Waziri Mkuu awaonya DC na DED 'wanaorogana'

Waziri Mkuu awaonya DC na DED 'wanaorogana'

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Mkuu wa wilaya ya Biharamulo, Sada Malunde na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Wende Ng'ahara wamalize tofauti zao na wasipojirekebisha atamshauri Rais Dkt. John Magufuli kufanya maamuzi mengine.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu ametoa kalipio hilo leo Jumatano, Februari 20, 2019 wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira wa shule ya msingi Nyakanazi, kijiji cha Nyakanazi, Biharamuko mkoani Kagera.

Amesema kutokuelewana kwa viongozi hao ambao wakati mwingine wanatuhumiana kufanyiana vitendo vya kishirikina kumesababisha kuzorota kwa shughuli za maendeleo katika wilaya,

"mliletwa hapa kuiwakilisha Serikali na kusimamia maendeleo ya wananchi nyie mnagombana." amesema Waziri Mkuu

Aidha Waziri Mkuu amesema, "sijaridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara, mkandarasi na mhandisi mshauri wote wanaonekana hawapo makini katika kufanya kazi hii."

- EATV
Ningekuwa rais ningeshapitisha panga katikati yao.
 
CCM na uchawi, wizi, ujambazi, uasherati, nk. ni sawa na samaki na maji.
 
Hao Makada wa chama ndo wanaonyofoa na kùua watoto na wanawake
 
Mkuu chilonge,kwa hiyo nani aliwahamisha toka kwa pm kwenda ofisi ya prezidar
Ni mabadiliko ya awamu ya 5 ndio yamepelekea TAMISEMI kuwa chini ya OR.
Naamini ilikuwa ni kwaajili ya uangalizi wa karibu wa Mh. Rais ili kuleta matokeo chanya kiutendaji.
 
Hakuna kupatana hapo, suluhisho ya hao ni kuwaondoa kuwahamisha au kuwaondoa madarakani,kiukweli sehemu za kazi kuna watu wapo kwa ajili ya kuwajera wenzao tu.
 
Kwani waziri mkuu hawezi kufanya maamuzi mengine?
DC na DED ni wateule wa Rais,WM hawezi ingilia teuzi za Mkulu,isipokua anatoa ushauri tu... Zamani DED walikua wanateuliwa na WM, ndiyo maana kina Pinda au Lowasa walikua wanafanya maamuzi.... Pia TAMISENI ilikua chini ya ofisi ya WM

Kaja mjuaji kapora ofisi kapeleka kwake,hivi unadhani kama TAMISENI ingekua chini ya WM, RC Makonda asingekua RC hadi sasa hivi... Kumbuka sakata la Shisha Dsm,WM alimwambia nini Makonda....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni wanawake wote hata DAS naye kumbe ni Agnes Alex mwanamke mwingine, kweli nyoka pale bustani ya Eden alileta tafrani.
What to Do?
1. Semina baada ya uteuzi hasa kujua mipaka ya kazi na mamlaka mfano hapa mmoja akikosea na akakosolewa na mwingine anaanzisha bifu. Na ikibidi uteuzi uwe unafuata weledi kama ni mkurugenzi lazima awe na elimu stahiki na uzoefu wa utumishi wa umma kuliko mkuu wa wilaya.
2. Viongozi wa kitaifa nao waache kuwakosoa hadharani viongozi wa wilaya mbele ya wananch wanaowaongoza, inawapunguzia hadhi na ari ya kuongoza siku za usoni.
3. Wakuu wa idara wana mchango mkubwa wa kushauri na kujenga mazingira rafiki ya wakuu wao kufanya kazi kwa pamoja, lakini kwa kuwa wanaishia kwenye kushauri tu, wasiposikilizwa wanaweza kuwa ni Early Warning elements nzuri zaidi kwa mamlaka za uteuzi, kabla mambo hayajawa makubwa maana anayeathirika ni mwananchi.
 
Sielewi viongozi hawa wanatupeleka wapi. JPM tumbua tu
 
Back
Top Bottom