Waziri mkuu anunua hisa za vodacom kwa Milioni 10

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,641
11,956
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mh; Kassim Majaliwa leo amejiunga na wananchi katika ununuzi wa hisa za Vodacom. Kwa siasi cha sh milioni 10. Waziri Mkuu amesema amemnunulia mkewe hisa hizo.

Aidha Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwataka watanzania kuona umuhimu na faida za ununuzi wa hisa bila kuwa na mashaka yoyote. Na kuwahakikishia usalama wa pesa zako.

Chanzo: TBC.
 
ni kweli nami imeona kupitia Clouds TV, Milioni 10 inaweza kuwa kama buku ten kwao, ila kwetu walalahoi ni fedha nyingi sana. sikuona haja yoyote ya kujitangaza kwa PM kununua hisa za VD, labda matangazo kuwashawishi na wengine
 
Humphrey Polepole ana maana gani juzi kusema kwamba "azimio la arusha bado linaishi na hata katiba ya nchi na ya Chama inatambua hilo?" Moja ya nguzo zake Kuu ni miiko ya uongozi ambapo pamoja na mengine inasema ni marufuku kwa "Viongozi kuwa na hisa katika Makampuni binafsi".

Hakika hakuna wakati mbaya kuwa mwana CCM kama leo kwani kinachoendelea ni "trickle down insanity."

MsemajiUkweli, Ritz, Kobello, ZeMarcopolo, Kobello, Waberoya, Gamba la Nyoka, Nguruvi3, Mag3
 
Safi sana majaliwa.Uwekezaji wa ndani ndio unaotakiwa badala ya kuwekeza pesa nje ya nchi
 
Heko Mh Waziri Mkuu kwa kununua hisa za Tsh 20,000,000/-. Kupanga ni kuchagua.
 
wazimu huo ww nenda katose mil zako harafu mwisho wa mwezi wanakwambia
Umepokeq gawio la 1000 kutoka vodacom

HAHHAHAHA WE NTAINGIA VODA OFSINI KWAO KAMA BABA UBAYA JEMBE SURURU SHOKA MSHALE VYOTE VITAUSIKA SIKU HIYO
 
Humphrey Polepole ana maana gani juzi kusema kwamba "azimio la arusha bado linaishi na hata katiba ya nchi na ya Chama inatambua hilo?" Moja ya nguzo zake Kuu ni miiko ya uongozi ambapo pamoja na mengine inasema ni marufuku kwa "Viongozi kuwa na hisa katika Makampuni binafsi".

Hakika hakuna wakati mbaya kuwa mwana CCM kama leo kwani kinachoendelea ni "trickle down Insanity."
Huo uongozi anakaa nao miaka mingapi? Tafuta hela kawekeze acha manung'uniko ya kipuuzi. Kama yeye kwa uwezo wake kawekeza 10m wee unakosa hata Elfu 80, ya kuwekeza? Kama ishu huoni umuhimu wake kufanya kwa maisha yako ya baadae usiwaonee kijicho wanaoamua kufanya
 
Humphrey Polepole ana maana gani juzi kusema kwamba "azimio la arusha bado linaishi na hata katiba ya nchi na ya Chama inatambua hilo?" Moja ya nguzo zake Kuu ni miiko ya uongozi ambapo pamoja na mengine inasema ni marufuku kwa "Viongozi kuwa na hisa katika Makampuni binafsi".

Hakika hakuna wakati mbaya kuwa mwana CCM kama leo kwani kinachoendelea ni "trickle down Insanity."
Ww kaa kizembe usubirie masuala ya azimio tu,wenzako wanapiga mpunga,usiamini wanasiasa,tembea na gap ufanye maisha.zubaa tu,wenzako wananeemeka
 
Ww kaa kizembe usubirie masuala ya azimio tu,wenzako wanapiga mpunga,usiamini wanasiasa,tembea na gap ufanye maisha.zubaa tu,wenzako wananeemeka
Kwanini Humphrey Polepole anadanganya wana ccm na wananchi kwa ujumla?
 
Kwanini Humphrey Polepole anadanganya wana ccm na wananchi kwa ujumla?
Usiamini wanasiasa,polepole alitafuta fursa kapata,saiv anakula kuku kwanza,akifulia ndio utamuona akijiita mzalendo wa katiba ya warioba,ha ha haa
 
Back
Top Bottom