Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,899
FEBRUARI 10 mwaka huu, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alipindisha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007) kwa lengo la kubembeleza urafiki wa Kaizari, kati yake na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Jambo hili lilitokea baada ya Mbunge wa Arusha, Godbless Lema (CHADEMA), kuomba apewe mwongozo wa spika kuhusu utaratibu aliohisi unakiukwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda, wakati akitoa maelezo kuhusu vurugu zilizotokea jijini Arusha Januari 5, mwaka huu.
Pinda alizungumzia vurugu hizo za Arusha wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, aliyetaka kujua serikali ina msimamo gani kuhusu mauaji ya raia yaliyofanywa na Jeshi la Polisi wakati wa vurugu hizo.
Akijibu swali la Mbowe, Pinda alilieleza Bunge kwamba chanzo asilia cha vurugu hizo ni uamuzi wa madiwani wa CHADEMA kutokubali kushindwa katika uchaguzi wa umeya mjini Arusha, wakati utaratibu uliofuatwa katika kumpata meya na naibu wake ni sahihi kabisa, kwa maana kwamba Meya wa Arusha yupo kihalali.
Kufuatia kauli hiyo na zingine zinazofanana nayo, Godbless Lema aliomba mwongozo wa Spika kuhusu utaratibu wa hatua zinazoweza kuchukuliwa na mbunge wa kawaida endapo kiongozi mkubwa wa nchi kama Waziri Mkuu amelidanganya Bunge.
Baada ya kuombwa mwongozo huo, Spika Makinda hakuutoa. Badala yake, Spika Makinda alisema: Bunge letu hili lazima liwe na adabu ya hali ya juu; waziri mkuu na ahadi yake aliyoiweka ndani ya Bunge hili anaweza kulidanganya?
Kisha, Spika alimpa siku tatu Lema ili awasilishe kwa maandishi utetezi wake wa kuthibitisha kwamba waziri mkuu alisema uongo bungeni siku hiyo.
Katika muktadha huu, tunakusudia kufanya mambo mawili. Kwanza ni kuonyesha kwamba ni kweli kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema uongo bungeni ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya.
Na pili tunataka kuonyesha kwamba, kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Spika Makinda hakumtendea haki Godbless Lema.
Waziri Mkuu alisema uongo: Meya wa Arusha si halali
Kwa lengo la kuonyesha kwamba Waziri Mkuu alisema uongo bungeni, inatosha kutoa ushahidi utakaokanusha usemi ufuatao kama ulivyotolewa naye bungeni: Kwamba, Utaratibu uliofuatwa katika kumpata meya na naibu wake ni sahihi kabisa, kwa maana kwamba Meya wa Arusha yupo kihalali.
Hapa inatosha kabisa kuonyesha kwamba miongoni mwa wajumbe waliompigia kura ya ndiyo Meya wa Arusha, yupo angalau mjumbe mmoja ambaye hakuwa na haki ya kisheria ya kuingia na kupiga kura hiyo. Na huyo si mwingine, bali ni Mary Pius Chatanda, ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Mkoa wa Tanga. Utetezi unafuata.
Kwa mujibu wa ibara ya 19(2) ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) (Local Governments (Urban Authorities) Act) ya mwaka 1982, kama ilivyofanyiwa marekebisho bungeni mwaka 2006, Mary Pius Chatanda atakuwa ni mjumbe mwenye sifa ya kisheria ya kupiga kura katika vikao vya Manispaa ya Arusha kama atatimiza sifa mojawapo kati ya sifa tano zifuatazo:
Kwanza, lazima awe ni miongoni mwa madiwani ambao ni wajumbe waliochaguliwa katika kata zilizomo katika Manispaa [ya Arusha] (Tazama ibara ya 19(2)(a)). Chatanda hakuwa miongoni mwa madiwani ambao ni wajumbe waliochaguliwa katika kata zilizomo katika Manispaa [ya Arusha]. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa meya wa Arusha.
Pili, lazima awe ni mbunge anayeliwakilisha jimbo la uchaguzi ambamo manispaa [ya Arusha] inapatikana (Tazama ibara ya 19(2)(b)). Chatanda hakuwa mbunge anayeliwakilisha jimbo la uchaguzi ambamo manispaa [ya Arusha] inapatikana. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.
Tatu, lazima awe ni Mbunge wa Taifa aliyechaguliwa (na chama) kutoka katika mkoa ambamo Manispaa [ya Arusha] inapatikana na kwa mpigo awe ni mkazi ndani ya eneo la manispaa [ya Arusha] (Tazama ibara ya 19(2)(c)). Chatanda hakuwa Mbunge wa Taifa aliyechaguliwa (na chama) kutoka katika mkoa ambamo Manispaa [ya Arusha] inapatikana. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.
Nne, lazima awe ni Mbunge wa Taifa aliyeteuliwa na Rais na kwa mpigo awe ni mkazi ndani ya eneo la manispaa [ya Arusha] (Tazama ibara ya 19(2)(d)). Chatanda hakuwa Mbunge wa Taifa aliyeteuliwa na Rais. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.
Na tano, lazima awe ni miongoni mwa wajumbe wasiozidi watatu [waliochaguliwa] na Waziri wa TAMISEMI ambaye katika uteuzi wake [amezingatia] makundi maalumu kama vile watu wenye ujuzi maalum, watu waliotelekezwa na watu walio katika mazingira magumu. (Tazama ibara ya 19(2)(e)). Chatanda hakuwa miongoni mwa wajumbe wasiozidi watatu [waliochaguliwa] na Waziri wa TAMISEMI. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.
Hivyo basi, Kwa mujibu wa ibara ya 19(2) ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) ya mwaka 1982, kama ilivyofanyiwa marekebisho bungeni mwaka 2006, Mary Pius Chatanda hakuwa na sifa yoyote ya kisheria ya kuingia katika kikao cha Manispaa ya Arusha na kupiga kura kama alivyofanya. Baraka za chama chake haziwezi na hazipaswi kubatilisha sheria za nchi.
Tena tusifananishe uwepo wa Mary Pius Chatanda na uwepo wa Rebecca Mngodo katika kikao kilichofanya uchaguzi wa Meya wa Arusha. Kufanya hivyo ni kufananisha maembe na machungwa. Mngodo ni mbunge viti maalumu aliyepatikana kupitia mkoa wa Arusha kupitia CHADEMA. Na hatimaye alipangiwa kazi na chama chake kufanyia kazi katika Mkoa wa Arusha. Kwa hiyo alikuwa na sifa zote za kisheria za kuwemo katika kikao kile.
Spika Makinda hakumtendea haki Godbless Lema
Na sasa, tuone ni kwa nini Spika Makinda hakumtendea haki Godbless Lema. Kabla ya spika kumnyima mwongozo kuhusu utaratibu wa kikanuni, spika alipaswa kufanya tafakari kadhaa kuhusu Katiba, Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi yetu.
Kwanza, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa Ibara ya 52(1) ya Katiba ya nchi, Waziri Mkuu (Mizengo Pinda) ni msimamizi mkuu wa shughuli zote za siku hadi siku zinazofanywa na vyombo vya dola katika Jamhuri nzima. Pili, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa Ibara ya 52(2) ya Katiba ya nchi, Waziri Mkuu (Mizengo Pinda) ni Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni.
Tatu, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa Ibara ya 62(2) na 66(1) za Katiba ya nchi, Waziri Mkuu (Mizengo Pinda) ni mjumbe halali katika vikao vya bunge kupitia kofia yake kama mbunge wa kuchaguliwa.
Nne, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(1) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Waziri Mkuu (Mizengo Pinda), kama ilivyo kwa Mbunge mwingine yeyote, anapokuwa akisema bungeni ana wajibu wa kuhakikisha kwamba anatoa kauli au maelezo kuhusu jambo au suala ambalo yeye mwenyewe anaamini kuwa ni la kweli na siyo jambo la kubuni au la kubahatisha tu.
Tano, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(3) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), mbunge mwingine yeyote (kama vile Godbless Lema) anaweza kusimama mahali pake na kuomba mwongozo kuhusu utaratibu uliokiukwa bungeni; na kwamba baada ya kuruhusiwa na Spika, anaaweza kudai kwamba, Mbunge aliyekuwa anasema kabla yake (kama vile Mizengo Pinda) ametoa maelezo ya uwongo kuhusu jambo au suala alilokuwa analisema bungeni.
Sita, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(4) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), mbunge anayeomba mwongozo kuhusu utaratibu uliokiukwa bungeni (kama vile Godbless Lema alivyofanywa), atakuwa na wajibu wa kutoa na kuthibitisha ukweli kuhusu jambo au suala hilo kwa kiwango cha kuliridhisha Bunge.
Saba, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(5) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Spika au Mbunge mwingine yeyote (kama vile Godbless Lema), baada ya kutoa maelezo mafupi ya ushahidi unaotilia mashaka ya dhahiri kuhusu ukweli wa kauli juu ya jambo ambalo mbunge mwingine (kama vile Mizengo Pinda) amelisema Bungeni, anaweza kumdai Mbunge huyo (Mizengo Pinda), ambaye kauli yake inatiliwa shaka, atoe uthibitisho wa ukweli wa kauli yake na kama atashindwa kufanya hivyo, afute maelezo yake hayo.
Nane, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(6) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Mbunge aliyetakiwa kuthibitisha ukweli wa kauli au usemi au maelezo yake aliyoyatoa Bungeni (Mizengo Pinda), atawajibika kutoa uthibitisho huo kwa kiwango cha kuliridhisha Bunge, papo hapo au katika muda atakaopewa na Spika kwa ajili ya kufanya hivyo.
Tisa, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(7) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), endapo Mbunge aliyetakiwa kuthibitisha kauli au usemi au maelezo yake aliyoyatoa Bungeni (Mizengo Pinda) atashindwa kufanya hivyo, anaweza kujirekebisha kwa kufuta kauli au usemi au maelezo yake hayo, papo hapo au katika muda atakaokuwa amepewa na Spika kwa ajili ya kuthibitisha kauli au usemi au maelezo yake.
Na kumi, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(8) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), endapo hadi kufikia mwisho wa muda aliopewa, Mbunge aliyetakiwa kutoa uthibitisho wa ukweli wa kauli yake aliyoitoa bungeni (Mizengo Pinda) atakataa au atashindwa kutoa uthibitisho huo kwa kiwango cha kuliridhisha Bunge, na kama atakataa kujirekebisha kwa kufuta kauli au usemi au maelezo yake, basi Spika atamwadhibu kwa kumsimamisha Mbunge huyo (Mizengo Pinda) asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi vitano.
Hivyo ndivyo Kanuni za Kudumu za Bunge (2007) zinavyosomeka. Na huu ndio mwongozo aliopaswa kuutoa Spika Makinda. Lakini, baada ya kuombwa mwongozo husika, Spika Makinda hakuutoa. Badala yake, akaona kwamba ombi hilo ni utovu wa adabu wa hali ya juu.
Kwa maneno yake mwenyewe, Spika alisema, Bunge letu hili lazima liwe na adabu ya hali ya juu; Waziri Mkuu na ahadi yake aliyoiweka ndani ya Bunge hili anaweza kulidanganya? Kwa hakika, lazima hapa tukubaliane kwamba spika alipindisha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007) kwa lengo la kubembeleza urafiki wa Kaizari kati yake na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Aliombe radhi Bunge na taifa kwa ujumla.
Source: Tanzania daima