Waziri Mkuu awaonya DC na DED 'wanaorogana'

Waziri Mkuu awaonya DC na DED 'wanaorogana'

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Mkuu wa wilaya ya Biharamulo, Sada Malunde na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Wende Ng'ahara wamalize tofauti zao na wasipojirekebisha atamshauri Rais Dkt. John Magufuli kufanya maamuzi mengine.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu ametoa kalipio hilo leo Jumatano, Februari 20, 2019 wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira wa shule ya msingi Nyakanazi, kijiji cha Nyakanazi, Biharamuko mkoani Kagera.

Amesema kutokuelewana kwa viongozi hao ambao wakati mwingine wanatuhumiana kufanyiana vitendo vya kishirikina kumesababisha kuzorota kwa shughuli za maendeleo katika wilaya,

"mliletwa hapa kuiwakilisha Serikali na kusimamia maendeleo ya wananchi nyie mnagombana." amesema Waziri Mkuu

Aidha Waziri Mkuu amesema, "sijaridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara, mkandarasi na mhandisi mshauri wote wanaonekana hawapo makini katika kufanya kazi hii."


- EATV
 
Bora hawaamishe tu, kila mtu apelekwe pande yake.
 
Eti waziri mkuu ana uwezo wakumsimamisha kazi mkurugenzi mpaka amuombe raisi hii ni hatari kwa kweli. Nafikili wakurugenzi wasingekuwa wanateuliwa na raisi ingesaidia.
 
Mkuu chilonge,kwa hiyo nani aliwahamisha toka kwa pm kwenda ofisi ya prezidar
 
Back
Top Bottom