Waziri mkuu akunjua makucha Shinyanga

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
aagiza watumishi walio iba hela katika halmashauri ya kishapu shinyanga wakamatwe. halimashauri amesema halmashauri ina sifa mbaya za ubadhilifu wa mali za uma. ameyasema hayo alipokuwa anafungua jengo kishapu. source rfa.
MY TAKE;
Sina uhakika kama kweli hao mafisadi wa Shinyanga watakamatwa. kwani si mara ya kwanza serikali inatoa maagizo bila utekelezaji wowote. kama ikitokea utakuwa mfano wa kuigwa.
 
Amekunjua makucha kama yale aliyokunjulia madaktari au siku hizi anatumia hadi ya miguu kwa sababu mikononi hana makucha yalikatwa na madaktari
 
nani analikumbuka VUVUZELA, lol, wazungu mwanzoni walidhani vuvuzela litasaidia ushindi kwa team za Afrika, hahaaah kumbe debe tupu haliachi kutima hilo,

59070_148259301874784_100000721457505_296399_438627_n.jpg
 
Hiyo ni danganya toto unakumbuka aliwapiga biti madr?mwisho wa siku akaishia kuwaomba msamaha nakuwasihi warudi kazini.
 
Machozi hayakumtoka wakati anakunjua makucha? Maana kukunjua makucha uchungu kweli, hadi machozi ya damu yanatoka!
 
Nchi hii kwa sasa hatuna waziri mkuu, raisi na makamu wa raisi. kwa ufupi kabisa nchi haina uongozi kila mtu anafanya atakalo......
 
Ni lini amekuwa na hayo makucha Bro? Angekuwa nayo angekuwa na ujasiri wa Tai, kurarua mawindo yake kwa uhakika na bila hofu. Lakini baba huyu hana hata ujasiri wa kunguru kunyakua kifaranga cha kuku.
 
Nchi hii kwa sasa hatuna waziri mkuu, raisi na makamu wa raisi. kwa ufupi kabisa nchi haina uongozi kila mtu anafanya atakalo......

Mimi siku hizi wala simsikilizi tena, amekwisha poteza uhalali wa kuwa kiongozi tangu alipo chemsha kwa issues za madaktari na walemavu wa ngozi. Mwenyezi MUNGU atusaidie tufike 2015 tutakapopata fursa ya kuwa na viongozi tunaowataka.
 
Mmmmmmmhhh! labda ngoja tusubili tuone! huenda safari hii atamanisha!
 
Nchi hii kwa sasa hatuna waziri mkuu, raisi na makamu wa raisi. kwa ufupi kabisa nchi haina uongozi kila mtu anafanya atakalo......
mpeleke mama yako akatuongoze basi. mijitu mingine sijiu yanafikiria kwa kutumia kiungo gani!
 
mpeleke mama yako akatuongoze basi. mijitu mingine sijiu yanafikiria kwa kutumia kiungo gani!

Si uungwana kumjibu mwenzio mitusi ya namna hiyo. Hata km wew ni Gamba uwe mstaarabu. Mana unamshangaa kuwa anafikiria kwa kutumia kiungo gani wakati nawe ni walewale kutokana na majibu yako. Ustaarabu hauuzwi ni suala la kuamua tu.
 
aagiza watumishi walio iba hela katika halmashauri ya kishapu shinyanga wakamatwe. halimashauri amesema halmashauri ina sifa mbaya za ubadhilifu wa mali za uma. ameyasema hayo alipokuwa anafungua jengo kishapu. source rfa.
MY TAKE;
Sina uhakika kama kweli hao mafisadi wa Shinyanga watakamatwa. kwani si mara ya kwanza serikali inatoa maagizo bila utekelezaji wowote. kama ikitokea utakuwa mfano wa kuigwa.

Msanii tu huyu!!! Hana jipya. Alishindwa kuwakamata mafisadi wa EPA, Meremeta na Kagoda kwa kudai kwamba mafisadi wa EPA ni matajiri wakubwa nchini hivyo wakikamatwa nchi itawaka moto. Na akazuia mjadala wa ufisadi wa $155 millioni Meremeta kwa kisingizio kwamba kuna siri za Serikali hivyo hawezi kuruhusu mjadala huo ufanyike bungeni. Kagoda ndio hata neno hajatia. Kama alivyo Boss wake hastahili kuwa na wadhifa wowote huyu Serikalini kutokana na usanii wake.

Back
Top Bottom