Waziri Mkuu atolewa nje bungeni New Zealand

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,369
8,072
Ni kawaida kwenye Mabunge mbalimbali duniani kuona Wabunge wametolewa nje au wenyewe wametoka nje lakini ni nadra sana kusikia Waziri mkuu kazingua bungeni na kusababisha Spika kuamuru atoke nje.

Imetoka huko New Zealand ambapo waziri mkuu mpya John Key ametolewa bungeni baada ya kukaidi kufata kanuni za bunge hilo ambalo limekua na mjadala mkali kuhusu ishu ya akaunti za siri ambazo zinadaiwa kuwepo kwenye kisiwa cha Panama.

Spika wa Bunge David Carter ametetea maamuzi yake na kusema waziri mkuu alikaidi onyo la kuheshimu kanuni za bunge na hivyo hakua na kinga ila kumuadhibu kama anavyofanya kwa Wabunge wengine.

BBC wameripoti kwamba rekodi za bunge zinaonyesha Waziri Mkuu huyu aliwahi kutolewa bungeni mara tatu wakati akiwa mbunge lakini pia hii sio mara ya kwanza kwa Waziri mkuu wa NewZealand kutolewa bungeni, Waziri mkuu wa zamani Helen Clark alitolewa mwaka 2005 vilevile David Lange kwenye miaka ya 1986 na 1987.

my take: kwa hapa nyumbani ndugai anaweza?!
 
Yah Kama akileta ubabe kama huu unaondelea nje ya bunge atatolewa tu... Sheria kwanza na hamna aliyejuu ya Sheria.... alisema Ankal Magu lakini yanayoendelea ni zaidi ya uvunjaji wa Haki za Binadamu... yaani Mtu unavamiwa tu na Jamaa wa Siasa hata hawafuati utaratibu wao wanakamata tena kwa vyombo vya habari wanajipaisha live siku moja baadae vyombo husika hustushwa na kuwasafisha waliokamatwa na Wanasiasa.... hapa nadhani kuna kitu au vitu havikuenda sawa kwenye uchaguzi... haiwezekani huu utaaratibu wa kufanya kazi hivi ni hatari na tuliambiwa na pinda mafisadi wakiguswa nchi itayumba... ndio tunayoyaona sasa hivi... Pinda haendelei kutoa Ushauri kwa Ankal Magu.... Tutapelekeshwa hadi tukome
 
Ndugai atatoka yeye. Badala ya bunge kulisimamia serikali, ni kinyume chake
 
Back
Top Bottom