Waziri Mkuu asema viwanda 4,000 vimejengwa tangu Serikali ya awamu ya 5 iingie madarakani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279

Aveline Kitomary, Dar es salaam

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, viwanda vipya zaidi ya 4,000 vimejengwa na hivyo kufanya sekta hiyo kuchangia Pato la Taifa kwa asilimia 8.05 na kutoa ajira 306,180 mwaka 2018.

Akizungumza kwa niaba ya Rais John Magufuli jana Dar es Salaam, wakati wa utoaji wa tuzo za Rais kwa wazalishaji bora wa viwandani (PMAYA) mwaka 2018 alisema kutokana na sekta hiyo kuwa na mchango mkubwa, Serikali itavipa kipaumbele viwanda vinavyotumia malighafi za ndani zaidi.

Tuzo hizo ambazo zimeandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) ilishirikisha makampuni 61 ambapo mshindi wa jumla ilikuwa ni kampuni ya Hanspaul iliyoko mkoani Arusha.

“Sekta ya viwanda imeendelea kuongeza pato la taifa na mwaka 2018 imeongezeka kwa asilimia 8.05 tofauti na mwaka 2017 ambao ilikuwa asilimia 7.67, Aidha, katika kipindi cha mwaka 2018 Sekta ya viwanda ilichangia asilimia 18.1 ya mauzo yote ya nje, ikilinganishwa na asilimia 15 mwaka 2017 pia, takwimu zinaonyesha kwamba katika mwaka 2018 Sekta ya viwanda imetoa ajira rasmi 306,180 ikilinganishwa na ajira 280,899 mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia 9.

“Mkakati wetu wa kuendeleza viwanda nchini kipaumbele kimewekwa katika viwanda ambavyo vinatumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini, tunahitaji kupunguza uuzaji wa mazao yetu ya kilimo, misitu, madini na maliasili nje ya nchi yetu yakiwa ghafi, hali kadhalika tunalenga kutumia rasilimali zilizopo nchini kuzalisha bidhaa ambazo hivi sasa tunaziagiza kutoka nje.

“Shabaha yetu ni kutosheleza mahitaji ya ndani ya bidhaa za viwandani, na kuwa na ziada tutakayouza nje ya nchi ili kupata fedha za kigeni, kukuza ajira na kuongeza kipato cha Watanzania kwa ujumla,yote haya yatawezekana kama tutatengeneza miundombinu kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa bora,”alisema Majaliwa.

Alisema ili kufikia lengo la kuwa nchi ya kipato cha kati inayoongozwa na uchumi wa viwanda Serikali haina budi kuhahakikisha ukuaji wa uchumi unafikia asilimia 12 kwa mwaka.

“Ikiwa ni mchango wa viwanda katika Pato la Taifa usiopungua asilimia 15,utoaji wa ajira rasmi na za moja kwa moja uongezeke na kufikia asilimia 40 ya ajira zote; na,pia ni muhimu sekta ya viwanda iweze kuiingizia nchi mapato ya fedha za kigeni zaidi ya asilimia 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni,”alieleza.

Aidha alisema kuwa serikali inaendelea kutatua changamoto zinazoikumba na kurudisha sekta ya viwanda nchini kwa kushirikiana na sekta ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya kufanya biashara.

Aidha Waziri Majaliwa alimpongeza Subhash Patel kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa CTI pamoja na wadhamini waliojitokeza kudhamini tuzo hizo.

“Kuchaguliwa kwako ni ishara tosha kwamba Wanachama wa CTI wanakupenda na wanatambua mchango wako mkubwa katika sekta ya viwanda pamoja na uwezo na uzoefu wako wa muda mrefu wa kusimamia masuala ya viwanda nchini,” alisema.

Kwa upande wake mshindi wa jumla wa tuzo hiyo Satbir Singh alitoa ushauri hasa kwa vijana ambao wanamalengo ya kuanzisha viwanda wawe na uthubutu.

“Kila kitu ni uthubutu na kutokukata tamaa ni muhimu kila mtu apambane kuhakikisha anafanikisha ndoto zake au malengo yake kwahiyo nawaambia hasa vijana wasikate tamaa katika wakati mgumu wa biashara wanaopitia kila kitu ni uvumilivu na uthubutu,”alisema Singh
 
Izo propaganda akawaambie uko lumumba

Utoto Mingine Bwana ivi waziri mkuu anajua output ya idadi ya ajira ambazo zingetokea kuanzia skilled labour na unskiled labour uko mtaani kwa viwanda ata 2000 vijana wangekuwa busy kiasi gani?

As the nation i think we are stupid.
 
Vinatengeneza bidhaa gani? Maana hata ukiangalia Hapo ulipo, ni vitu gani vya Tanzania? Angalia nguo ulizovaa, kiti ulichokalia, na mambo mengi mengine halafu angalia vitu vya Tanzania vinavyotokana na viwanda vyetu, kwa hakika ni vichache sana. Viwanda siyo propaganda inabidi vionekane, bidhaa zionekane na ajira zionekane pia.
 
Vipo vingi mkuu ngoja nianze na hivi vichache na kama tunavyojua kazi ya kiwanda izalishe bidhaa then iuzwe pesa ipatikane sasa hapa nakuletea viwanda vilivyozalisha pesa nyingi kwa ujanja na weledi wa hali ya juu wa awamu ya 5.

1.Viwanda vya kununua wapinzani(Madiwani na wabunge),hivi vilianzishwa kuanzia mwaka 2017 mpaka sasa vinaendelea.

2.Viwanda vya wahujumu uchumi(DPP bado anaendelea kukusanya mapato)

3.Viwanda vya utekaji(Mo alikamuliwa mabilioni)

4.Viwanda vya kubambika kodi(endelevu)

5.Viwanda vya 1.5 trilioni kilichoibuliwa na Polepole ooh sorry CAG

6.Kiwanda cha chatooo kule linalopaki Drimu la aina

7.Viwanda vya kuwapa watu kesi ya madawa ya kulevya kisha baadae wakatoa hela kesi zikaisha.

Nk viko ving vingine mtanisaidia
Hivi wanajenga wapi hivi viwanda? Nimesafiri mikoa yote sioni hivyo vitu. Mwenye location, please,comment fupi fupi.
 
Majina ya viwanda na orodha naisubiria kwa hamu
Nadhani tungekuwa na kiwanda kimoja au viwili tungekuwa mbali sana. Tungeomba TOYOTA au VW waje kuitengeneza magari hapa, au japo kuhamishia nusu ya viwanda vyao tungekuwa mbali sana.... inawezekana kuna mgongano wa tafsiri ya hili neno kiwanda. Kwa tafsiri ya jadi, kiwanda kimoja sio rahisi kuwa nacho kwa mwaka mmoja kwa nchi yenye uchumi kama Tanzania.
 
Vipo vingi mkuu ngoja nianze na hivi vichache na kama tunavyojua kazi ya kiwanda izalishe bidhaa then iuzwe pesa ipatikane sasa hapa nakuletea viwanda vilivyozalisha pesa nyingi kwa ujanja na weledi wa hali ya juu wa awamu ya 5.

1.Viwanda vya kununua wapinzani(Madiwani na wabunge),hivi vilianzishwa kuanzia mwaka 2017 mpaka sasa vinaendelea.

2.Viwanda vya wahujumu uchumi(DPP bado anaendelea kukusanya mapato)

3.Viwanda vya utekaji(Mo alikamuliwa mabilioni)

4.Viwanda vya kubambika kodi(endelevu)

5.Viwanda vya 1.5 trilioni kilichoibuliwa na Polepole ooh sorry CAG

6.Kiwanda cha chatooo kule linalopaki Drimu la aina

7.Viwanda vya kuwapa watu kesi ya madawa ya kulevya kisha baadae wakatoa hela kesi zikaisha.

Nk viko ving vingine mtanisaidia
Dah! Ila nyie watu! Watanzania huwa nawaona wa kimya, kumbe!
 
Mkipata definition ya kiwanda mni beep. Huwezi kubishana bila kujua hilo kwanza, mleta mada tuweke sawa.
 
Labda viwanda vya kufyatua watoto.

Aveline Kitomary, Dar es salaam

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, viwanda vipya zaidi ya 4,000 vimejengwa na hivyo kufanya sekta hiyo kuchangia Pato la Taifa kwa asilimia 8.05 na kutoa ajira 306,180 mwaka 2018.

Akizungumza kwa niaba ya Rais John Magufuli jana Dar es Salaam, wakati wa utoaji wa tuzo za Rais kwa wazalishaji bora wa viwandani (PMAYA) mwaka 2018 alisema kutokana na sekta hiyo kuwa na mchango mkubwa, Serikali itavipa kipaumbele viwanda vinavyotumia malighafi za ndani zaidi.

Tuzo hizo ambazo zimeandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) ilishirikisha makampuni 61 ambapo mshindi wa jumla ilikuwa ni kampuni ya Hanspaul iliyoko mkoani Arusha.

“Sekta ya viwanda imeendelea kuongeza pato la taifa na mwaka 2018 imeongezeka kwa asilimia 8.05 tofauti na mwaka 2017 ambao ilikuwa asilimia 7.67, Aidha, katika kipindi cha mwaka 2018 Sekta ya viwanda ilichangia asilimia 18.1 ya mauzo yote ya nje, ikilinganishwa na asilimia 15 mwaka 2017 pia, takwimu zinaonyesha kwamba katika mwaka 2018 Sekta ya viwanda imetoa ajira rasmi 306,180 ikilinganishwa na ajira 280,899 mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia 9.

“Mkakati wetu wa kuendeleza viwanda nchini kipaumbele kimewekwa katika viwanda ambavyo vinatumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini, tunahitaji kupunguza uuzaji wa mazao yetu ya kilimo, misitu, madini na maliasili nje ya nchi yetu yakiwa ghafi, hali kadhalika tunalenga kutumia rasilimali zilizopo nchini kuzalisha bidhaa ambazo hivi sasa tunaziagiza kutoka nje.

“Shabaha yetu ni kutosheleza mahitaji ya ndani ya bidhaa za viwandani, na kuwa na ziada tutakayouza nje ya nchi ili kupata fedha za kigeni, kukuza ajira na kuongeza kipato cha Watanzania kwa ujumla,yote haya yatawezekana kama tutatengeneza miundombinu kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa bora,”alisema Majaliwa.

Alisema ili kufikia lengo la kuwa nchi ya kipato cha kati inayoongozwa na uchumi wa viwanda Serikali haina budi kuhahakikisha ukuaji wa uchumi unafikia asilimia 12 kwa mwaka.

“Ikiwa ni mchango wa viwanda katika Pato la Taifa usiopungua asilimia 15,utoaji wa ajira rasmi na za moja kwa moja uongezeke na kufikia asilimia 40 ya ajira zote; na,pia ni muhimu sekta ya viwanda iweze kuiingizia nchi mapato ya fedha za kigeni zaidi ya asilimia 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni,”alieleza.

Aidha alisema kuwa serikali inaendelea kutatua changamoto zinazoikumba na kurudisha sekta ya viwanda nchini kwa kushirikiana na sekta ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya kufanya biashara.

Aidha Waziri Majaliwa alimpongeza Subhash Patel kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa CTI pamoja na wadhamini waliojitokeza kudhamini tuzo hizo.

“Kuchaguliwa kwako ni ishara tosha kwamba Wanachama wa CTI wanakupenda na wanatambua mchango wako mkubwa katika sekta ya viwanda pamoja na uwezo na uzoefu wako wa muda mrefu wa kusimamia masuala ya viwanda nchini,” alisema.

Kwa upande wake mshindi wa jumla wa tuzo hiyo Satbir Singh alitoa ushauri hasa kwa vijana ambao wanamalengo ya kuanzisha viwanda wawe na uthubutu.

“Kila kitu ni uthubutu na kutokukata tamaa ni muhimu kila mtu apambane kuhakikisha anafanikisha ndoto zake au malengo yake kwahiyo nawaambia hasa vijana wasikate tamaa katika wakati mgumu wa biashara wanaopitia kila kitu ni uvumilivu na uthubutu,”alisema Singh
 
Sasa Tanzania tuna viwanda vingi kuliko Ujerumani ambayo ina viwanda 2600 tu huku Tanzania ikiwa na viwanda zaidi ya 4000, tena vimejengwa kwa miaka 4 tu huku vya Ujerumani vikijengwa kwa miaka zaidi ya 200.

Nashangaa kwa nini hatujawa dona kantri.
 
Back
Top Bottom