanini bagamoyo, wakaja na hoja kuwa wazungu wanawapoka wananchi mashamba yao na hizi fitina nikasikia zinasimiwa na ACTIONAID........nashukuru kwenye huo mkutano nilijifunza mengi pamoja na kula msosi mzuri.
Ss hili bandiko hapa leo linanifanya nishtuke maana juzi tu nilikutana na mwandishi mmoja ambaye tulikuwa naye kwenye huo mkutano, tuliongea mengi mojawapo ni kuniambia kuwa ECOENERGY wameshinda kesi yao na huo mradi unaanza, ss hichi ninachosoma hapa tena kinanishangaza, mleta mada hembu tuambie vizuri, huo mradi upo au ndio Waziri Mkuu kadanganywa na ishu ndio imekufa?
 
HII MRADI KUWEPO AU KUTOKUWEPO ITATEGEMEA NA SERIKALI INAAMUA NINI?? WATU HAWAJIULIZI NIKWANINI MIAKA 15 ILIYOPITA SISI NA MSUMBIJI,MALAWI NA LESOTHO TULIKUWA NATATIZO YA SUKARI. LAKINI SASAHIVI TUNAPAMBANA KUZUIA SUKARI KUTOKA MALAWI. JIBU NI KWAMBA BAADHI YA WATANZANIA WENZETU WALIOKO SERIKALINI WANATAMUA KALAMU ZAO KUJINUFAISHA NA HIVYO KUWEKA VIKWAZO KWA MIRADI MIKUBWA AMABAYO INGELITOA TAIFA KWENYE MATATIZO YA SUKARI NA KUONGEZA UIGO WA KODI.

WATANZANIA HATUFANYI UTAFITI WA KINA NA BAHATI MBAYA NAONA NA VIONGOZI WETU WANAWASIKILIZA WATU WALEWALE WALIOTUFANYA TUSIENDELEE
 
Waziri mkuu yuko sahihi kabisa. Watafute sehemu nyingine wakawekeze mbona Tanzania ina maeneo mengi ya kuwekeza katika Sugar Industry.

Unasema Mh Waziri mkuu yuko sahihi kwa lipi? mbona hatutumii elimu zetu kuondoa vikwazo ili tuendelee?? Jiulize pia kama sehemu zingine ni Rahisi kwanini hadi hivi sasa hakuna kiwanda hata kimoja cha sukari kimejengwa tofauti na vile vilivyoachwa na Mwl. Nyerere??
 
Waziri mkuu yuko sahihi kabisa. Watafute sehemu nyingine wakawekeze mbona Tanzania ina maeneo mengi ya kuwekeza katika Sugar Industry.
Sehemu nyingine ni ipi? Unajua kuwa muwekezaji ukimbabaisha anaenda kuwekeza nchi nyingine!?

Suala la sekta ya sukari kuhujumiwa na wafanyabiashara liko miaka nenda miaka rudi. Mfano ni jinsi wakulima wa miwa walivyonyanyaswa na muwekezaji wa shamba la mtibwa bila serikali kutoa msaada wowote. Wakulima wameacha kulima miwa wako na mpunga kwa sasa. Bodi ya sukari ni jipu kubwa katika kuendeleza zao. Huwezi kuja na kisingizio cha maji yatashindwa kwenda mbugani wakati kuna mautaalam kibao ya kuvuna maji na ukamwagilia hata miaka miwili. Hii nchi imefikishwa hapa ilipo na hawa hawa tunaodhani wakombozi leo
 
SERIKALI IKIENDEKEZA MAMBO YA KUSIKILIZA WATU WALEWALE WALIOFANYA NCHI HII ISHINDWE KUZALISHA SUKARI YA KUTOSHA BASI TUSITARAJIE MABADILIKO.

SHAMBA hili la Bagamoyo lilitaka kuwekeza dolla 500 million. Na ili kiwanda kiweze kuwatendea haki wakulima (outgrowers), kiwanda amabcho kingejengwa kingetemea kupata miwa 50% kutoka kwa wakulima hivyo kutengeneza soko la miwa ya wakulima kwa uhakika. Sasa makampuni yalioyopo yanaopgopa hii kutokea kwani kama wakulima wakianza kuzalisha na kufaidika kuliko wa kulima wa kilombero na Mtibwa ina maana kampuni za kilombero na Mtibwa ziatatakiwa kufanya kama kiwanda cha ECOenergy kinavyofanya.HILI HAWALITAKI LIKTOKEE
jamaa alikimbia Ikulu kuweka mambo sawa na ndie aliyeimkapenia jamaa kwenda Ikulu na kuwaita Watanzania WAPUMBAVU. usitegemee hapo.jamaa yuko 80%

swissme
 
Nashangaa pamoja na shida hii ya sukari hakuna hata mwandishi wa habari za uchunguzi hata mmoja aliyefanya investigative journalism kugundua madudu mengi na nia mbaya zilizopo miongoni mwa wazalisha sukari. In fact Magufuli alipowaambia watu wa hifadhi za jamii kuwekeza kwenye viwanda huku kwenye sukari wangepiga sana bao. Lakini utashangaa na viwanda watakavyopendekeza.

Nawapa changamoto watu wa habari wafikieni wakulima wa miwa aka Outgrowers mkayajue madhira yao nyuma ya pazia
 
Huu mradi umepigwa sana vita, shida mpk ss sijajua ni kitu gani, nilipata kuhudhuria mkutano mmoja wa hawa jamaa, wakaeleza kile ambacho wananchi wa Bagamoyo wangefaidika nacho, kuanzia umeme wa uhakika mpk ajira, hawa jamaa ilikuwa watoe mafunzo ya kilimo cha mboga mboga na matunda kwa wananchi wa bagamoyo ili waweze kuzalisha vyema na kuwauzia wafanyakazi hapo Kiwandani (kama kingeanzishwa)
Tatizo lilianzia kwa wanasiasa......kwanini bagamoyo, wakaja na hoja kuwa wazungu wanawapoka wananchi mashamba yao na hizi fitina nikasikia zinasimiwa na ACTIONAID........nashukuru kwenye huo mkutano nilijifunza mengi pamoja na kula msosi mzuri.
Ss hili bandiko hapa leo linanifanya nishtuke maana juzi tu nilikutana na mwandishi mmoja ambaye tulikuwa naye kwenye huo mkutano, tuliongea mengi mojawapo ni kuniambia kuwa ECOENERGY wameshinda kesi yao na huo mradi unaanza, ss hichi ninachosoma hapa tena kinanishangaza, mleta mada hembu tuambie vizuri, huo mradi upo au ndio Waziri Mkuu kadanganywa na ishu ndio imekufa?
Tanzania ni nchi yenye bahati sana yaani mwekezaji had anaenda kushitaki ili aweze kuwekeza..!?
Kwanini wasimpe tu hilo shamba nililiona kwenye TV tu.
 
Kuna haja baona ya ky adilisha au kuleta njia mbadala ya miwa. Kutumia sugar bets. Naona hiyo ingefamyiwa majaribio ta kupanda hapo tanza. Nchi kama Sweden ndii wanatumia sugar bets kuzalishia sukari
 
Kuna haja baona ya ky adilisha au kuleta njia mbadala ya miwa. Kutumia sugar bets. Naona hiyo ingefamyiwa majaribio ta kupanda hapo tanza. Nchi kama Sweden ndii wanatumia sugar bets kuzalishia sukari

TATIZO TANZANIA TUNARIDHIKA NA VITU VIDOGOVIDOGO SANA.HATUFIKILII KWA UPANA.MAWAZO KAMA HILI LAKO YANAWEZA KUJENGA NCHI.UKWELI NIKWAMBA SERIKALI LAZIMA IAMUE KUSAPORT KWA NGUVU MASUALA YA UWEKEZAJI BILA KUSIKILIZA WAZILISHA FITINA.
 
Nashangaa pamoja na shida hii ya sukari hakuna hata mwandishi wa habari za uchunguzi hata mmoja aliyefanya investigative journalism kugundua madudu mengi na nia mbaya zilizopo miongoni mwa wazalisha sukari. In fact Magufuli alipowaambia watu wa hifadhi za jamii kuwekeza kwenye viwanda huku kwenye sukari wangepiga sana bao. Lakini utashangaa na viwanda watakavyopendekeza.

Nawapa changamoto watu wa habari wafikieni wakulima wa miwa aka Outgrowers mkayajue madhira yao nyuma ya pazia

kubw ani ile sheria ya uhuruhisiwi kuanzisha hata kiwanda kidogo cha sukari karibu na viwanda vilivyopo.
 
Kimla, huo mradi wa Ecoenergy ni ubia na Waswisi au Waswidi? Nadhani ni Waswidi (Sweden).

Jana kwenye Channel Ten waliweka kipindi maalum cha sakata la sukari, Ndugu Mkinga, kama kawaida yake, alifunguka na kufungua macho na masikio ya wengi.

Pia TBC walikuwa wanazungumzia suala hilo hilo (kwa muda huo huo), na wazungumzaji walieleza kwa ufasaha changamoto na figisu figisu kwenye sekta hiyo.

Mods kama mnaweza muweke hapo clips za vipindi hivyo viwili ili kuchochea mjadala juu ya kadhia hii ya sukari hapa nchini.
 
Back
Top Bottom