Kwa sasa katiba ya nchi inasema chama kinachoshinda ndio kinaunda serikali, so waziri mkuu atatoka chama kitakachoshinda!
SEHEMU YA TATU
WAZIRI MKUU, BARAZA LA MAWAZIRI
NA SERIKALI
Waziri Mkuu
51.-(1) Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
atakayeteuliwa na Rais kwa kufuata masharti ya ibara hii na
ambaye kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Rais
kwa kiapo kinachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwa
na Bunge.
(2) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku
kumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua
Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi
anayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi
Bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye Wabunge
wengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na Wabunge walio
wengi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika
madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa
na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabunge
walio wengi.
(3) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, Waziri
Mkuu atashika kiti cha Waziri Mkuu hadi(
a) siku ambapo Rais mteule ataapa kushika kiti chake;
au
(b) siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka; au
(c) siku atakapojiuzulu; au
(d) siku Rais atakapomteua Mbunge mwingine kuwa
Waziri Mkuu; au
(e) atakapoacha kushika kiti cha Waziri Mkuu kwa mujibu
wa masharti mengineyo ya Katiba hii.