Waziri Mkuu asema viwanda 4,000 vimejengwa tangu Serikali ya awamu ya 5 iingie madarakani

Nadhani tungekuwa na kiwanda kimoja au viwili tungekuwa mbali sana. Tungeomba TOYOTA au VW waje kuitengeneza magari hapa, au japo kuhamishia nusu ya viwanda vyao tungekuwa mbali sana.... inawezekana kuna mgongano wa tafsiri ya hili neno kiwanda. Kwa tafsiri ya jadi, kiwanda kimoja sio rahisi kuwa nacho kwa mwaka mmoja kwa nchi yenye uchumi kama Tanzania.

Mkuu hili la kuweka viwanda vyao kwetu nafikiri huwa wanafanya uchunguzi mkubwa sana na mpaka wajiridhishe na hao mabalozi wanachunguza vitu vingi sana
 
Tuzo hizo ambazo zimeandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) ilishirikisha makampuni 61 ambapo mshindi wa jumla ilikuwa ni kampuni ya Hanspaul iliyoko mkoani Arusha

Tuwe na tuzo za viwanda pia badala ya kua na Tuzo za makampuni pekee...

Cc: mahondaw
 
Aveline Kitomary, Dar es salaam

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, viwanda vipya zaidi ya 4,000 vimejengwa na hivyo kufanya sekta hiyo kuchangia Pato la Taifa kwa asilimia 8.05 na kutoa ajira 306,180 mwaka 2018.

Akizungumza kwa niaba ya Rais John Magufuli jana Dar es Salaam, wakati wa utoaji wa tuzo za Rais kwa wazalishaji bora wa viwandani (PMAYA) mwaka 2018 alisema kutokana na sekta hiyo kuwa na mchango mkubwa, Serikali itavipa kipaumbele viwanda vinavyotumia malighafi za ndani zaidi.

Tuzo hizo ambazo zimeandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) ilishirikisha makampuni 61 ambapo mshindi wa jumla ilikuwa ni kampuni ya Hanspaul iliyoko mkoani Arusha.

“Sekta ya viwanda imeendelea kuongeza pato la taifa na mwaka 2018 imeongezeka kwa asilimia 8.05 tofauti na mwaka 2017 ambao ilikuwa asilimia 7.67, Aidha, katika kipindi cha mwaka 2018 Sekta ya viwanda ilichangia asilimia 18.1 ya mauzo yote ya nje, ikilinganishwa na asilimia 15 mwaka 2017 pia, takwimu zinaonyesha kwamba katika mwaka 2018 Sekta ya viwanda imetoa ajira rasmi 306,180 ikilinganishwa na ajira 280,899 mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia 9.

“Mkakati wetu wa kuendeleza viwanda nchini kipaumbele kimewekwa katika viwanda ambavyo vinatumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini, tunahitaji kupunguza uuzaji wa mazao yetu ya kilimo, misitu, madini na maliasili nje ya nchi yetu yakiwa ghafi, hali kadhalika tunalenga kutumia rasilimali zilizopo nchini kuzalisha bidhaa ambazo hivi sasa tunaziagiza kutoka nje.

“Shabaha yetu ni kutosheleza mahitaji ya ndani ya bidhaa za viwandani, na kuwa na ziada tutakayouza nje ya nchi ili kupata fedha za kigeni, kukuza ajira na kuongeza kipato cha Watanzania kwa ujumla,yote haya yatawezekana kama tutatengeneza miundombinu kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa bora,”alisema Majaliwa.

Alisema ili kufikia lengo la kuwa nchi ya kipato cha kati inayoongozwa na uchumi wa viwanda Serikali haina budi kuhahakikisha ukuaji wa uchumi unafikia asilimia 12 kwa mwaka.

“Ikiwa ni mchango wa viwanda katika Pato la Taifa usiopungua asilimia 15,utoaji wa ajira rasmi na za moja kwa moja uongezeke na kufikia asilimia 40 ya ajira zote; na,pia ni muhimu sekta ya viwanda iweze kuiingizia nchi mapato ya fedha za kigeni zaidi ya asilimia 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni,”alieleza.

Aidha alisema kuwa serikali inaendelea kutatua changamoto zinazoikumba na kurudisha sekta ya viwanda nchini kwa kushirikiana na sekta ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya kufanya biashara.

Aidha Waziri Majaliwa alimpongeza Subhash Patel kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa CTI pamoja na wadhamini waliojitokeza kudhamini tuzo hizo.

“Kuchaguliwa kwako ni ishara tosha kwamba Wanachama wa CTI wanakupenda na wanatambua mchango wako mkubwa katika sekta ya viwanda pamoja na uwezo na uzoefu wako wa muda mrefu wa kusimamia masuala ya viwanda nchini,” alisema.

Kwa upande wake mshindi wa jumla wa tuzo hiyo Satbir Singh alitoa ushauri hasa kwa vijana ambao wanamalengo ya kuanzisha viwanda wawe na uthubutu.

“Kila kitu ni uthubutu na kutokukata tamaa ni muhimu kila mtu apambane kuhakikisha anafanikisha ndoto zake au malengo yake kwahiyo nawaambia hasa vijana wasikate tamaa katika wakati mgumu wa biashara wanaopitia kila kitu ni uvumilivu na uthubutu,”alisema Singh
Majaliwa ni kati ya watu nisiowaamini kabisa. Yeye anapenda sana kuongea kwenye macamera kudhalilisha watumishi wa Umma wadogo wadogo ili wamuone kuwa yuko Babu kubwa.

Ilitosha tu aseme tuna sera ya kujenga uchumi wa viwanda, tungemuelewa. Sasa unaongelea viwanda 4,000 wakati hata kwenye soko hatuoni bidhaa zenyewe.

Kwa mfano ndugu msomaji Ingia duka la Mchagga au Mpemba hapo jirani yako nenda kahesabu bidhaa zilizozalishwa Tanzania halafu jiulize haya anayoropoka PM Majaliwa.
 
Majaliwa ni kati ya watu nisiowaamini kabisa. Yeye anapenda sana kuongea kwenye macamera kudhalilisha watumishi wa Umma wadogo wadogo ili wamuone kuwa yuko Babu kubwa.

Ilitosha tu aseme tuna sera ya kujenga uchumi wa viwanda, tungemuelewa. Sasa unaongelea viwanda 4,000 wakati hata kwenye soko hatuoni bidhaa zenyewe.

Kwa mfano ndugu msomaji India duka la Mchagga au Mpemba hapo jirani yako nenda kahesabu bidhaa zilizozalishwa Tanzania halafu jiulize haya anayoropoka PM Majaliwa.
Kimsingi wote hawaaminiki. Yaani hizi propaganda ni kama za akina Paul Goebbels na Comical Ally. Viwanda 4000! Halafu una maelfu ya graduates wako barabarani,hawana ajira! Unamdanganya nani?
 
This guy must be crazy. He is playing with 4000 industries. The truth is that since the advent of this regime there are some industries that have been forced to wind up due to unfavorable conditions affecting investors in this country.
 
Aveline Kitomary, Dar es salaam

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, viwanda vipya zaidi ya 4,000 vimejengwa na hivyo kufanya sekta hiyo kuchangia Pato la Taifa kwa asilimia 8.05 na kutoa ajira 306,180 mwaka 2018.

Akizungumza kwa niaba ya Rais John Magufuli jana Dar es Salaam, wakati wa utoaji wa tuzo za Rais kwa wazalishaji bora wa viwandani (PMAYA) mwaka 2018 alisema kutokana na sekta hiyo kuwa na mchango mkubwa, Serikali itavipa kipaumbele viwanda vinavyotumia malighafi za ndani zaidi.

Tuzo hizo ambazo zimeandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) ilishirikisha makampuni 61 ambapo mshindi wa jumla ilikuwa ni kampuni ya Hanspaul iliyoko mkoani Arusha.

“Sekta ya viwanda imeendelea kuongeza pato la taifa na mwaka 2018 imeongezeka kwa asilimia 8.05 tofauti na mwaka 2017 ambao ilikuwa asilimia 7.67, Aidha, katika kipindi cha mwaka 2018 Sekta ya viwanda ilichangia asilimia 18.1 ya mauzo yote ya nje, ikilinganishwa na asilimia 15 mwaka 2017 pia, takwimu zinaonyesha kwamba katika mwaka 2018 Sekta ya viwanda imetoa ajira rasmi 306,180 ikilinganishwa na ajira 280,899 mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia 9.

“Mkakati wetu wa kuendeleza viwanda nchini kipaumbele kimewekwa katika viwanda ambavyo vinatumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini, tunahitaji kupunguza uuzaji wa mazao yetu ya kilimo, misitu, madini na maliasili nje ya nchi yetu yakiwa ghafi, hali kadhalika tunalenga kutumia rasilimali zilizopo nchini kuzalisha bidhaa ambazo hivi sasa tunaziagiza kutoka nje.

“Shabaha yetu ni kutosheleza mahitaji ya ndani ya bidhaa za viwandani, na kuwa na ziada tutakayouza nje ya nchi ili kupata fedha za kigeni, kukuza ajira na kuongeza kipato cha Watanzania kwa ujumla,yote haya yatawezekana kama tutatengeneza miundombinu kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa bora,”alisema Majaliwa.

Alisema ili kufikia lengo la kuwa nchi ya kipato cha kati inayoongozwa na uchumi wa viwanda Serikali haina budi kuhahakikisha ukuaji wa uchumi unafikia asilimia 12 kwa mwaka.

“Ikiwa ni mchango wa viwanda katika Pato la Taifa usiopungua asilimia 15,utoaji wa ajira rasmi na za moja kwa moja uongezeke na kufikia asilimia 40 ya ajira zote; na,pia ni muhimu sekta ya viwanda iweze kuiingizia nchi mapato ya fedha za kigeni zaidi ya asilimia 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni,”alieleza.

Aidha alisema kuwa serikali inaendelea kutatua changamoto zinazoikumba na kurudisha sekta ya viwanda nchini kwa kushirikiana na sekta ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya kufanya biashara.

Aidha Waziri Majaliwa alimpongeza Subhash Patel kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa CTI pamoja na wadhamini waliojitokeza kudhamini tuzo hizo.

“Kuchaguliwa kwako ni ishara tosha kwamba Wanachama wa CTI wanakupenda na wanatambua mchango wako mkubwa katika sekta ya viwanda pamoja na uwezo na uzoefu wako wa muda mrefu wa kusimamia masuala ya viwanda nchini,” alisema.

Kwa upande wake mshindi wa jumla wa tuzo hiyo Satbir Singh alitoa ushauri hasa kwa vijana ambao wanamalengo ya kuanzisha viwanda wawe na uthubutu.

“Kila kitu ni uthubutu na kutokukata tamaa ni muhimu kila mtu apambane kuhakikisha anafanikisha ndoto zake au malengo yake kwahiyo nawaambia hasa vijana wasikate tamaa katika wakati mgumu wa biashara wanaopitia kila kitu ni uvumilivu na uthubutu,”alisema Singh
huyu muislamu naye ameanza kuwa muongo?
Yani viwanda elf 4 means wma CEO 4000, WANASHERIA 4000, MAKARANI 4000, WALINZI 4000 MARA IDADI YA VIWANDA LEO HII TUNGEKUWA TUNAKODISHA WARWANDA WAJE KUFNYA KAZI TANZANIA.

WATUPE NA IDADI YA VIWANDA ALIVYO VIUA, NA MASHIRIKA KUANZIA MTANAO WA SIMU SMART, BILL CANAS, MASHAMBA YA MBOWE, MOUNT MERU MILLERS, RONDO TOURS, BUREAU DE CHANGE ZAIDI YA 500, MIRADI YA UJENZI NA MADUKA KARIAKOO KWA KURUHUSU WAMACHINGA KUPANGA BIASHARA BARABARANI TENA mzigo mkubwa kuliko maduka kwa ada ya Tshs 20000
 
Aiseee
Vipo vingi mkuu ngoja nianze na hivi vichache na kama tunavyojua kazi ya kiwanda izalishe bidhaa then iuzwe pesa ipatikane sasa hapa nakuletea viwanda vilivyozalisha pesa nyingi kwa ujanja na weledi wa hali ya juu wa awamu ya 5.

1.Viwanda vya kununua wapinzani(Madiwani na wabunge),hivi vilianzishwa kuanzia mwaka 2017 mpaka sasa vinaendelea.

2.Viwanda vya wahujumu uchumi(DPP bado anaendelea kukusanya mapato)

3.Viwanda vya utekaji(Mo alikamuliwa mabilioni)

4.Viwanda vya kubambika kodi(endelevu)

5.Viwanda vya 1.5 trilioni kilichoibuliwa na Polepole ooh sorry CAG

6.Kiwanda cha chatooo kule linalopaki Drimu la aina

7.Viwanda vya kuwapa watu kesi ya madawa ya kulevya kisha baadae wakatoa hela kesi zikaisha.

Nk viko ving vingine mtanisaidia
 
Uzuri ni kwamba akimaliza hotuba yake aliyoandikiwa hakuna wa kumuhoji
 
Mkuu Watanzania wengi mioyo yetu imejaa hasira na uchungu uliokithiri ila ukosefu wa elimu, uvumilivu na uoga uliokithiri ndo kina watia viburi hao viongozi wanaweza kesema chochote na kufanya lolote wanalojisikia sisi tupo tunakodoa na makofi ya unafki tunapiga.

Dah! Ila nyie watu! Watanzania huwa nawaona wa kimya, kumbe!
 
Kuhusu viwanda wala hautuwezzi kubisha. Inategemea tafsiri ya neno lenyewe na linatolewa na Nani kutoka awamu ipi. Awamu ya Kwanza hadi ya NNE kuna tafsiri yake, awamu ya TANO kamusi imebadilika.
 
Tuzo hizo ambazo zimeandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) ilishirikisha makampuni 61 ambapo mshindi wa jumla ilikuwa ni kampuni ya Hanspaul iliyoko mkoani Arusha

Tuwe na tuzo za viwanda pia badala ya kua na Tuzo za makampuni pekee...

Cc: mahondaw
Viwanda vinajengwa na nani hasa?Serikali,wawekezaji,watu binafsi,kampuni au nchi?Nini tafsiri ya neno kiwanda?
 
Hakika uongoz wa nchi hii unaharibiwa na taasisi ambazo vingoz wake wakubwa n mawazir
hiz taasis znaongoza kwa kupika taarfa za uongo
 
Back
Top Bottom